zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Zomba ni kweli, wabunge wanachota millioni 10 kwa mwezi sasa...Halafu inashangaza sisi wananchi tunaendelea kupiga makelele CCM Oyee, Chadema Oyee, CUF Oyee wakati hawa watu hakika hawana maana kabisa wala Uzalendo rohoni mwao wakiendesha hoja bungeni za mgomo, Dr.Ulimboka, Muungano na madudu mengine kutupoteza sisi wananchi kuelewa kilichofanyika..
I mean sasa hivi naanza kukosa kabisa imani ya hawa viongozi wetu wote! mtanisamehe viongozi wangu lakini hii sii kupigania haki wala M4C - I think time has come kwetu sisi wananchi kuchukua jukumu hilo maanake nilisikia mpango huu mapema kwamba badala ya kuongeza posho zilizokataliwa, wafanye ongezeko la mshahara wao na imekuwa. Huu ni mpango wa CCM baada ya mgomo wa kwanza wa madaktari, kuwaonyesha wananchi kwamba hao Chadema mnaowatetea sana mbona nao wanachukua mishahara mikubwa?. Mbona nao wanafanya yale yale maduidu ya CCM?.. Nikajiuliza sana lakini nikasema Chadema hawatakubali hili.. Heee kumbe wamejaa tele leo hii nao wamejitikwa zigo la ndizi kichwani wakati wanajua fika sii wabunge wanaotakiwa kutekeleza maendeleo majimboni bali Halmashauri zao. Kwa taarifa yenu hili swala litaibuka wakati wa Uchaguzi na Chadema mtashindwa kujitetea kwa wananchi.
Hili ongezeko kiuhalisia lilitakiwa kuongezwa ktk Halamshauri za majimbo yao maana wabunge wengi wanafanya kazi za Halamshauri ili kujenga majina yao wakati sii jukumu lao kutumia madai haya haya ya ongezeko la mshahara au posho zao. Mimi naomba viongozi wa Chadema walioko hapa janvini, watupe majibu ya swala hili hapa hapa JF maana wanatembelea sana. Hii habari ya sisi kushabikia vitu nadhani huu utakuwa mwisho wake, wengine hatuwezi kuwa bendera.
Kama serikali yetu inavyofanywa ombaomba na nchi matajiri ndivyo nao wana imani ya kuchukua kodi zetu halafu wanadai kwamba wanatusaidia bila fedha hawawezi kumudu maisha na sijui kutoa misaada majimboni. Nani kawambia tunahitaji misaada badala ya ujenzi wa nchi kwa kodi zetu?.. Fedha yetu inangia kwao mfuko mmoja inatoka mfuko mwingine wakidai ni uwezo wao?.. Itafika wakati mbunge atakuwa kama RC na ndio maana tunajichanganya..Hii haikubaliki kabisa, inaondoa imani zetu kwa hawa viongozi wetu na sasa naanza kurudi nyuma kujitazama upya!..
Si kweli kuwa mshahara wa Wabunge ni million 10 kwa mwezi:
UKWELI KUHUSU MISHAHARA YA WABUNGE
Jun 21st 2012, 17:14
http://1.bp.blogspot.com/-k1RiR2FloJY/T-NV574J6aI/AAAAAAAC9sU/1CBpWOgCxc0/s1600/bu.jpgWakati Bunge liko kwenye mchakato wa Bajeti ya 2012/13, yameanza kujitokeza maneno na taarifa mbalimbali juu ya kupanda kwa mishahara ya watumishi wa Umma wakiwemo Wabunge. Mathalani, siku ya Jumatano tarehe 20 Juni 2012, gazeti moja linatokalo kila siku lilikuwa na habari yenye kichwa kisemacho "Mishahara ya Wabunge juu".
Ofisi ya Bunge imeona ni vyema kutoa ufafanuzi juu ya suala zima la mishahara ya Wabunge ili umma uweze kuelimika ipasavyo juu ya taratibu zinazotawala jambo hili kama ifuatavyo:
· Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo inajumuisha Fungu Na. 42 lenye Bajeti ya Bunge bado haijasomwa Bungeni, na hivyo haiwezekani leo hii kueleza kuwa kuna nyongeza ya bajeti inayohusu mishahara kwa Wabunge.
· Si kweli kwamba mishahara ya Wabunge imeongezwa toka kiwango wanacholipwa sasa, kwa kuwa mishahara yao kama ilivyo ya watumishi wote wa umma, hurekebishwa kwa waraka maalum toka Ofisi ya Rais, na si Kamisheni au Kamati yoyote ya Bunge.
· Waraka wa mwisho wa toka Ofisi ya Rais unaotoa Masharti ya Kazi ya Mbunge ulitolewa tarehe 25 Oktoba 2010, na kueleza kuwa Mbunge atalipwa mshahara katika ngazi ya LSS (P) 2, na ni waraka huo unaotumika mpaka sasa.
· Mapendekezo ya ongezeko la 32% ya Bajeti ya Ofisi ya Bunge yaliyooneshwa kwenye kitabu cha Bajeti namba 2, cha matumizi ya kawaida yaliyowasilishwa mezani ni ya matumizi mengine ambayo hayana uhusiano na ongezeko la mishahara.
Mwisho, Ofisi ya Bunge wakati wote inathamini sana mchango wa vyombo vya habari katika juhudi za kuelimisha umma juu ya kazi za chombo chao cha uwakilishi. Hata hivyo, Ofisi inasikitishwa sana na habari za upotoshaji zinazotolewa kwa lengo la kujenga chuki kati ya Wabunge na watu wanao wawakilisha.
Kwa mantiki hiyo, tunazidi kuwasihi Waandishi waandike habari au makala baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu jambo husika na pale inapobidi waweze kupata ufafanuzi toka Idara husika katika Ofisi ya Bunge, ili kuepuka kuupotosha umma.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941, DODOMA.
21 Juni 2012