Mshahara wa wabunge wapanda mpaka 11,000,000/-

Mshahara wa wabunge wapanda mpaka 11,000,000/-

Mnyika ameshasema sababu za kwanini tumefikishwa hapo? JK anawaogopa wabunge, Pinda ndio amesistiza
 
images

Mheshimiwa Badwel akiwasili mahakamani.

​
Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani Dodoma, Omary Badwel, ambaye anakabiliwa na tuhuma za rushwa, leo alipandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kesi yake kuahirishwa hadi Julai 2 mwaka huu.
 
Yaani wabunge wamepandishiwa mishahara kuwahonga wapitishe budget mbovu? Hii nchi imeuzwa. Tuandamane tuwadai mgao.
 
Kwa hali hii migomo ya wafanyaakzi haitaepukika kamwe, lilobaki ni kwenda kazini, soma magazeti rudi nyumbani ukayasikilizie maumivu ya ugumu wa maisha
 
c c m oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
kidumu chama cha mapinduzi

 
Tuwaombee wauguage wao tu...na sisi aaahhh...hatuhitaji madaktari kama hatuugui.
 
Jinsi ya kutatu hili tatizo ni kupitia kutengeneza katiba ambayo haitawaruhusu wabunge kujiongezea mshahara.

Wakenya walithubutu wakaweza.
Kwao kule wabunge kuanzia mwaka 2013 wakati katiba itaanza kutekelezwa kikamilifu hakuna mbunge ataweza kujadili kujiongeza mshahara; vilevile asipowajibika katika eneo bunge lake, wapiga kura wanauwezo wakufuta saini kadha kumvua ubunge.

Pamoja Tunaweza
 
2015 kuna vijana kibao wazuri wanagombea ambayo kwao itakuwa ndio ajira ya kwanza kwahiyo hata ukiwapa 1,000,000/= bila hata ya marupurupu wanapiga mzingo mpaka asubuhi CDM imeshaanza kuwa andaa kilio ni kwa hao waliozoea mihela mingi
 
Ndio maana huwa sitembelei hili jukwa
Ni full stress
Ndo hongo hiyo waipitishe budget huwaoni wanavyoongea mpaka mapovu yanawatoka kuitetea budget kuwa ni nzuri wakati ni wiki iliyopita tuu walikuwa kwenye hivyo hivyo vyombo vya habari kuiponda
Washakula hongo ya ahadi ya mshahara mnono kwa hiyo hapo ni lazima waongee kwa jazba na hasira kuitetea budget hiyo waliyosema ni mbaya
Na wala hawawajali wananchi waliowatuma ambao madawa, madawati, chakula, miundo mbinu, mfumuko wa bei ni misamiati ambayo ishazoeleka kuwa ni ya shida na mdomoni mwao kama ilivyokuwa enzi za mzee wa megawatt
 
zitto ndo mtafunaji wako na we ndo mmezaji??acha uumin wa kibwatere ushapewa source unataka upigiwe tarumbeta uamin???

Kibwetere huamini kila source ya information. Kuna watu nawaamini, ili wa thibitishe kwa sababu ni wahusika. Una tabia za Kibwetere, kaongee na ndungai, mimi sio saizi yako.

Mnyika hebu thitisha hii taarifa.
 
Mshahara wa wabunge umepanda kutoka Tsh 6,000,000/- kwa mwezi mpaka Tsh 10,000,000/- kwa mwezi mbali na marupurupu mengine!..Hii inakuja ikiwa wadaktari tayari wameshatangaza mgogoro na serikali na kuipa wiki 2 kutimiza madai yao la sivyo watatangaza mgomo mkubwa nchi nzima kuanzia 23/6/2012...
Source: Mtanzania ya leo

"Hatuwezi kutatua matatizo kwa akili ile ile ambayo ilisababisha yawepo"..Mch. Peter Msigwa


....................


Hii kweli ni mbaya sana sana....

Lakini na mbaya mno kwa CCM ...

Maana CDM huwa wanatumia mihela hiyohiyo kuimarisha chama chao!




..........
 
Hapana mshahara wa mbunge haukuwa 6 milioni. Mshahara wa Mbunge kama mshahara ulikuwa 2.5 milioni. Sasa wanapokaa kwenye vikao vya muda mrefu kama hivi sasa ndipo wanafikisha hadi 7 milioni ukichanganya mazagazaga mengine ya mafuta, posho, n.k. Sasa mtoa hoja labda uniambie mshahara umepanda kutoka hiyo 2.5 milioni hadi 10 milioni.
 
Wakati huo Mwalimu analipwa 150000 kwa kuambiwa ualimu ni wito? Hawa wabunge wana akili gani jamani?
 
Ngoja nimtafute Zitto anipe mbinu za kuingia kwenye siasa.
 
Hapo sasa mgomo wa madokta haukwepeki Duh? kwa kazi ipi walipwe hivo? Bunge Dhaifu vile linajadili watu badala ya hoja?
 
Hapana mshahara wa mbunge haukuwa 6 milioni. Mshahara wa Mbunge kama mshahara ulikuwa 2.5 milioni. Sasa wanapokaa kwenye vikao vya muda mrefu kama hivi sasa ndipo wanafikisha hadi 7 milioni ukichanganya mazagazaga mengine ya mafuta, posho, n.k. Sasa mtoa hoja labda uniambie mshahara umepanda kutoka hiyo 2.5 milioni hadi 10 milioni.

Kaka nunua Mtanzania ya leo au mwulize mhariri!
 
Back
Top Bottom