Mshahara wa mwezi May vipi watumishi?

Mshahara wa mwezi May vipi watumishi?

Dadadeki!!!
Huku kitaa (field ) hali imekuwa ngumu na haimithiliki na kitu chochote. Sio mfanyabiashara wala mtumishi serikalini. Vitambi vimeisha. Kwisha kabisa ndembendembe. Suruali hazikai viunoni.
Ukisema hali ngumu zungumzia nafsi yako..kuna watu wana fweza eti. Lolz
 
Inasikitisha then inachekesha...

Maish halisi ya Mtumishi wa Umma.. Anasubiria kwa Shauku mshahara wake Kiduchu wa TGSD/E Wenye makato lukuki.. Take home itabaki laki 4..

Ana familia bado mchepuko unapiga vizinga[emoji23] yaani kila siku maisha yake yataishia kwenye madeni tuu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Maisha ni fumbo gumu sana!Nilijaribu biashara lakini ilifika mahali nikashindwa kulipa pango,kilimo ndio usiseme mazao yaliungua na jua,iliponyesha mvua,hats yaliyosurvive yakafunikwa na maji,nikaamua kuajiriwa bahati nzuri nikapata kazi,leo ni mtihani mwingine kwa vile hakuna anayeweza kutabiri kiongozi amefikiri nini jana!Unaweza kusikia wameanza kutafuta wananchi hewa ndani ya watumishi na ikawa sababu tosha ya kuchelewesha mishahara.Tumwombee rais awe na moyo wa utu ili aguswe na maisha ya watu wa chini kama watumishi wa umma na wakulima.
 
Back
Top Bottom