Mshahara wa Februari

Mshahara wa Februari

53326ceec26cd35ce5f900a1f55daa86.jpg
Si vyema sana ku upload screenshot ambayo imechukua hadi namba za watu hasa nyakati kama hizi za ****
ungeweza ku crop....
 
N
Labda Mahakama kuu itoe tafsiri kama ikiwezekana kwamba mtu aliyekopa kwa makubaliano ya riba asimila kadhaa, je sheria inaruhusu nyongeza ya riba katika kipindi cha LOAN REPAYMENT,yaani katikati ya muda ambao mkopaji analipa, sheria inaruhusu bila ya terms na conditions?
Sasa nani atapeleka huko mahakama kuu hata mahakama za kawaida kama hatutaishia kulalamika tu na ubumbuwazi wetu vichwani
 
Walio tajirika hawakusoma hivyo vitabu.
Yani hapo unamfanya aliye andika hicho kitabu awe tajiri kwa sababu umetoa pesa yako mfukoni na kumchangia huku yeye akikuacha na bla blaa kibao kichwani
Kweli mkuu umenena jambo. Huwa nashangaa sana machinga wanaouza vitabu vyenye kichwa JINSI YA KUWA TAJIRI KWA SIKU KUMI NA NNE. Ukiwaangalia wao hali zao ni bora ya jana, huwa najiuliza kwani hawasomi hivyo vitabu? Daaaaaah
 
Lipeni pesa za bodi kipindi mnaandama na kugoma kudai mikopo mlijua ni bure tena lipeni kama vipi acheni kazi kukopa harusi kulipa matanga leo hii povu linawatoka ilitakiwa hata kulipa muandamane na kugoma kama mlivyofanya huko nyuma
 
Lipeni pesa za bodi kipindi mnaandama na kugoma kudai mikopo mlijua ni bure tena lipeni kama vipi acheni kazi kukopa harusi kulipa matanga leo hii povu linawatoka ilitakiwa hata kulipa muandamane na kugoma kama mlivyofanya huko nyuma
Ni zamu ya bodi ya mkopo kuandana ili walipwe.

Kama unashabikia hili unatia shaka, watu hawashindwi kulipa ila mkataba wa kukopeshwa haukusema makato yatakua 15%
Mkataba ulisema makato ni 8%.
Hili ndilo linalolalamikiwa.

Kama huelewi hilo basi hata chuo hukufika mkuu na utakua unawachukia waliosoma chuo
 
Niwachukie waliosoma chuo kwani wanaleta msosi nyumbani kwangu awamu hii kila mtu atabeba msalaba kivyake kilichopo lipeni pesa za bodi mlikuwa na kihere here sana mnaandamana na kugoma kuishinikiza bodi iwape boom lenu sasa hivi mnalalamika mimi nasema wangekata 25% ni zamu ya serikali kudai pesa zake kwa nguvu kama nyie mlivyokuwa mnaandama kupewa mikopo braza usinichukie acha kazi njoo huku tuendeshe malorry tugombane na wenye nayo achana na serikali wanataka chao
 
Nani aliyekwambia kwamba hatulipi? Au ndo kupenda kushabikia usivyovijua? Tulipokea kwa mkopo na hatuna budi kurudisha kwa taratibu tulizokubaliana, maana ya mkataba ni Maridhiano baina ya mkopa na mkopeshaji...!! Watu wanacholalamikia hapa ni kukiukwa kwa miataba ambao umetuelekeza kulipa 8% na sio maamuzi ya Magu na wenzie ya 15% huu ni ukiukwaji wa mkataba na ni kinyume cha sheria,sema ni vile tu wafanyakazi wa Tanzania vyama vya wafanyakazi vinafanya kazi ya kukilinda chama cha serikali na watu wake hii 15% ingelikua Kenya kungenuka
Kama mkataba umekiukwa si muiburuze serikali mahakamani? sasa mnavyolialia nyuma ya keyboard hapa ndo mtapata haki yenu?
 
Yaani kwa waliokopa nawaonea huruma sana. Hapo ukiinclude tax na madude mengine unakuta karibia 50% ya mshahara wote siyo yako kabla haijakufikia mkononi.

Najua sababu ya kupandisha makato ni ukosefu wa pesa basi, sidhani kama kuna sababu nyingine. Ukimwambia mkubwa pesa hakuna inaitwa polisi kesho yake kwa kosa la uchochezi. Uzuri the truth always comes out one way or the other.
 
Back
Top Bottom