Mshahara wa Februari

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,023
1,315
3ba52620024e0e1cd43d983c87e4ac27.jpg
 
Mbona watumishi wengi kuanzia 2015- kwenda chini Mkataba wao na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ulikuwa ni Kukatwa 8% Sasa hiyo 15% inatoka wapi ni Mkataba Mpya au vipi tena.

Serikali lazima itambue Watumishi wengi
wanamikopo kwenye Taasisi mbalimbali za Kifedha hivyo kupandisha makato kutafanya Watumishi kuishi chini ya Theluthi 1/3 ya mishahara yao hivyo kupunguza tija kazini.

Kwanini hiyo 15% isitumike kwa Waajiriwa wapya kama huko Vyuoni walisaini Mikataba ya 15%.

Vyama vya Wafanyakazi simameni Imara katika hili siyo kukusanya michango mnayokula bila kazi ya maana, nanyi ni majipu tu hamna msaada wowote kwa watumishi. Mishahara haipandi mpo kimya, makato yanaongezeka mpo kimya, sasa mna faida gani kwa Watumishi wa Umma bora mvunje hivyo Vyama ambavyo ni chaka la kumuibia Mtumishi wa Umma.
 
Inaweza kuwa Magu ndiye anayehusika ktk mkakati wa kuikabidhi nchi mikononi mwa chama kingine ili tuone mabadiliko ya kweli, msibeze kila kitu, huu ni mkakati mzuri sana!
Wasiwasi wangu ni juu ya chama gani kipo tayari kupokea kijiti hiki?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom