Uchaguzi 2020 Msemaji wa Serikali, Dkt. Abbas: Suala la CHADEMA kuongeza ubeti wao katika wimbo wa Taifa tumemuachia Msajili wa Vyama vya Siasa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,281
SUALA LA CHADEMA TUMEMUACHIA MSAJILI WA VYAMA

Masuala yote yanayohusu maudhui ya utangazaji kisheria yapo chini ya Waziri mwenye dhamana ya habari, Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 pia imefafanua hilo, Sheria inatungwa lakini Kanuni zinatungwa na Mamlaka inayotekeleza sheria hiyo.

Suala la mabadiliko ya Sheria ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni wadau walishirikishwa, suala la Kanuni hizo kurekebishwa wakati huu wa uchaguzi halihusiani na kitu chochote kuhusu uchaguzi kwani mambo mengine ya nchi lazima yaendelee.

Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 imeruhusu mwanafunzi wa taaluma ya habari kuwa na kitambulisho cha mwanahabari ili asipate shida hata akiwa katika mafunzo yake kwa vitendo.

Vyombo vingi vya habari vya kimataifa havina mitambo hapa nchini hivyo kuna baadhi ya maudhui yanayotolewa na vyombo hivyo yanagusa usalama na maadili ya nchi, lazima nchi tuilinde hivyo kanuni imekuja kuweka uratibu katika eneo hilo.

Si kweli kuwa uhusiano wa kidiplomasia wa Tanzania na nchi nyingine umepungua kutokana na namna ambavyo nchi yetu ilipambana na ugonjwa wa Covid19, uhusiano ni mzuri.

Diplomasia inaongozwa na Kanuni inaitwa "reciprocity",Tanzania haikutajwa katika nchi zilizoruhusiwa kuingiza ndege zao Kenya hivyo kama hatujaruhusiwa basi kwa kipindi hiki nao wapumzike kuja. Kwahiyo sio ugomvi bali ni kanuni ya kidiplomasia.

Rais wetu bado ni Mwenyekiti wa SADC, bado Mabalozi wa nchi zingine wanakuja nchini kwetu na sisi tunaendelea kwenda kwenye nchi zao, bado sisi ni wanachama wa UN pia tuna miradi mingi ambayo tunafanya pamoja na benki kubwa ikiwemo ya AfDB na WB.

Wakati wa Uchaguzi hakuna Sheria yoyote inayosimamisha utekelezaji wake, sheria zipo na zinaendelea kutumika. Suala la CHADEMA kuongeza ubeti wao katika wimbo wa Taifa tumewaachia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wafate taratibu na sheria.
 
-
Diplomasia inaongozwa na Kanuni inaitwa "reciprocity",Tanzania haikutajwa katika nchi zilizoruhusiwa kuingiza ndege zao Kenya hivyo kama hatujaruhusiwa basi kwa kipindi hiki nao wapumzike kuja. Kwahiyo sio ugomvi bali ni kanuni ya kidiplomasia.
-

Naombeni hapo kwenye red tafadhali, Ni present tense au ni past present past participle tense. Yaani nauliza zuio bado lipo ama?
 
Katika kosa la kimataifa litakalo fanywa na viongozi wa ngazi za juu wa ccm ni kutumia kigezo Cha walioshinda Kura za maoni za madiwani na ubunge kupitishwa kupeperusha bendera ya CCM mwaka 2020.Walioshika nafasi zote za juu Kura za maoni ni kundi lililokubalika kwa wajumbe wachache ndani ya CCM kupitia kutoa rushwa na kushinda kura za maoni ,wakipitishwa kugombea na upinzani litakuwa kosa la kihistoria katika uchaguzi mkuu ujao ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom