Msemaji wa Serikali, Dkt. Abbas acha Dharau na Punguza Chuki zako kwa Msemaji wa Simba SC, Haji Manara

Tunaongoza Kundi letu huko CAF CL kwa Alama ( Points ) Saba ( 7 ) mbele ya Klabu Kubwa, Bora na Tajiri ya Al Ahly na Klabu Shindani hasa ya AS Vita Club huku Nyumbani Tanzania tukicheza Viporo vyetu Vinne ( 4 ) tu pia naongoza Ligi Kuu ( VPL ) kwa tofauti ya Alama ( Points ) Saba ( 7 ) mbele ya Timua Timua Makocha Benchi la Ufundi Mabondia FC ( Yanga SC )

Kama una Swali lingine niulize upesi tu.
Sasa gubu la nini?
 
Yuko sawa sababu wanashindwa kutofautisha uweledi kama afisa wa habari na ushabiki,matoke yake ndio kama hayo Manara kila kitu ana kichukulia personal.
Hopeless mkubwa Wewe yuko sawa Leo kwakuwa asiyempenda Haji Manara amekinukisha kwa Rafiki yake na Mshabiki mwenzie wa Yanga SC Mtangazaji Maulid Kitenge wa Wasafi FM, ila Kipindi kile aliyekuwa Msemaji wenu Yanga SC Jerry Muro ( sasa DC Arumeru ) alipokuwa akimdhihaki tena Personally kabisa Haji Manara huyu Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas alikuwa sahihi Kunyamaza na Kutolikemea Kimaadili kama alivyofanya sasa? Mnafiki mkubwa Wewe na Wanafiki wakubwa nyie.
 
Sasa kama hata hujui kuwa huyo ndio katibu mkuu wa wizara ya habari na michezo , tunakusaidiaje, insha ndefu!!!sasa haji manara unaona kweli anachokifanya ni majukumu ya msemaji wa timu?!!kwanza kutokana na kauli zake nyingi zenye utata, kusingekuwa na usimba na uyanga angeshafungiwa kwenye soka!!, ila kutokana na mapungufu yake, itaonekana ameonewa!!
Insha ndefu lakini umeisoma yote tu Pumbavu.
 
Wivu tuu unamsumbua, Manara ni maarufu kuliko yeye na hiyo PhD yake....
Kuna tofauti ya kuwa na umaarufa pamoja na uweledi,yeye analalamika tu sababu ya "tetesi za Simba".

Kuna waandishi wakubwa wa habari wa Skysports,The Guardians wanaandika tetesi za club kubwa duniani,zinazo weza kujiendesha zenyewe bila kutegemea mfuko wa mtu,lkn humsikii afisa wake wa habari akimuattack mwandishi wa habari kwa vitu personal.
 
Hopeless mkubwa Wewe yuko sawa Leo kwakuwa asiyempenda Haji Manara amekinukisha kwa Rafiki yake na Mshabiki mwenzie wa Yanga SC Mtangazaji Maulid Kitenge wa Wasafi FM, ila Kipindi kile aliyekuwa Msemaji wenu Yanga SC Jerry Muro ( sasa DC Arumeru ) alipokuwa akimdhihaki tena Personally kabisa Haji Manara huyu Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas alikuwa sahihi Kunyamaza na Kutolikemea Kimaadili kama alivyofanya sasa? Mnafiki mkubwa Wewe na Wanafiki wakubwa nyie.
Kwa hiyo kwa kuwa Jerry alikosea hata Manara akikosea naye sawa,sasa hizo akili au matope.

Wewe ndiye HOPELESS unayehalalisha kosa la Manara,kisa Jerry Muro alikosea NONSENSE.

Hivi nikuulize Jerry Muro alishawahi kumuattack mwandishi yoyote kwa vitu ambavyo ni personal?.

Hao Manchester,Liverpool,Real Madrid,Ac Milan vilabu vikubwa duniani,wandishi wanaandika sana tetesi kuzihusu hizo club lkn husikii maafisa wao wa habari kuwaattack waandishi kwa vitu personal,mwisho wa siku akitukanwa naye atadai "mnanionea sababu mimi mlemavu",unaanzisha ugomvi wa mawe wakati wewe mwenyewe unaishi nyumba ya vioo.

Atofautishe tu kati ya tofauti ya ushabiki na uweledi,kama nao wandishi wakireact kama afanyavyo yy,atakaye umia ni yeye.

Yeye mtu mgani kishagombana na Shaffih Dauda,Efm na leo hii Maulid wa Kitenge wa Wasafi kwa mambo ambayo haya make sense.Mbona akina Masao Bwire,Kifaru pamoja na kuongea kwao ila huwasikii kuwa attack waandishi kwa vitu personal.
 
Kwa hiyo kwa kuwa Jerry alikosea hata Manara akikosea naye sawa,sasa hizo akili au matope.

Wewe ndiye HOPELESS unayehalalisha kosa la Manara,kisa Jerry Muro alikosea NONSENSE.

Hivi nikuulize Jerry Muro alishawahi kumuattack mwandishi yoyote kwa vitu ambavyo ni personal?.

Hao Manchester,Liverpool,Real Madrid,Ac Milan vilabu vikubwa duniani,wandishi wanaandika sana tetesi kuzihusu hizo club lkn husikii maafisa wao wa habari kuwaattack waandishi kwa vitu personal,mwisho wa siku akitukanwa naye atadai "mnanionea sababu mimi mlemavu",unaanzisha ugomvi wa mawe wakati wewe mwenyewe unaishi nyumba ya vioo.

Atofautishe tu kati ya tofauti ya ushabiki na uweledi,kama nao wandishi wakireact kama afanyavyo yy,atakaye umia ni yeye.

Yeye mtu mgani kishagombana na Shaffih Dauda,Efm na leo hii Maulid wa Kitenge wa Wasafi kwa mambo ambayo haya make sense.Mbona akina Masao Bwire,Kifaru pamoja na kuongea kwao ila huwasikii kuwa attack waandishi kwa vitu personal.
umesahau na pia alishagombana na yule msemaji wa Azam
 
Mtu akirekebisha tayari amekua anamchukia? Sasa amchukie kwa kipi? Akikosoa tayari kashakua Yanga, angesifia usingeona huo u yanga unaosema
Hii Mikia hainaga akili kama tu taahira Manara

Mikia inafanana
 
Kuna Mtu Mmoja mpo nae sana huko Serikalini na katika ile Ofisi yako nyingine ya UNOKO UMBEA pale Oysterbay mkabala na St. Peter's Church aliwahi kuniambia kuwa una Dharau na Kujisikia sana nikamkatalia, ila kwa ulichofanya Leo nimemuamini kwa 100%.

Leo ukiwa Dodoma umefanya Press Conference yako ambapo umeongea Vitu vingi tu ila Mimi nitajikita katika Moja ambalo nina Interest nalo hasa nikiwa kama Mdau na Mdaawa vile vile wa Msemaji wa Taasisi ya Klabu yangu pendwa iliyoguswa japo ulijufanya Kufumba ila tusiokuwa na PhD kama yako lakini tumekuzidi Akili tukakugundua mapema mno.

Kauli yako ya kusema nainukuu.." Hawa Wasemaji wadogo wadogo wa hivi Vilabu ambao pia wako chini yangu Mimi wajirekebishe " ndiyo imenitoa Mafichoni All - Rounder ( Mzee wa Makavu Mubashara ) kuja Kukunyoosha kidogo kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa Wengine ili mbadilike.

Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) hiki Kiburi cha Kuwaita Wenzako ( hasa akina Manara, Bumbuli na Nugaz ) kuwa ni Wasemaji wadogo wadogo umekitoa wapi? Hivi Serikali unayoisemea ina Nguvu ya Kiushawishi kuliko hivi Vilabu viwili Vikongwe nchini vya Simba na Yanga? Umesahau kuwa wenye hivi Vilabu wakiamua Kushawishiana ili CCM yako yenye Serikali unayoisemea isishinde kwa Mashabiki wake Kutoipigia Kura inawezekana na ukaishia hata Kuikosa hiyo Kazi yenyewe?

Najua fika kuwa Wewe ni Mshabiki mkubwa wa Yanga SC pia ni Rafiki mkubwa tu wa Mtangazaji wa Wasafi FM Maulid Kitenge ambaye pia ni Yanga SC Mwenzako ila Unamchukia mno Msemaji wa Simba SC Haji Manara na kubwa zaidi ni kutokana na Fame yake ambayo inakufunika Wewe kwani Manara anaisemea Klabu Kubwa nchini ambayo pia ina Mafanikio ya Kimchezo kwa sasa Barani Afrika.

Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) nimeshangaa sana leo Kinafiki kabisa ( kwa Kujua kuna Mzozo mkubwa baina ya Rafiki yako Maulid Kitenge na Haji Manara ) ndiyo nawe ukajifanya Kukemea na Kuwafunda Maafisa Habari kwa kuwataka wafuate Maadili wakati Kimsingi hata Wewe Mwenyewe tu hayo Maadili huna. Na kuonyesha kuwa hukuwa Fair na Kufanya balance ya reference yako kwa Chuki zako Kwake Msemaji wa Simba SC Haji Manara ukaona utoe mfano mbaya wa Kumhusu Yeye ( hasa juu ya ile Kauli yake ya Kiutani ya kutowataka Mashabiki wa Yanga SC wasiingie Uwanjani dhidi ya Plateu FC ya Nigeria ) ila hukutoa Mifano mingine hasi inayowahusu Msemaji wa Yanga SC Hassan Bumbuli na Afisa Uhamasishaji wa Yanga SC Antonio Nugaz.

Labda leo nikusaidie tu Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) na sijui kwanini hili hukulijua ( hulijui ) pamoja na Kuringia hiyo Doctorate ( PhD ) yako ya SAUT Dar es Salaam Campus. Ni kwamba Simba na Yanga ni Watani wa Jadi hivyo Kutoleana maneno ya Shombo au Kucharurana Kwao ni Jambo la Kawaida mno na tena lina Afya ya Kiushindani Uwanjani na hata Chachu ya Kibiashara na Kuongeza Hamasa kwa Sisi Mashabiki wao. Hivyo basi kutaka Kuwafunga ' Spidi Gavana ' hawa Wasemaji wao ni kutaka Kudharaulika tu na Kujipotezea muda wako. Acha Kuwafananisha hawa Wasemaji wa hivi Vilabu vikubwa viwili na hao Wasemaji wako wa Taasisi za Kiserikali unaowaburuza utakavyo kila Uchao tu. Simba na Yanga ni zaidi ya Taasisi za Kiserikali na hata huyo aliyeko hapo Ikulu ( Boss wako ) sawa?

Halafu sijui ni kwanini Dkt. Abbas unakereka sana na Haji Manara hasa akiwa anajiita Kiutani tu Msemaji wa Taifa. Kwani akijiita Msemaji wa Taifa ndiyo ameshachukua Nafasi yako ya Msemaji wa Serikali? Acha Ushamba Wewe!!!! au hujui kuwa hata Kihistoria tu Jina la Utani la Simba SC ni Taifa Kubwa? Umeniangusha sana Mwanazuoni Wewe kwa hili ( japo najua Kichwani kwa IQ upo vizuri ukizingatia SAUT ulikopatia hiyo Doctorate yako huwa wanazalisha Geniuses tupu )

Nimeambiwa pia na Mmoja wa Wasaidizi wako kuwa unakereka sana pale ukisikia ama Haji Manara mwenyewe anajiita au Watangazaji wa Vipindi vya Michezo nchini Tanzania wakimuita ( wakimtambulisha ) kwa kusema ni Mkurugenzi wa Habari wa Simba SC. Hivi Logically tu Haji Manara akijiita hivyo kuna Kosa? Kwanini unakereka na kila Kitu tu Cha Kihabari na Kimawasiliano unataka Ukihodhi Wewe huku ukipenda Uogopeke na Watanzania? Hii Supremacy unayoitafuta ina faida gani na ipi Kwako? Badilika upesi tafadhali hujachelewa Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) sawa?

Mwisho namalizia kwa Kukuachia assignment ndogo tu. Tafadhali pitia Clips za aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC ( sasa DC Arumeru ) Jerry Muro halafu malizia na Clips za Msemaji wa sasa wa Yanga SC Bumbuli na Afisa Uhamasishaji wa Yanga SC Nugaz na ukimaliza nitaomba unipe Mrejesho wako ni nani hana Maadili hasa na pengine kwa uliyoyasikia alipaswa ama Kukemewa na hata Kuchukuliwa hatua za Kinidhamu ( Kisheria ) haraka. Je, Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) Kipindi kile aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC Mheshimiwa DC Jerry Muro alipokuwa akimdhalilisha Msemaji wa Simba SC Haji Manara kwa Ulemavu wake wa Ngozi na Kuwadhalilisha Viongozi wa Simba SC na wana Simba SC pia ulikuwa humsikii? Mbona hukuwahi Kujitokeza Kukemea na Kukazia katika Maadili kama unavyosisitiza leo? Acha Unafiki wako tafadhali na wala Unafiki haukupendezi kama Msemaji wa Serikali na Msomi ( Mwanazuoni ) ulivyo.
Mkuu, samahani, hivi yule GENTA ni ndugu yako? Mnafanana kweli UANDISHI!
 
Back
Top Bottom