Msemaji wa Serikali, Dkt. Abbas acha Dharau na Punguza Chuki zako kwa Msemaji wa Simba SC, Haji Manara

Tuwe tu wakweli Manara ni namba ingine kabisa na ana ushawishi yaani nyota yake inanga'aa sana kwenye usemaji. ..kwa propaganda kwakweli bado sijaona kama Manara,..... bado sana ...fame kazaliwa nayo na nyota yake inanga'aa siku hadi siku jua halizuiwi kwa ungo na Wamuache Manara msemaji wa taifa hata wakimpiga majungu ukwl tunaujua...Mimi Yanga lialia lkn kwenye ukwl usemwe tu.
 
Mtoa mada hata mimi nilishangaa sana anavyowaita wenzake wasemaji wadogo wakati yeye ikiwekwa top 5 ya wasemaji maarufu nchi hii bila kujali wanatokea taasisi gani, nadhani yeye anaweza kushika mkia au asiwemo.
Hicho ndicho kinachomkera!
 
Kuna Mtu Mmoja mpo nae sana huko Serikalini na katika ile Ofisi yako nyingine ya UNOKO UMBEA pale Oysterbay mkabala na St. Peter's Church aliwahi kuniambia kuwa una Dharau na Kujisikia sana nikamkatalia, ila kwa ulichofanya Leo nimemuamini kwa 100%.

Leo ukiwa Dodoma umefanya Press Conference yako ambapo umeongea Vitu vingi tu ila Mimi nitajikita katika Moja ambalo nina Interest nalo hasa nikiwa kama Mdau na Mdaawa vile vile wa Msemaji wa Taasisi ya Klabu yangu pendwa iliyoguswa japo ulijufanya Kufumba ila tusiokuwa na PhD kama yako lakini tumekuzidi Akili tukakugundua mapema mno.

Kauli yako ya kusema nainukuu.." Hawa Wasemaji wadogo wadogo wa hivi Vilabu ambao pia wako chini yangu Mimi wajirekebishe " ndiyo imenitoa Mafichoni All - Rounder ( Mzee wa Makavu Mubashara ) kuja Kukunyoosha kidogo kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa Wengine ili mbadilike.

Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) hiki Kiburi cha Kuwaita Wenzako ( hasa akina Manara, Bumbuli na Nugaz ) kuwa ni Wasemaji wadogo wadogo umekitoa wapi? Hivi Serikali unayoisemea ina Nguvu ya Kiushawishi kuliko hivi Vilabu viwili Vikongwe nchini vya Simba na Yanga? Umesahau kuwa wenye hivi Vilabu wakiamua Kushawishiana ili CCM yako yenye Serikali unayoisemea isishinde kwa Mashabiki wake Kutoipigia Kura inawezekana na ukaishia hata Kuikosa hiyo Kazi yenyewe?

Najua fika kuwa Wewe ni Mshabiki mkubwa wa Yanga SC pia ni Rafiki mkubwa tu wa Mtangazaji wa Wasafi FM Maulid Kitenge ambaye pia ni Yanga SC Mwenzako ila Unamchukia mno Msemaji wa Simba SC Haji Manara na kubwa zaidi ni kutokana na Fame yake ambayo inakufunika Wewe kwani Manara anaisemea Klabu Kubwa nchini ambayo pia ina Mafanikio ya Kimchezo kwa sasa Barani Afrika.

Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) nimeshangaa sana leo Kinafiki kabisa ( kwa Kujua kuna Mzozo mkubwa baina ya Rafiki yako Maulid Kitenge na Haji Manara ) ndiyo nawe ukajifanya Kukemea na Kuwafunda Maafisa Habari kwa kuwataka wafuate Maadili wakati Kimsingi hata Wewe Mwenyewe tu hayo Maadili huna. Na kuonyesha kuwa hukuwa Fair na Kufanya balance ya reference yako kwa Chuki zako Kwake Msemaji wa Simba SC Haji Manara ukaona utoe mfano mbaya wa Kumhusu Yeye ( hasa juu ya ile Kauli yake ya Kiutani ya kutowataka Mashabiki wa Yanga SC wasiingie Uwanjani dhidi ya Plateu FC ya Nigeria ) ila hukutoa Mifano mingine hasi inayowahusu Msemaji wa Yanga SC Hassan Bumbuli na Afisa Uhamasishaji wa Yanga SC Antonio Nugaz.

Labda leo nikusaidie tu Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) na sijui kwanini hili hukulijua ( hulijui ) pamoja na Kuringia hiyo Doctorate ( PhD ) yako ya SAUT Dar es Salaam Campus. Ni kwamba Simba na Yanga ni Watani wa Jadi hivyo Kutoleana maneno ya Shombo au Kucharurana Kwao ni Jambo la Kawaida mno na tena lina Afya ya Kiushindani Uwanjani na hata Chachu ya Kibiashara na Kuongeza Hamasa kwa Sisi Mashabiki wao. Hivyo basi kutaka Kuwafunga ' Spidi Gavana ' hawa Wasemaji wao ni kutaka Kudharaulika tu na Kujipotezea muda wako. Acha Kuwafananisha hawa Wasemaji wa hivi Vilabu vikubwa viwili na hao Wasemaji wako wa Taasisi za Kiserikali unaowaburuza utakavyo kila Uchao tu. Simba na Yanga ni zaidi ya Taasisi za Kiserikali na hata huyo aliyeko hapo Ikulu ( Boss wako ) sawa?

Halafu sijui ni kwanini Dkt. Abbas unakereka sana na Haji Manara hasa akiwa anajiita Kiutani tu Msemaji wa Taifa. Kwani akijiita Msemaji wa Taifa ndiyo ameshachukua Nafasi yako ya Msemaji wa Serikali? Acha Ushamba Wewe!!!! au hujui kuwa hata Kihistoria tu Jina la Utani la Simba SC ni Taifa Kubwa? Umeniangusha sana Mwanazuoni Wewe kwa hili ( japo najua Kichwani kwa IQ upo vizuri ukizingatia SAUT ulikopatia hiyo Doctorate yako huwa wanazalisha Geniuses tupu )

Nimeambiwa pia na Mmoja wa Wasaidizi wako kuwa unakereka sana pale ukisikia ama Haji Manara mwenyewe anajiita au Watangazaji wa Vipindi vya Michezo nchini Tanzania wakimuita ( wakimtambulisha ) kwa kusema ni Mkurugenzi wa Habari wa Simba SC. Hivi Logically tu Haji Manara akijiita hivyo kuna Kosa? Kwanini unakereka na kila Kitu tu Cha Kihabari na Kimawasiliano unataka Ukihodhi Wewe huku ukipenda Uogopeke na Watanzania? Hii Supremacy unayoitafuta ina faida gani na ipi Kwako? Badilika upesi tafadhali hujachelewa Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) sawa?

Mwisho namalizia kwa Kukuachia assignment ndogo tu. Tafadhali pitia Clips za aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC ( sasa DC Arumeru ) Jerry Muro halafu malizia na Clips za Msemaji wa sasa wa Yanga SC Bumbuli na Afisa Uhamasishaji wa Yanga SC Nugaz na ukimaliza nitaomba unipe Mrejesho wako ni nani hana Maadili hasa na pengine kwa uliyoyasikia alipaswa ama Kukemewa na hata Kuchukuliwa hatua za Kinidhamu ( Kisheria ) haraka. Je, Dkt. Abbas ( Msemaji wa Serikali ) Kipindi kile aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC Mheshimiwa DC Jerry Muro alipokuwa akimdhalilisha Msemaji wa Simba SC Haji Manara kwa Ulemavu wake wa Ngozi na Kuwadhalilisha Viongozi wa Simba SC na wana Simba SC pia ulikuwa humsikii? Mbona hukuwahi Kujitokeza Kukemea na Kukazia katika Maadili kama unavyosisitiza leo? Acha Unafiki wako tafadhali na wala Unafiki haukupendezi kama Msemaji wa Serikali na Msomi ( Mwanazuoni ) ulivyo.
Tumekusikia Haji Sunday Manara
 
Tuwe tu wakweli Manara ni namba ingine kabisa na ana ushawishi yaani nyota yake inanga'aa sana kwenye usemaji. ..kwa propaganda kwakweli bado sijaona kama Manara,..... bado sana ...fame kazaliwa nayo na nyota yake inanga'aa siku hadi siku jua halizuiwi kwa ungo na Wamuache Manara msemaji wa taifa hata wakimpiga majungu ukwl tunaujua...Mimi Yanga lialia lkn kwenye ukwl usemwe tu.
manara sio msemaji wa taifa, Tanzania tuna cheo kimoja tu cha MSEMAJI MKUU WA SERIKALI.
 
Back
Top Bottom