ni kwa sababu inaelekea bado huoni tofauti ya chama na serikali. Chan's kinajiendesha kwa matamko ya vikao na ya viongozi wao. Serikali inaendeshwa kwa Sheria na maamuzi bunge. Ni kinyume cha Sherpa kwa mtumishi wa serikali kuchanganya matamkoyakisiasa kwenye utendaji wake. Lazima Ccm wabadilishe ilani yao iwe sheria ya bunge ndipo itambuliwe kisheriaMkuu naona hujui unazungumza nini? Hivi kwenye sheria iliyounda shirika la nyumba inazungumzia kuwa kwamba watapitia upya utaratibu wa kupangisha? Ilani ya Chama kwa wakati husika ndio inayoweza kusema nini kifanyike kwenye sekta husika na nini kisifanyike. Unataka kusema Ununuzi wa Meli mpya ziwa Victoria upo kwenye sheria iliyounda mamlaka ya bandari? UUzaji wa nyumba za serikali umo kwenye seria iliyoanzisha NHC au ilikuwa ilani ya Chama? Ubinafsishaji, ujenzi washule za kata, ujenzi wa barabara n.k ni vitu gani kama sio ilani? Kinachofanyika Bunge linapitisha tu bajeti ambayo inatekelezwa na watumishi wa serikali.
Kuhusu kupandisha bei,sidhani hilo suala ni la kisiasa(it might be), inawezekana wamefanya cost analysis au wamejiamulia tu.Nakubaliana nawewe kwamba something definetely need to be changed.
Lakini kwa kuprofile race does it mean NHC wanataka kuintroduce quota system hata kwenye upangishaji wa nyumba zao?
au labda what is the significance of such an exercise?
Sijui umetafakari the wider implication ya kila landlord akiamua kuprofile wapangaji wake kwa kutumia race, kabila, dini mwisho
wake utakuwaje?
Halafu sijaelewa kwa kupandisha bei ya pango by over 300% kunawezaje kuchukuliwa kama ni affirmative action, maana kwa
ninavyoelewa affirmative action inatumika kuwanyanyua(kuwabeba) wale waliokua disadvantaged historically.
Nitashkuru ukiweza kufafanua zaidi.
Si kweli.Hapa nchini kuna tatizo la watu kushindwa kujua wanawajibika kwa nani katika sekta za umma hasa kutokana na utamaduni mbaya na wa hatari wa kuchanganya serikali na CCM.
Hii ndiyo maana utakuta waziri anawaambia watu kuwa kujenga barabara, mashule, huduma za afya, makazi, nk ni utekelezaji wa ilani ya CCM. Hii si kweli kwa sababu hizi ni huduma za lazima na ni haki ya binadamu yeyote kuwa nazo hivyo huwezi ukasema ni sehemu ya ilani ya chama chochote. Ilani katika mambo haya zinatofautiana katika kuyatimiza au mbinu za kuyaboresha.
Hii yote ni michezo ya cheap politics ambazo wanajua kuwa wengi hawana uwezo wa kuzichambua.
Wandugu nimeona news muda huu na nimemsikia Msechu anasema kwa kusisitiza anasema ayafanyao yeye huko NHC anatekeleza ilani ya CCM.
Kindly guys help me to understand, hii imekaaje?
Hekima na busara nyingine watu sijui wanazitoa wapi, eti anatekeleza ilani ya chama cha serikali inayotawala kwa kuivua nguo serikali tawala hadharani. Busara yangu inanituma ni mshauri huyu bwana Nehimia anze kutafuta kazi sehemu nyingine, maana hapo NHC kwa wenye akili ndio kibarua kimeshaisha hivyo, hayo mengine ni suala la muda tu.
Kipengele ilikua muhimu kukitaja ili tujue kama kweli tafsiri ya hicho kipengele inaendana na mambo yanayofanywa na NHC.
Mfano, kutengeza forms za kutaka kujua rangi ya ngozi ya wapangaji(racial profiling) imeandiakwa kwenye hiyo ilani? Huku tukijua
jinsi waasisi wa taifa letu walipingana na ukaburu kwa kila hali?
Na je serikali ya CCM inayosema haiwezi kupandisha kima cha chini cha mshahara kufikia laki tatu na nusu mpaka kurisk migomo
inapata wapi ujasiri wa kubariki viwango vipya vya kodi anavyopendekeza bwana Mchechu vya laki 5 kwa mwezi? Je sababu kuu
ya uanzishwaji wa NHC inazingatiwaje hapa ya kuwapatia affordable housing wananchi.
Isije kuwa "Natekeleza Ilani ya CCM" ikawa ni tired slogan isiyokuwa na mashiko yeyote.
Hapo mkuu umenena. Ukiangalia shutuma za Azim Dewji juu ya NHC kwenye Mwananchi ya tarehe 10 Oktoba 2011 ukurasa wa 13 unajuwa kabisa huyu Bwana siku zake si nyingi pale NHC. Arudi kwenye banking industry atafanya vizuri zaidi.
hapa a town ukimuita mtu msechu lazima mzichape
dr,My friend Nehemiah, Just do the right thing as you have been doing so far. I know you know this, that your operations are, or at least they should be, guided by your Board and the appropriate relevant statuses. We also know that you are currently serving under the current government, but your service is definitely larger that the government. Did you really have to justify your actions by making reference to CCM Manifesto? What you did yesterday is exactly what other CEOs for public corporations have been doing in this country and they failed miserably because, instead of doing the right thing, they're busy doing what was politically correct! We thought and you made us believe that you're different, or are you not??!!