Msanii wa Nigeria, Kizz Daniel akamatwa na Polisi Jijini Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,848
12,080
Baada ya kushindwa kutoa burudani usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Next Door Arena msanii huyo kutoka Nigeria amekamatwa na Polisi.

=========

Baada ya kushindwa kutoa burudani usiku wa kuamkia leo Agosti 8, 2022 katika Ukumbi wa Next Door Arena, msanii Kizz Daniel kutoka Nigeria amekamatwa na Polisi.

Chanzo kutoka kwa waratibu wa shoo hiyo kimeeleza kuwa msanii huyo alichelewa ndege kutoka Nigeria na kuwasili Dar es Salaam usiku mwingi muda mfupi kabla ya shoo kuanza.

Mara baada ya kuwasilia Dar ikagundulika kuwa begi lake la nguo halionekani.

Usiku huohuo simu zikaanza kupiga sehemu tofauti ili msanii huyo apate nguo, baadaye zikapatikana baadhi ya nguo lakini alizikataa zote, hadi inafika saa tisa usiku hakukuwa na mwelekeo na mwisho hakutokea kwenye shoo.



 
Huwa nawashangA watu
Yaani wewe ndy utoe hela sjui
Ukamuona msanii alafu hyo msani
Anakuletea miyeyusho dharau,wakat hela yako hiyo hiyo ndy inamfanya msanii hyo kuishi na kuwa tajir
Acha hela zetu tuzidi kumwagia mioyo
Yetu tu

Ova
 
Kawaletea ubuga wabongo 😁😁😀 tatizo wabongo shobo hawatamshambulia huko mitandaoni ila wangekua n wakenya asingeleta hii dharau
 
Back
Top Bottom