Msanii wa Muziki wa Dansi nchini "Amigolas" Amefariki Dunia

Msanii wa Muziki wa Dansi nchini "Amigolas" Amefariki Dunia

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
76,827
Reaction score
110,077
amigo.jpg


Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa.

Amigolas alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote kufanyika.

Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Amigolas alikuwa mmoja wa wanamuziki waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa uaminifu mkubwa kwa miaka mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na wenzake kadhaa kuanzisha Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na JKT na kuwa Ruvu Stars Band.


Chanzo: irenemwamfupejamii
 
Rip Amigolas 'baba na Sophy'.(nasikiaga wanamuimba hivyo sijui nimepatia).
 
RIP Amigolas ulikuwa mwimbaji mzuri sana. Nakumbuka ulifanya vizuri sana ulipokuwa twanga pepeta ukishirikiana kuimba na Ally Choki.
 
Namkumbuka sana kipindi kile na kina Ali choki na Jesca charles wamening'iniza c25 viunoni.
 
Daah kama siamini vile wakuu! Huku Rwanda habari hiyo ndiyo tunaipata kupitia JF
 
twanga.JPG

Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta,pichani kulia enzi za uhai wake akiwa kazini,ajulikanae kwa jina la Amigolas amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo,katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.

Taarifa za awali ambazo chumba cha habari cha Globu ya Jamii imezipata kutoka kwa vyanzo vya kuaminika,zinaeleza kuwa Marehemu Amigolas alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo mpaka kufariki kwake.

Tutaendelea kupeana taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin

Chanzo:Michuzi
 

Attachments

  • 1415514447196.jpg
    1415514447196.jpg
    12.2 KB · Views: 702
Amigolas ni mmoja wa wanamuziki wenye respect sana nchi hii na wasio na makuu. Katumikia kwa heshima kubwa sana twanga pepeta. Mungu msamehe makosa yake, Aaaamin.
 
Daah kama siamini vile wakuu! Huku Rwanda habari hiyo ndiyo tunaipata kupitia JF

JF ndo kila kitu siku hizi. Ukitaka kuamini, wasikilize radio one eti wanajifanyaga Breaking News kwamba haijatangazwa popote, wakati wanaitangaza wewe fungua JF muda huohuo utaikuta. Mimi nimeshahakiki hilo kama mara mbili hivi. JF ipo juu
 
RIP Amigolous, nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 90 wakati ndo Twanga iko moto na akina Alli Choki, Jesca Charles, Masanja, Katapila, Lwiza Mbutu na yule bwana mpiga gitaa aliyekuwa na sharubu jina limenitoka. Ilikuwa ni baraa kwelikweli pale Mango garden na wakati mwingine pale Leaders club. Ilikuwa wanapo_perform imifika saa sita usiku inapopigwa kidali po mango garden mpaka watu huku kwenye mataa ya Mwananyamala wanapigana kidali poo. Nakukumbuka Amigolous wakati huo mnacheza na ungo mikononi, ulikuwa unatisha kwelikweli. Kalale mahali pema Mr Amigolous.
 
Back
Top Bottom