Msanii wa Muziki wa Dansi nchini "Amigolas" Amefariki Dunia

Msanii wa Muziki wa Dansi nchini "Amigolas" Amefariki Dunia

RIP Amigolas. Tutakumbuka sana, wimbo wa Aminata uliotunga ukiwa Twanga Pepeta utanifanya nikumbuke daima.
 
Namkumbuka sana kipindi kile na kina Ali choki na Jesca charles wamening'iniza c25 viunoni.

daah,,,,kiongozi umenikumbusha mbali asee,,nahii ndio sababu ya zile CM kuitwa TWANGA PEPETA naikawa km fashen flan kwenye Maonyesho yao mashabiki utakuta meza nyingi zimewekwa hizo c25 nacjui km itakuja utokea Bendi ya wazawa kufanya kazi nzuri naika kubalika km TWANGA ya wakati ule ,,! R.I.P AMIGOLAS
 
RIP Amigolous, nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 90 wakati ndo Twanga iko moto na akina Alli Choki, Jesca Charles, Masanja, Katapila, Lwiza Mbutu na yule bwana mpiga gitaa aliyekuwa na sharubu jina limenitoka. Ilikuwa ni baraa kwelikweli pale Mango garden na wakati mwingine pale Leaders club. Ilikuwa wanapo_perform imifika saa sita usiku inapopigwa kidali po mango garden mpaka watu huku kwenye mataa ya Mwananyamala wanapigana kidali poo. Nakukumbuka Amigolous wakati huo mnacheza na ungo mikononi, ulikuwa unatisha kwelikweli. Kalale mahali pema Mr Amigolous.

anaitwa Adolph Mbinga "mtuhumiwa namba moja" ni moja kati ya wapiga gita bora wa kizazi cha kati
 
RIP Amigolous, nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 90 wakati ndo Twanga iko moto na akina Alli Choki, Jesca Charles, Masanja, Katapila, Lwiza Mbutu na yule bwana mpiga gitaa aliyekuwa na sharubu jina limenitoka. Ilikuwa ni baraa kwelikweli pale Mango garden na wakati mwingine pale Leaders club. Ilikuwa wanapo_perform imifika saa sita usiku inapopigwa kidali po mango garden mpaka watu huku kwenye mataa ya Mwananyamala wanapigana kidali poo. Nakukumbuka Amigolous wakati huo mnacheza na ungo mikononi, ulikuwa unatisha kwelikweli. Kalale mahali pema Mr Amigolous.

Yaaah,,,, hicho kilikuwa ni kikosi cha kz ya Burdani huyo jamaa mwenye Masharubu ni ADOLPH MBINGA kulikuwa na Jamaa mmoja nae akiitwa JOSEPH WATUGURU huyu alikuwa mtaalam wa kutwanga BAS GUITER,,,,daah,,,,R.I.P AMIGOLAS
 
Pole mkuu.
Naamini ulifahamu kuhusu kuugua kwake na ulipata nafasi ya kufanya chochote kusaidia matibabu yake.

Amigo alianza kuwa na matatizo ya moyo muda mrefu sana pengine ni mwaka wa tano sasa...

Hivyo huyo bwana kama ni nduguye bila shaka atakuwa anafahamu...
 
Pumzika kwa amani Amigolasi muzee ya mustachi wa amigo!
 
Back
Top Bottom