Msanii wa JF tunahitaji maelezo ya kina hapa

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Hongeraa.
Hapo kwenye bold naomba nikusahihishe kwamba mnatoa elfu 53 cash na siyo laki moja. kama umepewa na receipt basi ada itakuwa imepanda.
sisi wa mwanzo tulilipa alfu 35, waliokuja awamu ya pili wanalipa hizo alfu 53.
Kama kuna msanii, mwanamichezo na Mwanahabari achangamkie hiyo ishu maana kuna wajanja wameshakula sana vichwa kwa kuwalipisha malaki kibao ilihali bei ni chee. Ukilipa zaidi ya elfu 53 nitumie PM nitakuelekeza cha kufanya ili urudishiwe chenji yako.

Viwanja hivi ni juhudi za viongozi wa SHIWATA na siyo maono ya serikali, tuliifuata serikali baada ya kuanza kutekeleza habari hii. Ingawa baadhi ya viongozi serikalini wanaipiga vita hii programu lakini tunajitahidi kukubalika na kufuata taratibu muktadha ili kupata viwanja zaidi.
(nadeclare interest------ mimi nimo ktk mradi huu)

Hii ishu ya viwanja haiusiani na kampeni za Kikwete.
Nenda pale SHIWATA ukasome katiba na malengo ya shirikisho ndipo utafunguka kwamba hakuna smaslahi ya kisiasa kwenye mradi wa viwanja.

Mzee umeanza wazimu wa kukurupukia hoja.
umebalansi story?
nimewapigia viongozi wa SHIWATA wamefafanua na hata kwenye clouds (walioshikia debe negatively) wameelewa na kusuport hatua zilizochukuliwa.

Mimi ni sehemu ya uongozi wa sanaa, huwa nafguatilia kwa karibu sana ishu zote za sanaa zipitazo mbele yangu.

Wasanii hawajatapeliwa pesa zao.

Msanii heshima mbele nakuomba kwa heshima na taathima ufafanue kwa vipi hatujatapeliwa na ilihali umemsikia hata mkuu wa wila ya mkuranga na wenyeviti wa mtaa wakikanusha maeneo ya wazi eneo la mkuranga? wanadai yaliyoko yamejaa na sisi hela zetu tayari mmekula?
 
Risiti zinaonyesha tsh 4000/= gharama za usafiri hadi mkuranga, tsh 4000/= gharama za kupima kiwanja na tsh 45,000/= ada ya uanachama kwa miaka mitatu.sasa wasanii wanadai nini, labda hio tsh 4000/= ya kupima viwanja ambavyo ni hewa.bongo dar ya dude hii, hata dude mwenyewe kaliwa.big up mwenyekiti wa wasanii.
 
Kweli wewe Tonge tena lisilo na mchuzi huwezi kujibu ka chizi
 
Msanii aliwapiga usanii! Hawezi kuja hapa mzee anatumbua pesa za wasanii kisanii!
 
Ha ha ha yamewakuta ya DECI?

Kweli mkuu inatuuma sana wengine wetu ni wanafunzi bagamoyo chuo cha sanaa wametumia ka pocket money kununua viwanja kumbe fake na kuna huyo member hapo juu kumbe anahusika inatuuma sana mkuu ila tufanyeje? wametupa hadi vedocument fake . Hata Ephraim Kibonde wa clouds fm yamemkuta sema anaogopa kusema.
 
Msanii aliwapiga usanii! Hawezi kuja hapa mzee anatumbua pesa za wasanii kisanii!

Tena alisema tu MP tukikwama kumbe tuna PM account zetu. ila kuna watu wana dhambi hata sisi jamani wanatuibia kazi zetu wanaiba inauma sana
 
Mtu anaitwa msanii wewe unacheza naye dili....lazima msanii akupige usanii kama msanii kisanii
 
Jina tu linaonyesha yeye ni msanii shauri yenu.
Bora mnegejenga heshima Bar tu.
 
Hii sio hoja ya kuchukua airtime kwenye radio.

Mmetapaliwa kalaki tu mnapiga mayowe. Sisi tuliotapeliwa mamilioni kwenye NICOL mbona hatupigi kelele, mnakutaka kukasulubisha kasangara ka Mkuranga kwasababu sio kaselebriti.

Mbona masangara ya NICOL hamuyaongelei?

Ivi hao wasanii wangekua wa sumbawanga kungekua thread zaidi ya tatu humu?
Hao vuvuzela wa clouds wangesikia waliotapeliwa ni wanakijiji wa tandahimba, wangetumia zaidi ya 45min free airtime kuzungumzia hiyo ishu kama walivyofanya.
Msiwe na double std. Tanzania si Dar pekee.
 
Kweli mkuu inatuuma sana wengine wetu ni wanafunzi bagamoyo chuo cha sanaa wametumia ka pocket money kununua viwanja kumbe fake na kuna huyo member hapo juu kumbe anahusika inatuuma sana mkuu ila tufanyeje? wametupa hadi vedocument fake . Hata Ephraim Kibonde wa clouds fm yamemkuta sema anaogopa kusema.

poleni, kweli mmeingizwa mkenge...
 
Nimesikia watu wakijadili hili sakata lakini kimzaha zaidi ati " walitaka kuanzisha kijiji cha wasanii cha nini wakati tuna nchi nzima ya wasanii, na kila mtu ni msanii?" Nilicheka siyo kwa kufurahi bali kwa kushangaa namna tunavyochukulia kila kitu kimzahamzaha.
Inasikitisha kweli kuona utapeli ukizagaa kila kona.Inatuonyesha kuwa utawala wa sheria bado ni ndoto.
 
Back
Top Bottom