Kwa sasa makazi yameshagawiwa kwa wasanii huko mkuranga.
Kule kisarawe taratibu zote zilifuatwa, ila mwishoni mkuu wa wilaya akageuka na kudai wasanii ni matapeli. ila ukweli ni kwamba kuna ardhi kubwa ya kijiji imeuzwa kinyemela kwa mwekezaji, hivyo ujio wa wasanii na wanahabari huko ikawa ni tishio kwa uongozi wa wilaya. hivyo juhudi zimefanyika kubatilisha uhalali wa wasanii kujiunga na kijiji cha visegese. Kuna wananchi walijitolea sehemu zao wanazomiliki kwa wasanii lakini mkuu wa wilaya amesema kwamba hawana haki ya kuja visegese. na kibaya zaidi hataki hata kuonana na viongozi wa wasanii kwani hata walipomtembelea ofisini aliwatolea lugha chafu na kuwatimua.
Kuna mavundo mengi sana nchi hii ila sisi tunayaona ya mijini na ofisi kubwa kubwa tu. huko chini ni jehanamu tupu