Msamaha na Kisasi

Msamaha na Kisasi

Nyoka akikugonga kisigino na kukuachia sumu ukajitibu ukapona inabidi akija tena umpe kisigino agonge mara ya pili kwa sababu shambulio la kwanza halikufanikiwa

Come on bro 🤦
Mkuu umenichekesha kweli,dah! Pointing hii inalenga kuhalalisha kisasi
 
Hapa tunaamua kuyapokea maumivu tunaugulia weee halafu tunayaacha yapite.Tunaanza kujifariji,kama ulinidhulumu nitajisemea mbona hiki kinatafutwa TU,au hakuna atayezikwa na Mali nk.
Tukifanya hivi maumivu yanaisha ila kumbukumbu itabakia
Mbona haya ni mateso sasa dah
 
Kuna msemo unasema, hakikisha unachagua upande

Usiwe vuguvugu
Kama ni moto, kuwa moto
Kama ni baridi, kuwa baridi

Japo watu wengi husema usijulikane kirahisi, ila tambua kuna hasara ya kutokujulikana

So unapokosewa, unapoudhiwa au kuumizwa, hakikisha unajulikana umesimama upande gani

Hii tabia ya kujifanya neutral kila wakati kuna muda sio nzuri

Jifunze kujua ni wapi uwe baridi, ni wapi uwe moto, na mara chache sana ujue ni wapi uwe vuguvugu

Kama mada inavyosema...

Msamaha au Kisasi?

Kama umekosewa na umeumizwa, halafu una uwezo wa kusamehe, samehe

Lakini samehe kwa dhati kabisa, kutoka ndani ya moyo

Kwa sababu ukisamehe, amani ya kwanza ataipata wewe kabla hata hajanufaika huyo uliyemsamehe

Sio unasema umesamehe halafu kila siku unanung'unika, unalalama na kurudia lile tukio

Hapo hujasamehe
Unajidanganya mwenyewe
Na huo unafiki wa kuonekana umesamehe wakati bado umebeba mzigo ndani, unaweza kukugharimu kihisia na hata kuharibu mambo mengine kwenye maisha yako

So kama umeamua kusamehe, samehe kweli
Usiwe vuguvugu

Lakini kama umechagua kisasi, ina maana kwako msamaha hauna tija, haukupi amani na unaamini kulipa kisasi ndio haki

Kuna dini inasema kisasi ni haki ya aliyekosewa

Kuna dini nyingine inasema samehe saba mara sabini

Yule aliyechagua kisasi amechagua kuamini kisasi ni haki yake

Na ukweli ni kwamba ana hoja, kwa sababu ni yeye pekee anayejua ameumizwa kwa kiwango gani

Lakini swali linabaki...

Baada ya kulipa hicho kisasi, una uhakika utapata amani, au ndio utaanza kuishi na majuto?

Mfano ukaona adhabu anayostahili aliyekukosea ni kumuua

Je, baada ya hapo utajisikia vizuri, au ndio utaanza kuishi na trauma ya kumwaga damu?

Unaweza ukaamini una haki ya kulipa kisasi

Lakini hakikisha kisasi chako hakiondoki na furaha yako hakichukui amani yako, wala hakiharibu destiny yako

Swali la mjadalašŸ‘‡

Wewe unaamini katika msamaha au kisasi?

Kwa nini umechagua upande huo?

Au wewe ni vuguvugu?

Na kama ni vuguvugu, unaelewa gharama za kutokuwa na msimamo?

ShesRise_1 🤚
My friends, ladies and gentlemen,
ni muhimu sana kusamehe na kusahau, kwasababu mbingu si hasira wataingia watakatifu tu.

Maisha hayana extra time,
chagua upande sasa, ili hatimae uwe na uhuru kamili, ujasiri usiotikisika na uwe na uhakika wa kusimamia unachokiamini kibinafsi na mbele ya jamii. Kua neutral ni unafiki na ubinafsi wa kindezi mno.

ondoka kwenye Giza na sheria kali za agano la kale, na uingie kwenye Nuru katika agano jipya lenye sheria zilizohuishwa. Kung'ang'ana na habari ya visasi dhidi ya ubaya uliotendewa kabla, ni kujitafutia maradhi ya kimwili na kiroho, lakini pia ni maandalizi ya kujiangamiza kwa makusudi kijami, kisiasa na kiuchumi.

ni muhimu sana kuchukuliana kibinadamu na kusonga mbele bila manung'uniko na itapendeza zaidi šŸ’
 
Utusamehe... Makosa yetu... Kama nasi tuwasamehevyo walio... Tukosea.......
Amina........
Ambao hawatoi msamaha hawaendi.... Mbinguni
 
Msamaha.... Ila hua sisahau nikimsamehe mtu.... Sijui ni mimi tuĀ” ila hata huyo niliemsamehe tunacheka vizuri tuĀ”
Achana na neno kusahau ambalo haiwezekani
Je unapokua unacheka
Hua na moyo mweupe au unafiki?
 
Daima mimi ni ntu wa kisasa. Ntu akinfanyia ubaya nami humlipa kwa ubaya na kuuzidisha kidogo.

Ukiwa ntu wa wa kumsamehe sana watu wanakuona kama mataqo yao.
 
My friends, ladies and gentlemen,
ni muhimu sana kusamehe na kusahau, kwasababu mbingu si hasira wataingia watakatifu tu.
Kusamehe tunasemehe ila kusahau ni uongo ubongo kazi yake ni kuhifadhi kumbukumbu ziwe nzuri au mbaya

Ili uamini hili
unaweza kuona tukio fulani
Ubongo ukakukumbusha kua hii sio mara ya kwanza kuona

na hapo wewe kama wewe ulikua umesahau ila Ubongo unakukumbusha baada ya kuona mfanano wa tukio
so kusahau sio rahisi na sidhani kama inawezekana
Maisha hayana extra time,
chagua upande sasa, ili hatimae uwe na uhuru kamili, ujasiri usiotikisika na uwe na uhakika wa kusimamia unachokiamini kibinafsi na mbele ya jamii. Kua neutral ni unafiki na ubinafsi wa kindezi mno.
Eeh chagua upande ishii
ondoka kwenye Giza na sheria kali za agano la kale, na uingie kwenye Nuru katika agano jipya lenye sheria zilizohuishwa. Kung'ang'ana na habari ya visasi dhidi ya ubaya uliotendewa kabla, ni kujitafutia maradhi ya kimwili na kiroho, lakini pia ni maandalizi ya kujiangamiza kwa makusudi kijami, kisiasa na kiuchumi.

ni muhimu sana kuchukuliana kibinadamu na kusonga mbele bila manung'uniko na itapendeza zaidi šŸ’
Hapa umejuja kama shemasi šŸ’
 
Kusamehe ni jambo moja kusahau ni jambo lingine...

Naweza kusamehe ila kusahau hapana..
Wala sio tatizo lako nadhani kila mtu yupo hivi
Samehe kwa dhati usibebe kinyongo
Ila kusema usahau labda kicwa uki format
 
Kisasi ni haqq ila fikiria Je? baada kulipa kisasi nitapata nafuu na hasira zangu.kushuka..?au ndo nitazidisha matatizo.? je.? hayo matatizo yanaepukika..?

NITACHANGIA VZR.:
 
Back
Top Bottom