Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 41
- 57
NSSF imetangaza msamaha kwa waajiri wenye malimbikizo ya michango na tozo kwa kuzingatia masharti yafuatayo;
- Waajiri watakaolipa malimbikizo yote ya michango ya wanachama (principal amounts) kabla au ifikapo 31 Agosti 2026, na kuendelea kulipa michango kwa wakati mpaka ifikapo 31 Desemba, 2026, watasamehewa tozo (overdue penalties) wanazodaiwa kwa asilimia 100.
- Waajiri watakaolipa malimbikizo yote ya michango ya wanachama (principal amounts) kabla au ifikapo 31 Oktoba 2026, na kuendelea kulipa michango kwa wakati mpaka ifikapo 31 Desemba, 2026, watasamehewa tozo (overdue penalties) wanazodaiwa kwa asilimia 75.
- Waajiri watakaolipa malimbikizo yote ya michango ya wanachama (principal amounts) kabla au ifikapo 31 Desemba 2026, watasamehewa tozo (overdue penalties) wanazodaiwa kwa asilimia 50.
- Waajiri wote ambao hawana malimbikizo ya michango ya wanachama (principal amounts) wanayodaiwa mpaka kufikia 31 Mei, 2026 na kuendelea kulipa michango kwa wakati mpaka ifikapo 31 Desemba, 2026, watasamehewa tozo (overdue penalties) wanazodaiwa kwa asilimia 100.
Kipindi kinachohusika na msamaha huu kwa waajiri kulipa madeni yote wanayodaiwa katika makundi manne kama ilivyoelekezwa, kitadumu kuanzia tarehe 1 Juni 2026 mpaka 31 Desemba 2026.