ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 16,861
- 39,923
- Thread starter
- #121
Ahaa basi tumuachie MunguKisasi ni juu ya Mungu.
Ahaa basi tumuachie MunguKisasi ni juu ya Mungu.
Unajiona una deserve kuitwa babu🤣Babu.
Mada nzuri sana ila yataka watu wenye kuwa wavumilivu katika kusoma muda mrefu(Maneno/mchango mrefu). Kwa mfano mtu amekuibia ndizi yako moja shambani. Kiuhalisia huyo ukimkamata anastahili na ni haki yake aadhibiwe.Kuna msemo unasema, hakikisha unachagua upande
Usiwe vuguvugu
Kama ni moto, kuwa moto
Kama ni baridi, kuwa baridi
Japo watu wengi husema usijulikane kirahisi, ila tambua kuna hasara ya kutokujulikana
So unapokosewa, unapoudhiwa au kuumizwa, hakikisha unajulikana umesimama upande gani
Hii tabia ya kujifanya neutral kila wakati kuna muda sio nzuri
Jifunze kujua ni wapi uwe baridi, ni wapi uwe moto, na mara chache sana ujue ni wapi uwe vuguvugu
Kama mada inavyosema...
Msamaha au Kisasi?
Kama umekosewa na umeumizwa, halafu una uwezo wa kusamehe, samehe
Lakini samehe kwa dhati kabisa, kutoka ndani ya moyo
Kwa sababu ukisamehe, amani ya kwanza ataipata wewe kabla hata hajanufaika huyo uliyemsamehe
Sio unasema umesamehe halafu kila siku unanung'unika, unalalama na kurudia lile tukio
Hapo hujasamehe
Unajidanganya mwenyewe
Na huo unafiki wa kuonekana umesamehe wakati bado umebeba mzigo ndani, unaweza kukugharimu kihisia na hata kuharibu mambo mengine kwenye maisha yako
So kama umeamua kusamehe, samehe kweli
Usiwe vuguvugu
Lakini kama umechagua kisasi, ina maana kwako msamaha hauna tija, haukupi amani na unaamini kulipa kisasi ndio haki
Kuna dini inasema kisasi ni haki ya aliyekosewa
Kuna dini nyingine inasema samehe saba mara sabini
Yule aliyechagua kisasi amechagua kuamini kisasi ni haki yake
Na ukweli ni kwamba ana hoja, kwa sababu ni yeye pekee anayejua ameumizwa kwa kiwango gani
Lakini swali linabaki...
Baada ya kulipa hicho kisasi, una uhakika utapata amani, au ndio utaanza kuishi na majuto?
Mfano ukaona adhabu anayostahili aliyekukosea ni kumuua
Je, baada ya hapo utajisikia vizuri, au ndio utaanza kuishi na trauma ya kumwaga damu?
Unaweza ukaamini una haki ya kulipa kisasi
Lakini hakikisha kisasi chako hakiondoki na furaha yako hakichukui amani yako, wala hakiharibu destiny yako
Swali la mjadala👇
Wewe unaamini katika msamaha au kisasi?
Kwa nini umechagua upande huo?
Au wewe ni vuguvugu?
Na kama ni vuguvugu, unaelewa gharama za kutokuwa na msimamo?
ShesRise_1 🤚
Bila shaka ninastahili kuitwa babu 😎Unajiona una deserve kuitwa babu🤣
Asante sana kaka napokea pongezi zako😊🙏🙏Mada nzuri sana ila yataka watu wenye kuwa wavumilivu katika kusoma muda mrefu(Maneno/mchango mrefu). Kwa mfano mtu amekuibia ndizi yako moja shambani. Kiuhalisia huyo ukimkamata anastahili na ni haki yake aadhibiwe.
Ukimsamehe utakuwa hujamsaidia kwani kesho atarudia tena. Ukimwadhibu i.e. ukimpa haki yake huwezi jua - adhabu inaweza kumsababishia madhara makubwa e.g. kifo au ulemavu wa kudumu. Katika scenario hiyo, mtu anaweza kutumia hekima na kumwambia mwizi wake "Ondoka hapa" (manake hajasema Nimekusamehe). Mwizi ataondoka lakini atakuwa na dukuduku moyoni mwake kwamba ni nini kitafuata? Wewe uliyemwambia ondoka hapa, hujamtendea haki i.e. hukumpa haki yake mwizi wako - Kesho ataiba tena kwa mwingine.
Sasa tufanyeje(The way forward)? Mtu apime mwenyewe gharama na madhara ya kutoa adhabu kama Haki au Kughairi kutoa hiyo haki i.e. kuacha kutoa adhabu na kubaki kimya. Lakini endapo huyo mkosaji hatimaye atajirudi na kuja kuomba msamaha, basi inafaa umtamkie "Nimekusamehe".
TuliaaBila shaka ninastahili kuitwa babu 😎
Una uhakika ukiwa na majuto utakua na furaha na kisasi chakoKisasi ni haki ya aliyetendewa ubaya haijalishi atabaki na amani au majuto.
Kisasi kama haki ya mtendewa, ni pia sawa na umerudisha Ubaya kwa Mbaya wako. i.e. +1 - 1 =0. Tukija kwenye uhalisia, hesabu hilo halifundishi kweli wa maisha katika jamii tunamoishi kwani linajikita kwenye usemi "Kula na kulipa ndo mtindo wa kisasa". Tutaendelea kupiga na kupigwa na hiyo itaitwa kupigana. Hapo haitakaa itokee Amani -kila siku ni kuviziana katika madhaifu na kukomoana kama sehemu ya ulipizaji kisasi hata kama ni kisasi kwa kosa la mwaka juzi.Kisasi ni haki ya aliyetendewa ubaya haijalishi atabaki na amani au majuto.
yapi ni maoni yako kwenye hili nduguKisasi kama haki ya mtendewa, ni pia sawa na umerudisha Ubaya kwa Mbaya wako. i.e. +1 - 1 =0. Tukija kwenye uhalisia, hesabu hilo halifundishi kweli wa maisha katika jamii tunamoishi kwani linajikita kwenye usemi "Kula na kulipa ndo mtindo wa kisasa". Tutaendelea kupiga na kupigwa na hiyo itaitwa kupigana. Hapo haitakaa itokee Amani -kila siku ni kuviziana katika madhaifu na kukomoana kama sehemu ya ulipizaji kisasi hata kama ni kisasi kwa kosa la mwaka juzi.
Naomba kukunukuu hapa:Asante sana kaka napokea pongezi zako😊🙏🙏
Ni kweli mkosewa ndio inabidi apime ni namna gani afanye asamehe au amuwajibishe alimkosea
Kwenye comment yako nimejifunza kwa mfano huo iliotoa wa mwizi kukuibia shamani kwako
Kwamba kumwambia mwizi ondoka hapa haina maana umesamehe bali mtu husamewa kwa kua ameomba kusamehewa na wewe umeridhia huo msamaha
Na pia kamba mwizi akiwajibishwa sio makosa maana unakua kama una m shape hiyo tabia ya wizi either kurudi kuiba mara ya pili au kwenda kuiba kwa mwingine
Maana yaake mwizi kuadhibiwa ni haki yake msamaha ni busara tu
kwanza unapswa kuelewa kuwa kisasi hakileti furaha bali kinaleta uwiano.Una uhakika ukiwa na majuto utakua na furaha na kisasi chako
Tutumie Busara na Hekima kufanya maamuzi hata kama ni maamuzi magumu.yapi ni maoni yako kwenye hili ndugu
Ni kweli mkuu mi nilinukuu kutoka kwenye comment yakoNaomba kukunukuu hapa:
"Maana yake mwizi kuadhibiwa ni haki yake msamaha ni busara tu"
Hoja kubwa hapa ni inakuwa unamwadhibuje mwizi wako?
1. Ukimpeleka kwenye vyo vinavyoitwa ni vyombo vya Sheria, utasumbuliwa sana na pengine Haki isipatikane; ukajikuta umejijengea uhasama .....
2. Utapoteza muda wako mwingi bila faida yoyote eti "ninampatia haki yake mwizi wangu"
3. Hii ndo mbaya zaidi: Unampepeleka kwenye vyombo vya sheria na anahukumiwa kifungo 5yrs. Ndani ya muda huo wa kifungo (5yrs) Familia yake ambayo sio mlengwa wako, itapitia wakati mgumu sana kwa sababu ya wewe kutaka kutoa haki. Kwa hiyo umeadhibu hata wasio husika ktk kosa hilo.
Halafu, katika harakati za kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria huyo mwizi, ghafla linaibuka kundi la mashabiki na kuanza kutoa kipigo kwa mwizi na kwa bahati mbaya mwizi anapoteza maisha kama tunavyowaona wengi huko mjini. Wewe utaisaidia Polisi kutoa maelezo ya tukio lilivyotokea, Familia itakulaumu ........
Kwa mantiki hiyo mtu anaamua kujinyamazia Nafsi (Karma) ifanye kazi yake
Unafikiri ni hekima na busara ya aina gani ita override maumivu ya ndugu yako kuuliwa alafu huyo aliyemuua ndugu yako still yupo anadunda tu?Tutumie Busara na Hekima kufanya maamuzi hata kama ni maamuzi magumu.
Kama hupati furaha kwa kulipa kisasi basi kinyume chake ni majutokwanza unapswa kuelewa kuwa kisasi hakileti furaha bali kinaleta uwiano.
Anaelipa kisasi hatarajii furaha bali analenga kuleta uwiano juu ya kile alichotendewa.
Kwanini ke ndio apate majuto mwanaume yeye hawezi kupata magonjwa nakujutia?Mfano hivi visasi vya kwenye mahusiano kwamba me kacheat, ili pawepo na uwiano ke nae lazima acheat (kwa jina la kisasi). ambapo automatically kwenye kulipa kisasi kwa ke akipata magonjwa kwenye hii mode ndo majuto yanaanza.
Naomba nieleweke kwamba lengo la kisasi ni kuleta uwiano na sio kuleta furaha kwa sababu unaweza kulipa kisasi usipate furaha wala hayo majuto ila kukawa na uwiano wa matukio kwamba alifanyia hivi na mimi nimemfanyia hivi. inabaki hivyoKama hupati furaha kwa kulipa kisasi basi kinyume chake ni majuto
frequency ya majuto ya ke yatakuwa tofauti na me kwa sababu, huyu ke alikuwa anajaribu kuleta uwiano ambapo alikuwa na option ya kutokufanya hivyo kwahy anapofanya hivyo af ikamuathiri ndo safari ya majuto.Kwanini ke ndio apate majuto mwanaume yeye hawezi kupata magonjwa nakujutia?
Ila mkuu hakuna kitu kibaya kama kumfanyia ubaya mtu asiye na hatia,kisasi chake kinalipwa na nguvu nyingine kabisa ambayo engine wanasema Mungu.Kuna nyakati kisasi ni halali
Muhimu kisikuache na majuto
Hakuna mateso,sema mateso yanabaki kwa mfanya ubaya,anakuwa mtu wa kujistukia TU mkikutana wakati we ushatoka huko muda tuMbona haya ni mateso sasa dah