Msaidieni rafiki yangu achague lipi kati ya Ndoa au Scholarship (Elimu)?

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,807
13,054
Ni rafiki yangu wa kazi, tumpe Jina la John (yupo Halmashauri jirani). Amenipigia simu, na amenieleza jambo fulani nimeshindwa kumshauri.

Sababu ya kushindwa kumshauri ni kwamba; mi ningemjibu fasta kuwa PIGA CHINI NDOA fata SHULE ila "the problem is" alishani tahadharisha nisiwe "bias" katika majibu japo SIFAGILII NDOA.

Wakati ananiomba ushauri alisema ""Mr. Liverpool najua hupendi na hutaki kuoa, ila nakushirikisha hili jambo naomba usiwe bias, japo najua huzitaki ndoa". Na mimi nimeona niwashirikishe humu najua mpo mliopitia situation kama yake na mkapata jawabu.

SCENARIO:-
Mwaka jana kupitia matangazo ya Wizara ya Utumishi mimi na John tuliomba Scholarship ya PhD. Na ashukuriwe Mungu sotee tumepata post.

Wiki kama mbili zilizo pita Wizara ya Utumishi walituma barua za ruhusa kwa waajiri wetu ili waturuhusu kwenda shule pindi admission documents zitakapo tumwa. Mimi nilishirikisha familia na John akaenda kumshirikisha mchumba ake.

Flash back:-
John na mchumba ake walikutana tokea 2018. Uchumba wao ukaendelea kwa mabonde na milima mpaka kufika mwaka huu John alipo amua kuufanya officialize.

January/2022 alimpeleka kumtambulisha mchumba ake kwao. February/2022 John alituma mshenga kwa mchumba. Kwasasa wanaishi wote na wana mtoto mmoja. Na wapo kwenye process za ndoa kanisani. Wanahitaji kupanga tarehe, na mambo mengine ya ndoa.

The Problem:-
John alivyomshirikisha mchumba ake anasema mchumba alipoteza furaha ghafla na alinuna. Alikaa siku mbili haongei na John. Baada ya kubembelezwa sanaa mchumba ndio akafunguka.

1. Hataki John apande ndege aende kusoma kwasababu miaka mi3 ya masomo ni mingi, na yeye hawezi kuishi pekee yake TZ halafu John yupo nje.

2. Amesema na karudia sana hili jambo kwamba ""John akisepa tu basi atamkuta mchumba kashaolewa, kwamaana ye mchumba hawezi kuishi mpweke halafu John yupo nje"".

3. Mchumba kasema hawezi kukaa wiki moja bila kugongana na John, hivyo akisepa "Nani atakuwa anamtoa hamu?"

4. Mchumba analalamika John anamuacha vipi mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili na mama pekee yake. Kwahiyo mchumba anahisi kama John anataka kusepa nje amuachie mchumba malezi ya mtoto mwenyewe.

Kaeleza mengi ila kifupi MCHUMBA HATAKI JOHN AENDE SHULE HUKO NJE YA NCHI na KASEMA AKIENDA TU KAMKOSA.

Difficults:-
John yupo njia panda kwa maana NDOA anaitaka na SHULE anaitaka, ila hajui achague kipi aache kipi. John anamuhitaji mchumba Tena anamuhitaji sanaa awe mkewe. John anahitaji sanaa mtoto ake alelewe na mama aliyemzaa, kwamba kutafuta mwanamke mwengine ahitaji kabisaa. Ila mchumba kashamuonya kwamba akipanda ndege na yeye KAMKOSA.

Uzi tayari.
Ushauri wako Muhimu.

#YNWA
 
Ukweli ni kwamba uyo sio mwanamke wa kuoa, eti awez kukaa wiki bila kutiwa na jamaa duuuuh!! Ivi wanawake wa miaka hii mkoje? Eti akiondoka na yeye anaolewa!

Remind you MENS ARE RATIONAL AND WOMENS ARE EMOTIONAL. Mm wakati nasoma high school miaka ile likizo nilikua naenda dar kwa anko moja kati ya vitu alikua ananisisitizia in kwamba NISIACHE KUFANYA JAMBO LOLOTE LENYE KULETA MAFANIKIO KWAKO KWASABABU YA MWANAMKE.

Kwahyo ningekua mm ni ngerefer to kauli za mjomba wangu maana mfano wa kwanza alikua ananitolea uo wa km ukipata nafasi ya kwenda kusoma nje na una mke hata km akikataaa nenda kasome.

Achana na uyo mwanamke sio mwanamke wa kuaminika maana hayo maneno yake ni ya kumshika mapembe jamaa na mwanamke anaejua nini anakifanya asingeongea huo upuuzi.
 
Vipi wewe mkuu unaendaa kupigaaa kitabu au?
Mi Mzee baba lazima niende.

Yaani hata wafufuke wazazi wanikataze kwenda ila kwenda kwangu kusoma ni LAZIMA.

Nimesotea hii nafasi tokea 2020 imekuja kutiki 2022 halafu atokee mtu anikataze, aisee SITOMUELEWA KWA LOLOTEE.
Kama unaendaa ww inatoshaa mwachee John apambaniee anatakoona kwakwe n muhimuu kwa wkt husikaaa.
John ni mshikaji wangu Tena anatimiza miaka 33 mwaka huu.

Nimemwambia apige chini ndoa tupande ndege tukasome.

Mchumba na mapenzi yapo tu ila kusoma Kunategemea umri na majukumu(finance).

Kwahiyo kipindi hiki cha majukumu kidogo na umri wa ujana basi TUKAMALIZIE PhD kabisaa ili tumalizane na mambo ya Shule ibaki KUTAFUTA HELA tu.

#YNWA
 
Aende shule John watu, miaka 3 kwa masomo syo mingi kbsa, hlfu akae na kujua fursa ya kusoma haiji Mara mbili Mambo yana umri Ohooo.
Yap this is my concern.

Ana miaka 33 mimi nina miaka 32
Tukirudi atakua na 36 Mimi 35.

Then tutakuwa bado na umri wa ujana sanaa tu. Akimkosa huyu mchumba basi atapata mwengine.

#YNWA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom