Chief Isike
JF-Expert Member
- Jan 17, 2010
- 445
- 462
Wana JF
bila shaka hii kitu itaripotiwa vyema kesho na magazeti kadhaa hivi. Kwa yale yanayowahi online hata usiku huu wanaweza kutoa picha na stori. Nami kwa makusudi kabisa sitapenda 'kumaliza' stori zao hapa. Nimeamua kuiweka baada ya kuona it is likely to go unnoticed kwenye social media na different fora za mijadala na upashanaji habari online.
Msafara wa Rais uliokuwa ukienda mahali fulani msibani, nafikiri maeneo ya Kimara ulipata ajali baada ya mwongoza msafara, mtu wa pikipiki, kuanguka wakati wakiwa katika mwendo kuwahi huko msibani. Nimeambiwa eneo hilo la Kimara Corner ni 'maarufu' kwa ajali. Maana hata nikiwa maeneo hayo majira ya mchana pia kulitokea ajali nyingine tena.
Nilipita maeneo hayo muda mfupi mara baada ya ajali ya msafara wa rais kuwa imetokea na 'majeruhi' ameshaondolewa. Infact nilikutana na msafara wa Rais ukiwa tayari unatoka ulikokuwa unakwenda. Lakini wanahabari waliofanikiwa kuwepo just very very few minutes baada ya ajali kutokea, wakamwona askari mwongoza msafara aliyeanguka akingali chini wanasema rais alilazimika kushuka kwenye gari yake kwenda kumwangalia, kisha ambulance (kama mjuavyo siku hizi ni part ya entourage ya mkulu) ikageuza kumkimbiza hospitali.