Msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wapata ajali. Mmoja wa Watumishi wake afariki

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,361
Hii ni kwa mujibu wa ITV .

Taarifa zaidi zitawajia ....

UPDATE
Mhudumu wa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hamis Machenga amefariki dunia baada ya msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupata ajali nje kidogo ya mji wa Zanzibar na watu kadhaa wamejeruhiwa.
 
Mhudumu wa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamis Machenga amefariki dunia baada ya msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupata ajali nje kidogo ya mji wa Zanzibar na watu kadhaa wamejeruhiwa.
 
Kulikuwepo na Mchungaji mmoja kila alipokuwa akihudhuria kwenye misiba kauli yake Ni moja tu, Tunamshukuru Mungu Kwa tukio hili, na kama isingelikuwa hivi, pengine lingetokea kungetokea Jambo kubwa zaidi kuliko hili hiyo ndiyo ilikuwa moja ya faraja yake Kwa kila mahali ambapo kungetokea shida

Jamii ya pale ilimchukia na ikaanza kusema, labda yeye Kwa kuwa hajafiwa, Acha tutamwonesha,

Siku kukatokea harusi ktk mtaa anaoishi, akapewa Kadi yeye pamoja na familia yake kushiriki sherehe hizo,

Kumbe kuna Baadhi ya watu walipanga kuwaangamiza yeye na familia yake, chakula kilipotengwa tayari Kwa kula, simu ikapigwa Kutokea kwao mch, na tarifa ilikuwa Baba yake mzazi amefariki, Mchungaji pamoja na mkewe na wanae wawili ikabidi waondoke palepale na kumwacha mtoto wao mmoja Ili yeye alinde nyumba, wakaondoka hao wote bila Kula chochote, ispokuwa aliyebaki ndiye aliyekula, kumbe kwenye chakula kile kulikuwa kumewekwa sumu, na baada ya muda mfupi akapigiwa simu ya msiba wa mwanaye aliyemwacha harusini,

Ikabidi warudi wote Kwa ajili ya msiba wa mtoto wao, na alipofika wengi kumbe walikuwa wakimngoja atatoa kauli ipi, mch alisema kauli yake Ile Ile kuwa namshukuru Mungu Kwa hili, na pengine isingelikuwa tukio hili Nani ajuaye pengine lingetokea Jambo kubwa Sana kuliko hili!!

Watu wakaangua kilio hasa wale waliokuwa wamepanga kuiangamiza familia ya Mchungaji!!

Maneno aliyokuwa akiyatumia Mchungaji ni magumu Ila ni ukweli mchungu

Poleni wote mlioumia na ajali Hii, Mungu awape uponyaji wa haraka kwani Wazanzibari na Watanzania tunahitaji huduma yenu
 
Back
Top Bottom