Msafara wa Rais ulipata ajali leo asubuhi Kimara

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462

Wana JF

bila shaka hii kitu itaripotiwa vyema kesho na magazeti kadhaa hivi. Kwa yale yanayowahi online hata usiku huu wanaweza kutoa picha na stori. Nami kwa makusudi kabisa sitapenda 'kumaliza' stori zao hapa. Nimeamua kuiweka baada ya kuona it is likely to go unnoticed kwenye social media na different fora za mijadala na upashanaji habari online.

Msafara wa Rais uliokuwa ukienda mahali fulani msibani, nafikiri maeneo ya Kimara ulipata ajali baada ya mwongoza msafara, mtu wa pikipiki, kuanguka wakati wakiwa katika mwendo kuwahi huko msibani. Nimeambiwa eneo hilo la Kimara Corner ni 'maarufu' kwa ajali. Maana hata nikiwa maeneo hayo majira ya mchana pia kulitokea ajali nyingine tena.

Nilipita maeneo hayo muda mfupi mara baada ya ajali ya msafara wa rais kuwa imetokea na 'majeruhi' ameshaondolewa. Infact nilikutana na msafara wa Rais ukiwa tayari unatoka ulikokuwa unakwenda. Lakini wanahabari waliofanikiwa kuwepo just very very few minutes baada ya ajali kutokea, wakamwona askari mwongoza msafara aliyeanguka akingali chini wanasema rais alilazimika kushuka kwenye gari yake kwenda kumwangalia, kisha ambulance (kama mjuavyo siku hizi ni part ya entourage ya mkulu) ikageuza kumkimbiza hospitali.
 
kwa hiyo Rais ataenda kumtembelea kesho muhimbili au ataenda kutoa pole kwa wanafamilia nyumbani kwao??
 
Walikuwa wanakimbilia wapi? Baraza lenyewe bovu. Tena huenda kafurahi ili akamtembelee

Kwa mujibu wa Habari ya saa 2 ITV,Msafara wa Kikwete ulikuwa waelekea Kimara Kilungule kwenye Ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Dereva wa Ikulu Kaliyefariki Usiku wa kuamkia Jumamosi Tar.04.05 kwa ajali mbaya ya gari Binafsi iliyotokea maeneo ya Kimara Korogwe( another Black Spot between Ubungo-Kibaha) ila ITV walionyesha tukio la kuaga tu. Kuna jamaa alipost mchana huu (06.05.12) kuhusu tukio hili ZAHAMA YA KEBEHI ALIYOPATA. HAKURUDI TENA!
 
Watu wameshajadili sana hapa kuhusu mwendo kasi wa misafara ya magari ya viongozi wetu. Hata kwa akili ya darasa la kwanza mwendo kasi hauwezi kuwa njia mojawapo ya kulinda usalama wa kiongozi. Kinachotakiwa ni kuwa na gari bullet/bomb proof na sio kukimbiza gari.

Obama na madhira yote anatumia beast inayotembea kama kinyonga. Hapa tunakimbiza gari eti kwa usalama? Na ukuangalia wakati mwingine utadhani ni mashindano ya Formula 1, wanakwenda zigzag utafikiri ni computer game kumbe wanamwendesha kiongozi wa nchi.
 
kwa hiyo Rais ataenda kumtembelea kesho muhimbili au ataenda kutoa pole kwa wanafamilia nyumbani kwao??

hajatumia ofisi kwa shughuli binafsi hapo! kwani kuna msiba wa kitaifa maeneo ya kimara?
angeanguka rais na ku RIP hiyo safari yake binafsi si ingetutia hasara ya kuingia kwenye uchaguzi.
kama vipi mbona hahudhurii kipaimara cha mtoto wa matonya jirani yetu, au yeye si mtz
 
Kipindi cha pasaka pale dar nilipigiwa simu na rafiki yangu kutoka nchi za nje akiniaribu kuwa kuna uwezekano wa dhoruba kali kutokea pwani yetu, akanitahadharisha kutokaa karibu na bahari.

Nilikuwa pale St. Joseph, au posta ya zamani, nikakuta daladala zimestopishwa na mara pikipiki ilipita kwa kasi sana ikifuatiwa na magari mengine kama manne hivi moja likiwa na nembo ya Ikulu, watu wakasema anakimbilia Dodoma kuogopa dhoroba ya bahari asije kufunikwa na maji hapa.

Nilichoshangaa ni kasi ile kwani kosa kidogo linaweza sababisha madhara makubwa. Hivi hata huyo mwongoza msafara kilichosababisha kuumia zaidi huenda ni magari yaliyomfuata kutokana na mwendo kasi.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hajatumia ofisi kwa shughuli binafsi hapo! kwani kuna msiba wa kitaifa maeneo ya kimara?
angeanguka rais na ku RIP hiyo safari yake binafsi si ingetutia hasara ya kuingia kwenye uchaguzi.
kama vipi mbona hahudhurii kipaimara cha mtoto wa matonya jirani yetu, au yeye si mtz

Alipoombwa na Slaa kwenda kwenye matembezi ya kutafuta pesa za michango mlikaa kimya!
 
ila wajiulize juzi kafa dereve jana wamemuaga jana hiyohiyo apate ajali mwingine bado tu wanauamin huo mwendo kasi? sijui familia zao nani anawapa matunzo tena baada ya baba kupoteza maisha kwa kazi ambayo inarisk kiasi hicho.
 
Wana JF

bila shaka hii kitu itaripotiwa vyema kesho na magazeti kadhaa hivi. Kwa yale yanayowahi online hata usiku huu wanaweza kutoa picha na stori. Nami kwa makusudi kabisa sitapenda 'kumaliza' stori zao hapa. Nimeamua kuiweka baada ya kuona it is likely to go unnoticed kwenye social media na different fora za mijadala na upashanaji habari online.

Msafara wa Rais uliokuwa ukienda mahali fulani msibani, nafikiri maeneo ya Kimara ulipata ajali baada ya mwongoza msafara, mtu wa pikipiki, kuanguka wakati wakiwa katika mwendo kuwahi huko msibani. Nimeambiwa eneo hilo la Kimara Corner ni 'maarufu' kwa ajali. Maana hata nikiwa maeneo hayo majira ya mchana pia kulitokea ajali nyingine tena.

Nilipita maeneo hayo muda mfupi mara baada ya ajali ya msafara wa rais kuwa imetokea na 'majeruhi' ameshaondolewa. Infact nilikutana na msafara wa Rais ukiwa tayari unatoka ulikokuwa unakwenda. Lakini wanahabari waliofanikiwa kuwepo just very very few minutes baada ya ajali kutokea, wakamwona askari mwongoza msafara aliyeanguka akingali chini wanasema rais alilazimika kushuka kwenye gari yake kwenda kumwangalia, kisha ambulance (kama mjuavyo siku hizi ni part ya entourage ya mkulu) ikageuza kumkimbiza hospitali.

jamaa ana afinity na misiba
 
Safari hii ilikuwa zamu ya Dereva wa Ikulu Marehemu Deokalyus Makwasinga, JK is Man of the People.Yes ofcose!
 
Hahahaha! Mi naona leo rais aende tu kwenye msiba kutoa pole, huyo wa Muhimbili drs wahakikishe hafi hadi rais aende kumpa pole jumanne.
kwa hiyo Rais ataenda kumtembelea kesho muhimbili au ataenda kutoa pole kwa wanafamilia nyumbani kwao??
 
Wana JF

............ulipata ajali baada ya mwongoza msafara, mtu wa pikipiki, kuanguka wakati wakiwa katika mwendo kuwahi huko msibani. .....

Kama ni yule niliyewahi kumuona mie hata sishangai, Jamaa huwa anaendesha pikipiki kwa mbwembwe sana, kuna wakati anaachia mikono yote halafu yeye analala kwa nyuma wakati pikipiki iko kwenye speed kali saaana, hii nimeshuhudia kwa macho yangu, na siku nilipoona nikasema, huyu lazima atakuja kupata ajali mbaya!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom