Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Misafara ya viongozi mara zote huongozwa na sweeper ambao hutangulia mbele kwa speed zaidi ya 100kmph na mara nyingi ni kukwepa ma-sniper labda wakifika mjini ambako wanapadhibiti.
huenda huyo dereva hakuwa mzoefu au vumbi lilimtibua ndio maana akaingia bondeni
hilo dude ni V8 na lina speed mpaka 220kmph au 140mph ila ukilikosea ndani ya sekunde linakutoa barabarani
Ni ulichosema kiongozi!!

ila:
1.Wanaharakishia wapi?
2.kwani nchini kwetu kuna masniper?

Mi naona wanahatarisha tu maisha yao....anyway waendelee hivyo hivyo...

sisi tutawapa pole yakitokea
 
Watu 4 wamejeruhiwa katika msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya gari moja kuanguka huko Nanguruwe wakati wakitoka mtwara kuelekea Tandahimba.

View attachment 396831

View attachment 396808

Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula,

Chanzo: Radio One

=======
UPDATES:

Msafara wa Makamu wa Rais wa wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo taarifa zinasema kati ya majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu Rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari lililokuwa limebeba baadhi ya waandishi wa habari walioambatana na ziara hiyo, liliacha njia na nusura lipinduke.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba, imekuwa ikitajwa kutokuwa na kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Neno mwendokasi halipo kwenye ajali za viongozi.....
 
Poleni majeruhi. ..MOLA awabariki mpone upesi
 
Hawa madereva huwa mnawapata wapi???????
Kwa muonekano wa hiyo barabara
*zaidi ya speed 80km/hr lazima gari ikutoe nje
*Ni hatari kukimbia kwenye barabara usiyo ifahamu vyema(hupiti kila siku)
*Safari ndefu,zina viwango na masharti yake.
 
Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzani Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara

Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
 
hiyo bara bara ipo vizuri tuu sema hao viongozi wanaendeshwa speed sana na pia hizi gari za Japan ni nyepesi sana katika kona inakutoa kirahisi wangefanya Tafiti ya kutosha ili kupata gari nzito na si hizi nyepesi sana ila nzuri body tuu...
 
Poleni sana waliopatwa na mkasa huo mungu awape wepesi viongozi wetu!!!ila hilo jina la hicho kijiji sijafurahishwa nalo!!!
 
Duh pole makamu wa raisi nina wasi wasi na mazingira ya ajali hiyo ngoja tusubiri taarifa rasmi kwa wahusika.
kwa hiyo unataka kuhusisha ajali hii na zile tetesi? ama sijakuelewa vyema mkuu
 
Nimem zoom Afande kubwa nikapendezwa na uchapu wake katika uokoaji
Zoom uniambie wewe unaona nini?
 
Attachments

  • 1473434464963.jpg
    1473434464963.jpg
    68.2 KB · Views: 28
Back
Top Bottom