Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzani Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara

Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
 

Attachments

  • IMG-20160909-WA0013.jpg
    IMG-20160909-WA0013.jpg
    20.5 KB · Views: 76
  • IMG-20160909-WA0014.jpg
    IMG-20160909-WA0014.jpg
    79.8 KB · Views: 72
Yaani mnazidi kumtia makamu stress na maoni yenu

Ni juzi tuu kakanusha kujiuzulu

Leo msafara wake ndio hivyo na ninyi mitazamo hasi

Amani kwako mama,najua wanayemchukia ni baba ila wanamaliza hasira kwako
 
Inawezekana alizoea kuendesha kwenye lami.
Pole sana
 
Ajali inatokea mara nyingi gari ya mbele ikifunga breki ya ghafla!nilishakuwa sana kwenye convoy hilo ndio huwa tatizo gari moja inaweza kuleta ajali ya gari zote
 
Madereva wakamatwe na kupandishwa kizimbani kama inavyofanyika kwa madereva wa usafiri wa umma.
 
Tengenezeni barabara... Hizo ndo adha za kila siku za wananchi wenu, oneni na nyie....
 
Kwa dereva ambaye si mzoefu wa balabala aina hiyo plus mwendo kasi lazima "agalauke"
 
Back
Top Bottom