Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,079
- 15,357
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Mayungi, ameshiriki zoezi la usafi katika Mkoa wa Mbeya pamoja na Balozi wa Mazingira Tanzania, Michael Msechu, vijana wa vyuo, wafanyabiashara wa eneo la Kabwe Standi, viongozi wa chama pamoja na madiwani.
Zoezi hilo limeendelea kuhamasisha umuhimu wa utunzaji wa mazingira na kuongeza juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea Dira ya Taifa ya 2050.
Aidha, viongozi hao wameendelea kusisitiza mshikamano wa wananchi katika kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani na salama kwa vizazi vijavyo, huku wakitoa rai ya kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika agenda ya Tanzania ya Kijani.
Pia soma ~ Utaratibu wa uzoaji Taka Jiji la Mbeya ni shida, zimezagaa mitaani licha ya Wananchi kulipa ili zizolewe