Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

namwona bodi gad wa Makamu wa raisi amekuwa nes sasa ghafla hizi kazi jaamni poleni wote mlio patwa na matatizo jamani p[oleni sana
 
Mwandishi wa thread punguza u******u r last paragraph does not make sense. How come barabara inayotajwa kutokua na kiwango cha kuridhisha (broken road/rough road) na kuruhusu magari kwenda mwendo Kasi! !!![emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Basically madereva wa serikali (sio wote) competence yao ni ya ku-question, halafu wamezoea kukimbia ovyo kwa kua wanafagiliwa njia kwenye motorcade za viongozi. So in rough road tena zenye mbavu za mbwa na mambio yao huwa wanazipiga sana chini gari , further land cruiser hutumia coil spring which reduces stability of the car at high speed on a learned or bumps road na hivyo matokeo yake mweleka.

Angekua raia ungesikia mwendokasi /ametumia vilevi huku wanaendesha vyombo vya moto. Anyway pole kwa waliopatwa na ajali na Mwenyezi Mungu awajaalie recovery ya haraka Inshallah
 
Watu 4 wamejeruhiwa katika msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya gari moja kuanguka huko Nanguruwe wakati wakitoka mtwara kuelekea Tandahimba.

View attachment 396831

View attachment 396808

Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula,

Chanzo: Radio One

=======
UPDATES:

Msafara wa Makamu wa Rais wa wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo taarifa zinasema kati ya majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu Rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari lililokuwa limebeba baadhi ya waandishi wa habari walioambatana na ziara hiyo, liliacha njia na nusura lipinduke.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba, imekuwa ikitajwa kutokuwa na kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Kwa mwonekano wa haraka hawa walikuwa ni maofisa usalama na kwa aina ya gari walilokuwemo hawakupaswa kuumia kiasi hiki, wanaonekana wanamaumivu makali lakini hawavuji damu ni dhahiri hawakuwa wamefunga mikanda hivyo walirushwa rushwa ndani ya gari wakati likibiringita.

Hili la maofisa usalama kutokuzingatia usalama tumeliongelea siku mbili zilizopita walimruhusu rais kupanda juu ya jengo lililoko kwenye ujenzi bila kuwa na vifaa vya usalama kazini, hebu mtizame huyu hapa chini hana kifaa cha usalama hata kimoja na dhahiri hilo eneo halikuwa salama ndio maana kila mmoja alitafuta sehemu ya kujishikiza.

1.png


Watizame na hawa waliolala chini hawakupaswa kuumia kwa kiwango hicho kama walikuwa wamefunga mikanda (safety belt)

aqaq-jpg.396808
 
.....hiyo barabara haifai kwa matumizi ya binadamu.....maaana wananchi wamepiga kelele tangu uhuru mpaka leo hakuna cha lami au mila gari likibeba korosho linapita kudondosha ukiwa na kindoo kidogo ukilifuatia unajaza.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom