Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali

Chanzo cha ajali ni kipi?
Itakuwa mwendo kasi na kuyumbisha yumbisha magari barabarani. Mara nyingi misafara ya wakubwa haizingatii zile 30km au 50km wao ni kasi tu huku wakichezesha magari barabara yote. Sijui kwanini traffic huwa hawa wakamati na kuwapiga faini au kuwapa notification kama magari mengine
 
..haya ndio matokeo ya kukimbia mno kwenye hii misafara...mi huwa najiuliza huwa wanakimbia nini?kama lengo ni kuona matatizo ya watu wao...hizi speed kali za nini??..kwani hapa tuko iraq ama somalia?..kwamba tunaogopa labda kulipuliwa?.....speed kali kwenye misafara ya viongozi tz ziangaliwe...labda siku moja watajifunza akidhurika mheshimiwa....lakini tayari mifano ipo...ajali mbili tayari zikimuhusisha yule naibu waziri wa tamisemi...bado hawajifunzi??
 
Akiwa anatokea mjini mtwara kuelekea wilaya ya tandahimba makamu wa rais msafara wake umepata ajali eneo la nanguruwe sehemu ambayo barabara ina rasta nyingi sana na kuwa tishio kwa dereva mgeni wa hilo eneo
1473420475092.jpg
 
Pole kwa Majeruhi wote mliofikwa na ajali hii mbaya Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi mpone haraka mtoke hospital muendelee na majukumu yenu Ameen.
 
Si alisema tumwombee au kuna watu wana mwombea kinyume na alichoomba tumuombee???
 
Kwa hiyo barabara inaonyesha kuwa dereva hakuwa na uzoefu wa ku handle gari yake kulingana na wembamba wa barabara na kona zake na style yake ya uchongaji barabara (kuchongwa huku mtaro na huku mtaro) ukiplus na speed kali ya sababu za kisiasa lazima V engine iongee makavu yake.
 
Watu 4 wamejeruhiwa katika msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya gari moja kuanguka huko Nanguruwe wakati wakitoka mtwara kuelekea Tandahimba.

View attachment 396831

View attachment 396808

Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula,

Chanzo: Radio One

=======
UPDATES:

Msafara wa Makamu wa Rais wa wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo taarifa zinasema kati ya majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu Rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari lililokuwa limebeba baadhi ya waandishi wa habari walioambatana na ziara hiyo, liliacha njia na nusura lipinduke.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba, imekuwa ikitajwa kutokuwa na kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

V.I.P Protection team tunajua kuwa moja ya mafunzo yenu ni kwenda " spidi " tena hasa mkiwa na " taita " sehemu za maporini ambazo ni Enemies Potential Targets ila niwashaurini tu muwe mnazingatia kiwango cha spidi, njia husika na uimara wake. Tunajua kuwa mna kazi ngumu na nzito ya Kiulinzi lakini basi umakini pia unahitajika ili msipatwe na madhara yanayoweza kuzuilika kama hayo. Poleni sana na nawatakia matibabu mema wote wahanga wote wa hiyo ajali na nina amini watakuwa tu vizuri na kuendelea na majukumu. Muda mwingine msiwe mnatawaliwa mno na Convoy Protocal Principles kwani huwa zinakubali kulingana na mazingira na si lazima iwe vile vile kama mlivyojifunza. Tandahimba huko maporini na spidi yote hiyo kubwa mliokuwa nayo wapi na wapi?
 
Ni kweli kabisa hawa watu wana mafunzo ya hari ya juu kabisa ya uendeshaji gari(high speed emergence driving) sasa sijui kwanini huwa unatokea uzembe ambao ni wakitoto kabisa ambao hata kwa dereva L anaweza ku control. Hatutaki kusikia uzembe kama huu tena kutokea sababu ni kama kudharirisha idara.
 
Pole jamani. Anapata ajali kiongozi wa nchi halafu tufanyeje watanzania? Huyu aendelee kuwa salama ili tuendelee kuwa na kiongozi wa kitaifa. Ajali nazo, yaani kile unachokitegemea na shetani anaangalia hapohapo, haendi kwa kile kinachotugawa na kutuchonganisha na kututakia mabaya ya kutumbukizwa kisimani!
 
Poleni sana,Mwenyezi atawapa wepesi wa kupona haraka na kurejea kwenye majukumu yenu.
 
Ni kweli kabisa hawa watu wana mafunzo ya hari ya juu kabisa ya uendeshaji gari(high speed emergence driving) sasa sijui kwanini huwa unatokea uzembe ambao ni wakitoto kabisa ambao hata kwa dereva L anaweza ku control. Hatutaki kusikia uzembe kama huu tena kutokea sababu ni kama kudharirisha idara.

Haya mambo za ajali hizi za Kizembe za Watu wa idara nimeanza kuzisikia sana awamu iliyopita na na naona hii nayo wameshaanza kupata urithi wa hizi ajali. Sikuwahi kusikia ajali kama hizi hasa za Watu wa PSU wakati wa Awamu za Mwalimu, Mwinyi na hata Mkapa. Ni aibu ya kutukuka kwa Watu wa Idara kupata ajali hizi mara kwa mara na mnawatia pia aibu Trainers wenu. Tafadhali tunaomba leo iwe mwanzo na mwisho kusikia kuna ajali yoyote imetokea katika misafara inayohusisha high profile V.I.P's nchini Tanzania. Nyie huwa mnapewa extraordinary training hivyo msitutie wasiwasi tuanze kuhisi kuwa labda " hamjakwiva ". Yangu ni hayo poleni sana Wahanga, Mwenyezi Mungu awapiganie na majukumu mema.
 
Back
Top Bottom