Msaada wa njia bora ya kuondoa nyuki waliowekamakazi kwenye chumba changu

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,072
1,697
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa tanzania na kazi iendelee

Wanajamvi, nimekuwa na tatizo la nyuki kuweka makazi ndani kwenye dirisha la nyumba changu hali iliyolelekea kuhama kabisa na kukiacha kile chumba

Sina hakika lini nyuki hawa walianza kuweka kambi ila leo hii usiku wa tar 08/09/23 majira ya saa 3 usiku niliporejea tu nyumba nikakuta luku imeisha hivyo nikalazimika kuingia na tochi ya simu

Nilipoingia chumban ghafla nikakutana na nyuki kama wawili hv wapo kitandan

Nikastaajabu kwamba hawa nyuki wametoka wapi, ghafla ikabid niangalie dirishan

Nilipoangalia tu dirishan nikakuta nyuki wengi sana wametanda juu ya dirisha ikanibid nifunge nyumba na kuondoka.

Baadhi ya watu kutokana na iman zao wakasema hao ni ndugu zangu wamenikumbuka, wengine wakasema nitafute moto niwaondoe

Wengine wakasema ninunue rungu, sasa mpaka hapa nipo njia ya panda sijui ni njia gan bora ya kuwaondoa wale nyuki

Hivyo bas kwa yeyote mwenye ufaham juu ya jambo hili naomba anijuze tafadhal
 
Ngoja giza liingie,wakojolee tena mchana kutwa unywe maji mengi ili uwamwagie kojo la haja!kesho yake asubuhi hutawakuta!
 
Kwa Chini au pembeni ya dirisha Choma kitu chochote ambacho kitatoa Moshi mzito Mkuu ,
Just chukua extra caution wasikupige tukio la kutisha .
 
Moshi....

Hawapendi Moshi...hudhani "msitu" unaungua....

Halafu mkuu uache "UCHAFU"...isije ikawa ndani unaacha "uchafu wa maganda ya matunda" ama matunda yaliyooza na kuacha unyevunyevu

Jengine

Kuta za nyumba(ndani ama nje)zikipakwa rangi zifuatazo ujue "nyuki" huwa rafiki zako

-NJANO

-MCHANGANYIKO WA BLUU NA KIJANI

-MCHANGANYIKO WA NYEKUNDU NA PURPLE(MAGENTA)

Ndio maana wajanja hupaka rangi zisizo hizo

#SiempreJMT

Karibu Wanzuki
 
Back
Top Bottom