Msaada wa namna ya kudeal na Mpangaji msumbufu

Msaada wa namna ya kudeal na Mpangaji msumbufu

Fanya kama wazungu wanavyo fanya
Kabla ya kumpangisha aoneshe bank statement inayoonesha kipato chake ..uridhike kwanza ana kipato kweli au anabangaiza...

Kingine aweke dhamana ya hela ...mfano kuna mikataba unaweka Kodi ya miezi miwili kama dhamana ya kuharibu kitu....ikitokea mnasumbuana unampa notice haraka...
Pesa unamrushia ya dhamana kama hajaharibu kitu au humdai....
Upanga ndo wanafanya hivyo, unaweka deposit
 
Bora uweke lodge ...wanakupa chako mapema na ikifika asubuhi Saa nne unawagongea waondoke hata kama waliingia Saa nane usiku
Lodge nayo unaweza kuta anayefaidi ni msimamizi kwa kubeba za short time
 
Hiv hii ya kuingia saa nane usiku nankutolewa asbh saa nne imekaaje. Mana pale unaandka tarehe uloingia na kutoka inayofuata. Nahis wateja ndio hatuelewi
Hotel za waswahili asubuhi inahesabiwa ni siku.
Kuna sehemu niliwahi enda nikaambiwa vyumba hawapangishi asubuhi, hadi jioni saa 2
 
Hizo sheria kwangu zitakuwa applicable na mtu mwenyewe kama mstaarabu, mkataba wako kabla ujaisha nakupa notice halafu halafu nishakupa notice uniambie nikusubiri miezi3 daaah wewe unaweza?
Lazima uwahusishe Serikali za Mtaa ambao watakwambia mvumilie akulipe au mpe Notice ya Miezi 3
 
Habarini Wanajamvi,

Kuna mpangaji wangu ni msumbufu balaa kulipa kodi anasumbua (ana deni la miezi 2) na bill ya maji ndiyo kabisa hajisumbui.

Naombeni msaada jinsi ya kudeal na wapangaji wasumbufu kama hawa maana nataka nishike hata mali yake moja ya gharama asije akahama usiku usiku.

Asanteni, nasubiri ushauri wenu
Ukisubiri ataondoka mwenyewe bure. Nenda serikali za mtaa omba barua ya wito akigoma, siku inayofuata omba kibali chukua na mjumbe mmoja vunja kitasa. Katika vitu vyake uza kitakacho kulipa kodi na bill yako mpe vingine aende zake.

Kama vitu vyake havina thamani fukuza tu.
 
Acha ujinga, jenga nyumba yako acha kupigia kelele nyumba za wenzio, unajua gharama ya ujenzi wewe. Me natoa vitu vyako nje na makofi nakupiga unadhani nyumba ni matako.
Unaongea tu, utajikuta unapigwa wewe
 
Wewe jifanye sababu upo nyuma ya keyboard hivi wale maboss waliotolewa vitu NHC unawajua ? Wewe ni Nani usitolewe vitu nje wakati hulipi hela ya pango ulisaidia hata Pesa ya tofali kwenye hio nyumba au umeona nyumba ni ya baba yako unakaa tu bure ? Endelea kujifanya utalala nje siku moja
Pale washafika hadi mahakamani ie Billcanas
 
Lazima uwahusishe Serikali za Mtaa ambao watakwambia mvumilie akulipe au mpe Notice ya Miezi 3
Sheria ya kodi ya pango hakuna sehemu inayosema ni miezi3 inataja kumpa mtu Mda unaoingilia akilini lakini hakuna muda specific kama hiyo sheria ipo hapa ilete tuone. Yaani miezi3 sikuoni unapigiwa simu upokei unakimbia HALAFU nikuvumilie miezi3 hata mungu atanichoma moto
 
Ninaweza kukupa ushauri kadhaa juu ya jinsi ya kushughulikia mpangaji msumbufu na namna ya kushikilia mali yake kama hatua za mwisho. Hapa kuna hatua unazoweza kuzingatia:

1. Wasiliana na mpangaji: Anza kwa kuzungumza na mpangaji wako kwa njia ya kirafiki na uwasilishe wasiwasi wako juu ya malipo ya kodi na bili za maji. Jaribu kuelewa sababu ya kutolipa na ongeza umuhimu wa kulipa madeni yake kwa wakati.

2. Weka maandishi: Ikiwa mazungumzo ya awali hayajazaa matunda, andika barua rasmi kwa mpangaji wako. Taja malimbikizo yake ya kodi na bili za maji na wapeleke barua hiyo kwa njia ya kuthibitika ili kuwa na rekodi ya mawasiliano.

3. Panga ratiba ya malipo: Kwa matakwa ya pande zote, unaweza kujaribu kufikia makubaliano ya kulipa madeni yake kidogo kidogo kwa muda fulani. Kwa mfano, unaweza kukubaliana kuwa anaweza kulipa nusu ya kodi na bili za maji katika kipindi cha mwezi mmoja.

4. Toa ilani ya kisheria: Ikiwa mpangaji wako haendelei kulipa au kutoshirikiana, unaweza kufikiria kutoa notisi ya kisheria. Hii inaweza kuwa notisi ya kulipa madeni ndani ya muda fulani au kuwaachisha mkataba wa kupangisha.

5. Lipa hatua za kisheria: Ikiwa mpangaji wako bado anashindwa kulipa na hajali notisi ya kisheria, unaweza kuchukua hatua zaidi za kisheria. Hii inaweza kujumuisha kufungua kesi ya kumwondoa mpangaji au kuchukua hatua zingine za kisheria zinazotolewa katika eneo lako.

6. Shikilia mali: Ikiwa hatua zote za kisheria zimeshindwa, unaweza kujaribu kushikilia mali ya mpangaji wako kama njia ya kurudisha madeni yaliyopotea. Kabla ya kufanya hivyo, hakikisha kushauriana na mwanasheria na kuzingatia sheria za eneo lako kuhusu utekelezaji wa mali.

Ni muhimu kukumbuka kwamba sheria na taratibu za kukabiliana na mpangaji msumbufu zinaweza kutofautiana kulingana na eneo lako na mikataba ya kupangisha. Ni vyema kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa mwanasheria au mamlaka husika ili kuhakikisha kuwa unafuata taratibu sahihi.

Natumai ushauri huu utakusaidia kushughulikia hali hi

yo. Kumbuka kuwa ni muhimu kuwa na rekodi sahihi ya mawasiliano yote na kuzingatia taratibu za kisheria ili kulinda maslahi yako kama mwenye nyumba.
Ushauri mzuri kwa sisi wapangaji sugu
 
Inategemea na namna ulivyomuonesha heshima, Mimi enzi zangu hadi siku nahama Mwenye nyumba anang'ang'ania niendelee kukaa hata bure kutokana na heshima na uungwana niliwahi kumuonesha, imagine 😅
HAO MKUU WAPO. UNAMFANYA KAMA FAMILIA YAKO. HATUNA SHIDA MPANGAJI ANAKUJA ANAKWAMBIA NDUGU YANGU MOJA MBILI TATU HALI YANGU SIYO KIUKWELI MTU KAJA KWA UNYENYEKEVU ANAOMBA MSAADA HUYO HATA KAMA NI MIEZI4 KAJA KUNIPA TAARIFA NA NAJUA HALI ANAYOPITIA ATAENDELEA KUKAA.


UNPIGIWA SIMU UPOKEI MARA UNAZIMA, MARA UNARUDI USIKU KAMA ZOMBI UTAKI KUONYESHA UTU TUNAKUFANYIA UNYAMA TU UNATOKA UTAKE USITAKE
 
Sheria ya kodi ya pango hakuna sehemu inayosema ni miezi3 inataja kumpa mtu Mda unaoingilia akilini lakini hakuna muda specific kama hiyo sheria ipo hapa ilete tuone. Yaani miezi3 sikuoni unapigiwa simu upokei unakimbia HALAFU nikuvumilie miezi3 hata mungu atanichoma moto
Umenichekesha sana. Ila nina uhakika we huna nyumba bali vistoo
 
Back
Top Bottom