Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,174
Amani iwe juu yenu Waungwana,
Miezi kadhaa iliyopita tume hudhuria ndoa iliyofungwa kati ya Kaka na Dada Mabinamu (Mtoto wa Mjomba na Shangazi), Harusi ilifana na pande zote mbili zilishiriki kikamilifu.
Sasa tumepata habari tena kua kuna Kaka na Dada (Mtoto wa Mama mkubwa na Mama Mdogo) wamependana na wanataka kufunga ndoa,
Ajabu familia imetikisika, wazazi wa pande zote mbili wanapinga kwa afya na nguvu zote, kua hawawezi kuoana kwa kua wale ni kaka na dada hivyo ni ndugu.
Sasa nimeshindwa kuelewa jambo hili, Kwani watoto wa Mjomba na Shangazi almaarufu kama BINAMU sio NDUGU???
Kwanini jamii ikubali ndoa zao na ikatae ndoa za Watoto wa Mama mkubwa na Mama mdogo???.