Msaada: Ni hatua gani kisheria naweza chukua dhidi ya uonevu wa kampuni ya EROLINK ?

Mtanganyika008

New Member
Sep 6, 2021
1
0
Habari wana Jamii Forums, samahanini kwa wale wenye ujuzi wa kisheria, naomba msaada juu ya ni hatua gani za kisheria naweza kuchukua kwa kampuni inayoitwa EROLINK.

Kampuni imekua inaleta usumbufu sana kwa wafanyakazi wake, hasa pale mikataba yao ya kazi inapoisha, na uwa haiwasilishi michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii kama NSSF licha ya kua imekua ikiwakata wafanyakazi wake kila mwezi, kampuni hii imekua ikilalamikiwa miaka mingi sana kutokana na historia yake ya ubabaishaji, usumbufu na uonevu ikiwemo dharau ya hali ya juu kwa wafanyakazi wake bila kuwahi kuchukuliwa hatua yeyote na mamlaka husika ikiwemo mifuko ya kijamii na wizara husika, na mmoja ya mtu ambae ni mjivuni na msumbufu mkubwa wa kampuni hii ni mhasibu wao anejulikana kwa jina la Eric.

Huyu amekua akijinasibu waziwazi kua anafanya chochote atakacho ikiwemo kukwamisha michango ya wafanyakazi hata kama ni miaka kadhaa na hakuna wa kumfanya kitu. Sasa naombeni ushauri wenu ni namna gani naweza kuishitaki hii kampuni kwa kutopeleka michango yangu NSSF na wakati mkataba wangu na wao ulishakiwsha zaidi ya miaka mitatu sasa, na kila nikienda NSSF hakuna majibu ya kueleweka zaidi ya porojo tu, kiasi kwamba nakua na shaka kuna wezekana kuna mazingira ya kushirikiana kati ya EROLINK na NSSF ili kuwakwamisha wafanyakazi walioachishwa kazi au kumaliza mikataba yao kuweza kupata stahiki zao. Naomba msaada wa ushauri wa kisheria na namna ninavyoweza kuonana na waziri husika na mashirika hayo ili kuweza kuwachukulia hatua.
 
Back
Top Bottom