DOKEZO Kampuni ya M-gas Cooking Limited imetutelekeza wafanyakazi kwa miezi miwili bila kutulipa mshahara na kuanzisha kampuni mpya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni miongoni mwa wafanyakazi (150+) wa M-gas Cooking Limited. Hatujalipwa mshahara wa mwezi wa pili bila taarifa yoyote zaidi ya hapo tulipokea taarifa kwa njia ya email kwamba kampuni imeshindwa kutulipa mshahara kutokana na matatizo yao ya kibenki na masuala yote ya kampuni tumuone Andron Mendes ambae alikuwa mkurugenzi wa kampuni kabla ya kutangaziwa mkurugenzi mpya, ila kilichotushtua zaidi ni kuondolewa kwenye mifumo ya mawasiliano ya ofisi na ofisi za kampuni kufungwa mwanzoni mwa mwezi wa tatu.

Maboss waliokua wakitusimamia wamefungua kampuni mpya M-gas Resources na kuhamishia shughuri zote za kampuni huko huku sisi tukiterekezwa bila kulipwa mishahara na bila kuvunjiwa mikataba yetu. Michango yetu ya NSSF haijalipwa tokea mwezi wa 12 mpaka sasa na hatuna hata termination letter ili iweze kutusaidia kupata stahiki zetu.

Hii ni njia mojawapo tumeamua kuitumia ili suala letu liweze kuwafikia wahusika ngazi za juu tuweze kupata msaada na kukomesha wamiliki wote wa kampuni wenye nia ovu kwa vijana wanaopambana kujikwamua kimaisha.

IMG_3961.jpeg

Ahsante
 
View attachment 2941282
Ahsante
Poleni sana.
Fungueni shauri Commission for Mediation and Arbitration (CMA) haraka sana.
Website yao ni hii hapa kwa taarifa zaidi:https://www.cma.go.tz/

Pia, wamemuweka huyu hapa chini kama contact person wao kwa Dar es salaam, unaweza kumpigia pia maana ni muwakilishi wa CMA Dar es salaam kulingana na taarifa za kwenye website yao, atakuelekeza cha kufanya.
CMA DAR ES SALAAM

P.o.Box 79590 Dar es Salaam. In charge Honourable Usekelege Mpulla Mobile No: 0655922448
 
Poleni sana ,sasa kama CEO anatumia gmail basi kuna shida hapo,kama kampuni ina fedha za kutosha kwanini wasikope sehemu nyingine kuwalipa nyinyi? Tafuteni mwanasheria fasta afungue shauri CMA na ikibidi mahakani kuzuia mali za kamupuni.
 
Ma CEO wa ki bongo wanataka waishi maisha Kama ma CEO wengine duniani wao na familia zao tu. Ila ikija kwenye kulipa mishahara on time, kuendesha kampuni kumataifa wako kibongobongo zaidi.
 
Sure ,wanajilipa mishahara mikubwa sana ,wanapangiwa masaki ,wanasomeshewa watoto shule za kimataifa ,halafu local staffs wanaopambana jua lao mvua yao kuingiza mapato wanaishia kulamba mishahara PENENGE haifiki hata tarehe 10.
 
Hata wateja tumeibiwa. Mimi nimenunua gas ya kutumia mwezi, baada ya siku 2 wakazima mitambo, siwezi kutumia na salio hawajarejesha. Wamenyang'anya wateja wote mitungi, mimi nimegoma kuwapa wakitaka mtungi warejeshe salio na hela ya mita waliyoniuzia. Wajaribu kusogea kwangu nipo palee nawasubiri na mapanga. Mendes ni mhalifu
 
Poleni sana.
Fungueni shauri Commission for Mediation and Arbitration (CMA) haraka sana.
Website yao ni hii hapa kwa taarifa zaidi:https://www.cma.go.tz/

Pia, wamemuweka huyu hapa chini kama contact person wao kwa Dar es salaam, unaweza kumpigia pia maana ni muwakilishi wa CMA Dar es salaam kulingana na taarifa za kwenye website yao, atakuelekeza cha kufanya.
CMA DAR ES SALAAM

P.o.Box 79590 Dar es Salaam. In charge Honourable Usekelege Mpulla Mobile No: 0655922448
Asante sana
 
Back
Top Bottom