Mlume Ndago
Member
- Jul 28, 2025
- 41
- 53
Habari wakuu,
Poleni na msiba wa kitaifa tunaoendelea kuuomboleza.
Moja kwa moja nijikite kwenye mada husika kwa kuwaomba msaada wa mawazo na ushauri kwa ujumla.
Mimi nina cheti cha kuzaliwa lakini cheti changu ni cha zamani sana kimetoka tangu mwaka 1988.
Katika cheti changu jina langu limekosewa herufi moja ya mwisho, na majina ya mama yangu pia yamekosewa mawili la kwanza na la mwisho katika yale majina yake matatu .
Msaada ninaohitaji ni kujua;
1.Endapo nitaenda ofisi za RITA nahitajika kwenda na nyaraka zipi ili niweze kurekebishiwa jina langu na majina ya mama yangu?
2.Je, naweza kwenda ofisi yoyote ya RITA iliyo karibu nami katika wilaya yoyote Tanzania au lazima niende katika ofisi ambayo ipo katika wilaya niliyozaliwa?
Yangu ni hayo tu, naombeni ushirikiano wenu kwa yeyote mwenye kujua au kufahamu anaweza kutoa ushauri au msaada kwa ku comment
Asanteni na muwe na siku njema...🙏