Msaada: Mwenye uwezo wa kutafsiri ndoto zangu hizi tafadhali

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,962
6,891
Habari wakuu,

Nimekwama tafadhalini. Naamini kila mtu humu ana talanta yake ambayo amebarikiwa, Naamini pia huku kuna wakina Yusuf walioweza kutafsiri ndoto kipindi cha utawala wa Wamisri kwa Israel na ndiyo maana sinaga tabia ya kudharau watu. Ni marefu kidogo ila nakuomba soma hadi mwisho.

Tuanzie hapa, kuna ndoto nimekuwa nikiziota na nimeshindwa kuzielewa kabisa na ubaya zinamuhusisha baba yangu na uchumi wangu. Nitaeleza kwa uchache maisha yangu ili mjue wapi mtaanzia.

Mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro, Nimelewa na mzazi mmoja ambae ni baba maana walishaatengana na mama, Mahusiano ya mimi na wazazi wote yapo vizuri asilimia zote japo sometimes tunapishana lakini huwa najitahidi kila upande ujue kwamba mtoto wetu hana ubaguzi.

Baada ya mimi kumaliza elimu yangu mkoani Arusha ambapo nilikuwa nikiishi na baba wote tulihamia Kilimanjaro ambapo ni nyumbani kwao wazazi wangu yaani kwa Bibi na ilikuwa hivyo kutokana na baba kufail kimaisha kiasi cha kurudisha mpira kwa kipa, Mimi nilikuja kuhama pale kijijini na kuhamia Dar ambapo ninaishi hadi sasa.... So ipo hivi Mama anaishi Mwanza, Baba anaishi Moshi na Mimi ninaishi Dar es Salaam.

Ndoto ya Kwanza: Niliota kama ninaishi pale kijijini yaani mimi,baba na bibi na katika harakati zangu nilikuwa na tabia ya ku-save pesa kiasi kwaajili akiba ambapo nilikuwa nahifadhi mahali fulani katika chumba ninacholalia, Siku moja tukiwa sebuleni Mimi, Baba na bibi ndipo baba akaniomba hela na kwa kuwa mimi sipendi kumzoesha vibaya kwa kuwa namjua tabia yake kupenda kunijaribu hasa kwenye hela mimi nikamjibu "hapana sina kitu mzee" ndipo wote wakaanza kunishambulia kwa maneno yaani Baba na bibi kwamba mimi ni mtoto mwenye roho mbaya sana na mchoyo huku baba akitoa kakibunda ka sh.300,000 akinionesha na kuniuliza "unasema huna hela hizi ni nini?" Mimi kumbukumbu zinakuja kurudi ndo nakumbuka kwamba mbona kama hizi ni hela zangu ninazohifadhigi chumbani, ndipo nikatoka mbio kwenda kucheki ninapohifadhi na kweli nikakuta hazipo so, it mean kwamba baba alizichukua.... Lile tukio lilinikwaza sana nikarudi na kujaribu kumsihi kwamba hizo hela ni kwaajili ya akiba ya maisha ya baadae hivyo najiribu kuchanga ili ike inisaidie nijitegemee baadae lakini bado alidai kutokana na tabia yangu ya roho mbaya hatorudisha zile hela na akaapa kabisa huku mama yake pia akimjaza kichwa, Mimi nilipoona vile ikabidi niwe mpole na kujaribu kumshawishi japo anipatie 150,000 abaki na nyingine lakini akagoma kabisa kunipatia....Na ndoto ile hadi nakuja kushtuka ilionesha kwamba ile 300,000 kwenye ulimwengu ule ni hela nyingi mno kiasi kwamba nilirudi chini kama mtu asie na dira yaani kama aliefilisika huku waliohusika kunifilisi wasijali chochote.

Ndoto ya pili: Hii ni baada ya kama week baada ya kuota ile ya kwanza ipo Hivi, Hii imenirudisha kipindi naishi na baba katika room aliyopanga jijini Arusha, Mwanzo mimi naonekana najaribu kuweka saving yangu kwenye moja ya shelves zilizopo pale ndani na wakati huo baba alikuwa kazini... Saving yangu ilikuwa ni Tsh.300,000, Ilipofika usiku baba alikuja na watu wawili ambao mwanza alivyoingia nao ndani walionekana kama marafiki zake, Lakini nilipomtaza baba usoni hakuwa na furaha na alikuwa busy sana kukusanya vitu baadhi huku akiwapatia wale watu wawili, Sasa wakati akiendelea na hiyo shughuli ya kuwakusanyia kwa bagati mbaya akaenda kugusa sehemu ambayo ina saving yangu ndipo nikamuwahi na kumuambia 'Ngoja baba hapa kuna hela zangu', baada ya kusema vile tu ndipo mmoja ya wale watu wawili akachomoa panga na kusema 'We tulia kaa pale nitawakatakata mapanga sasahivi, hizo hela ndo tumezijia' kumbe bhna wale watu walikuwa majambazi na vile walivyokuja na baba yangu ni kama walimteka aje nao hadi nyumbani kuwapatia kila alichokuwa nacho... Hii ndoto pia hadi inafika mwisho ilionesha kwamba mimi baada ya kuchukuliwa ile saving yangu tsh 300000/= basi maisha yetu mimi na baba yalibadilika na kufeli maisha kiujumla.

Sasa maswali ninayojiuliza kwanini ndoto hizi zinamuhusisha baba yangu na kuporomoka kwa uchumi wangu?, Na Je, ni kwanini 300,000 zimejirudia kama saving yangu ambapo kwenye ulimwengu ule zimeonekana kama ndiyo Nguzo ya uimara wangu?

Naombeni mnisaidie kutafsiri, natanguliza shukran🙏
Mshana Jr
 
Wewe ni dini gani? Wengine tuna amini katika kila tunacho kipata tuna tolea fungu la 10 kama sadaka ya ulinzi inawezekana hiyo ni tahadhari una pewa kama huwa hutoi fungu la 10 anza sasa huja chelewa mali zako zitakuwa na ulinzi madu madu wala nzige hawatoshambulia, wala hutozaa mapoza 🙏
 
Wew ni dini gani? Wengine tuna amini katika kila tunacho kipata tuna tolea fungu la 10 kama sadaka ya ulinzi inawezekana hiyo ni tahadhari una pewa kama huwa hutoi fungu la 10 anza sasa huja chelewa ....... malizako zitakuwa na ulinzi madu madu wala nzige hawatoshambulia .... wala hutozaa mapoza 🙏
Hili ndilo jibu sahihi chukua hatua.
 
Wew ni dini gani? Wengine tuna amini katika kila tunacho kipata tuna tolea fungu la 10 kama sadaka ya ulinzi inawezekana hiyo ni tahadhari una pewa kama huwa hutoi fungu la 10 anza sasa huja chelewa ....... malizako zitakuwa na ulinzi madu madu wala nzige hawatoshambulia .... wala hutozaa mapoza 🙏
sawa mkuu nimekuelewa sana, nashukuru... Je, fungu la kumi natakiwa kutoa kanisani, msikitini au hata nikitoa kumpa mtu msaada pia inafaa?
 
Wasaidie masikini , yatima, wazee , hata kanisani kwako unapo abudia ....fanya kwa imani.... tia nia.... toa kama unamtolea MUNGU ....
 
Habari wakuu,

Nimekwama tafadhalini. Naamini kila mtu humu ana talanta yake ambayo amebarikiwa, Naamini pia huku kuna wakina Yusuf walioweza kutafsiri ndoto kipindi cha utawala wa Wamisri kwa Israel na ndiyo maana sinaga tabia ya kudharau watu. Ni marefu kidogo ila nakuomba soma hadi mwisho.

Tuanzie hapa, kuna ndoto nimekuwa nikiziota na nimeshindwa kuzielewa kabisa na ubaya zinamuhusisha baba yangu na uchumi wangu. Nitaeleza kwa uchache maisha yangu ili mjue wapi mtaanzia.

Mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro, Nimelewa na mzazi mmoja ambae ni baba maana walishaatengana na mama, Mahusiano ya mimi na wazazi wote yapo vizuri asilimia zote japo sometimes tunapishana lakini huwa najitahidi kila upande ujue kwamba mtoto wetu hana ubaguzi.

Baada ya mimi kumaliza elimu yangu mkoani Arusha ambapo nilikuwa nikiishi na baba wote tulihamia Kilimanjaro ambapo ni nyumbani kwao wazazi wangu yaani kwa Bibi na ilikuwa hivyo kutokana na baba kufail kimaisha kiasi cha kurudisha mpira kwa kipa, Mimi nilikuja kuhama pale kijijini na kuhamia Dar ambapo ninaishi hadi sasa.... So ipo hivi Mama anaishi Mwanza, Baba anaishi Moshi na Mimi ninaishi Dar es Salaam.

Ndoto ya Kwanza: Niliota kama ninaishi pale kijijini yaani mimi,baba na bibi na katika harakati zangu nilikuwa na tabia ya ku-save pesa kiasi kwaajili akiba ambapo nilikuwa nahifadhi mahali fulani katika chumba ninacholalia, Siku moja tukiwa sebuleni Mimi, Baba na bibi ndipo baba akaniomba hela na kwa kuwa mimi sipendi kumzoesha vibaya kwa kuwa namjua tabia yake kupenda kunijaribu hasa kwenye hela mimi nikamjibu "hapana sina kitu mzee" ndipo wote wakaanza kunishambulia kwa maneno yaani Baba na bibi kwamba mimi ni mtoto mwenye roho mbaya sana na mchoyo huku baba akitoa kakibunda ka sh.300,000 akinionesha na kuniuliza "unasema huna hela hizi ni nini?" Mimi kumbukumbu zinakuja kurudi ndo nakumbuka kwamba mbona kama hizi ni hela zangu ninazohifadhigi chumbani, ndipo nikatoka mbio kwenda kucheki ninapohifadhi na kweli nikakuta hazipo so, it mean kwamba baba alizichukua.... Lile tukio lilinikwaza sana nikarudi na kujaribu kumsihi kwamba hizo hela ni kwaajili ya akiba ya maisha ya baadae hivyo najiribu kuchanga ili ike inisaidie nijitegemee baadae lakini bado alidai kutokana na tabia yangu ya roho mbaya hatorudisha zile hela na akaapa kabisa huku mama yake pia akimjaza kichwa, Mimi nilipoona vile ikabidi niwe mpole na kujaribu kumshawishi japo anipatie 150,000 abaki na nyingine lakini akagoma kabisa kunipatia....Na ndoto ile hadi nakuja kushtuka ilionesha kwamba ile 300,000 kwenye ulimwengu ule ni hela nyingi mno kiasi kwamba nilirudi chini kama mtu asie na dira yaani kama aliefilisika huku waliohusika kunifilisi wasijali chochote.

Ndoto ya pili: Hii ni baada ya kama week baada ya kuota ile ya kwanza ipo Hivi, Hii imenirudisha kipindi naishi na baba katika room aliyopanga jijini Arusha, Mwanzo mimi naonekana najaribu kuweka saving yangu kwenye moja ya shelves zilizopo pale ndani na wakati huo baba alikuwa kazini... Saving yangu ilikuwa ni Tsh.300,000, Ilipofika usiku baba alikuja na watu wawili ambao mwanza alivyoingia nao ndani walionekana kama marafiki zake, Lakini nilipomtaza baba usoni hakuwa na furaha na alikuwa busy sana kukusanya vitu baadhi huku akiwapatia wale watu wawili, Sasa wakati akiendelea na hiyo shughuli ya kuwakusanyia kwa bagati mbaya akaenda kugusa sehemu ambayo ina saving yangu ndipo nikamuwahi na kumuambia 'Ngoja baba hapa kuna hela zangu', baada ya kusema vile tu ndipo mmoja ya wale watu wawili akachomoa panga na kusema 'We tulia kaa pale nitawakatakata mapanga sasahivi, hizo hela ndo tumezijia' kumbe bhna wale watu walikuwa majambazi na vile walivyokuja na baba yangu ni kama walimteka aje nao hadi nyumbani kuwapatia kila alichokuwa nacho... Hii ndoto pia hadi inafika mwisho ilionesha kwamba mimi baada ya kuchukuliwa ile saving yangu tsh 300000/= basi maisha yetu mimi na baba yalibadilika na kufeli maisha kiujumla.

Sasa maswali ninayojiuliza kwanini ndoto hizi zinamuhusisha baba yangu na kuporomoka kwa uchumi wangu?, Na Je, ni kwanini 300,000 zimejirudia kama saving yangu ambapo kwenye ulimwengu ule zimeonekana kama ndiyo Nguzo ya uimara wangu?

Naombeni mnisaidie kutafsiri, natanguliza shukran
Mshana Jr
Post in thread 'Hizi sio ndoto za kawaida' Hizi sio ndoto za kawaida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom