Hii inategema na mtoto yupoje.
Mfano kwa wangu:
Nina watoto wawili wa 9 yrs(Std 3) wakiume na 6 yrs wakike(Top class)
Hawa wanajua katuni zote mpaka wajukuu wa katuni.
Ila wao ratiba yao wanaiweza.
Wanaosoma English Medium School:
Time Table:
06h30:Kuamka kunywa chai
07h00:Kwenda Shule(Wanatembea Maana tupo Karibu na Shule)
15h00:Wanatoka shule(Wanakuwa wameishakula shule)
15h15:Wanaenda Madrasa(Chuo)
18h45:Baada ya kuwa mameswali Salat Isha,wanatoka chuo wanakuja Home
19h00 - 20h00:Home Work,kisha chakula
20h00 - 09h00:Katuni kwenda mbele mpaka usingizi unakuwakuta hapo hapo
Weekends:
08h00 - 10:00 Madrasa(Chuoni)
10h00 - 12:00 Weekend Home works
12h00 - 14:00 hatuni na kula
14h00 - 15:00 Kulala,hapa wengine wanapoteneza baadhi ya siku
15h00 - 18h45:Madrasa (Chuo)
Nimechogundua kwenye Catoons ni kwamba wame Gain alot.
Asikuadangaye mtu,mtoto ambae anatizama katuni ana uelewa mkubwa sana kuliko mtoto asietizama katuni.
1)Kwangu nime experience uwezo wao wa Lugha ya Kiingereza umekuwa kwa kazi ya ajabu sana.
Na hii ilikuwa kwamba wanafuatilia vitendo na maamrisho,na mara nyingi neno kama likiwapita basi wanauliza,na ukiwaambia hawasahau tena,maana mmoja akisahau mwingine anamkumbusha,is really good.
2)Uwezo wa kufanya maamuzi pia ni tofauti sana,mtoto mwenye kutizamana Catoons wengi wanamaamuzi ambayo ni sahihi sana,na uwezo mkubwa wa kujieleza na kukwepa maswali ya mitego na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo.
Unaweza kukuta kwamba mtu mzima kichwa kinakuzunguka hata hujui ufanye maamuzi yapi,basi wakati huo utashangaa anakuambia Baba au Mama siufanye hivi itakuwa hivi(Jaribuni hilikufanya majaribio mtagundua)
3)Kujiamini:watoto wengi wenye kutizama catoons wanajiamini sana,hata mwalim akimuita basi jua anakwenda with confidence na yupo tayari kwa lolote.Na hata mzazi ukimuhoji basi anajiamini sana na kutoa maelezo sahihi.
Kama mtoto anapenda Catoons mwachie tu,atakapokuwa basi ratiba ya Shule ndio itakayobadilisha maisha yake.La Sivyo ukimdhibiti hapo basi atatoka nje atakutana na watoto waliopinda kama ni wakike basi wataanza kuchezeana uchi Sasa kipi bora.
Mie wangu niliwaachi,mpaka umri huo wameofikia ndio ratiba ya shule na Madrasa ika waset outomatically,na wala walikuwa hawana michezo ya ajabu nje,unajua lazima tukubali sasa hivi unavyomlea mwanao sio mwenzio anavyomlea mwanae,kuna watoto wadogo sana wanamambo ya kikubwa,na hii inaanzia katika makuzi yao na familia zao.Kwahiyo fanya kitu kitakachofanya mtoto awe busy.
Yangu ni Hayo