Wow, nimepitia comments zote na nyingi zinafurahisha, zingine zinachekesha, zingine zinasikitisha. nashukuru sana mawaidha ya Faizafox. Mimi nilishamaliza malezi ya watoto wadogo niko kwenye malezi ya watoto wakubwa (believe me it is also a challenge)
Katuni ni nzuri sana ila unatakiwa kujua ni aina zipi aziangalie. Kuna Nursery rhymes, alphabet, numeracy, science, geography, life skills, etc. Kwa mfano, kuna cartoons za "Going to market" au going to hospital, at the police station, visiting a farm, etc, etc, ..... Ukizichagua vizuri unaweza usihitaji kumpeleka "tuition".
Kikubwa kilichokuwa kinanisumbua ni uwiano mbaya wa kinachofundishwa huko chekechea (usually horrible, hasa kwa sisi tusioweza kupeleka watoto kwenye shule za uhakika) na ideal situation inayoonyeshwa kwenye video. Walimu ni wabaya, wasiojua kufundisha, kiingereza kibovu, etc. Hata hizi wanazoita academy ni tatizo. Ole wako mwanao awe anafundishwa na mhindi halafu unampa kanda za England. Atachanganyikiwa kwenye pronounciation.
Pamoja na hizo cartoons, mzoeshe kuangalia documentaries hasa za wildlife, history, arts and cultures. Mara nyingi ukiwa karibu na mwanao unakuwa ndio "role model" kwa hiyo unachopenda wewe anajitahidi kukipenda. Jitahidi uwe unafuatilia vitu vya muhimu ambavyo unafikiri vitamjenga kwenye all spheres of child development. Of utmost importance, ni kupata muda wa kumjengea uwezo wa ku-interact na watu halisi. Mazungumzo ya kifamilia, kwenda kwenye bustani au shambani, ujijengee utaratibu wa "technology free hour" ili muweze kuzungumza pamoja, hasa wakati wa chakula, kufua, kufagia mazingira, etc.
naomba niishie kapa kwa sasa.