Msaada: Mwanafunzi wa kike kupotea kwao haonekani siku ya 5

mtungu

JF-Expert Member
Dec 15, 2021
249
403
Ni binti mdogo tu wa jirani yangu huku Tanga mtaa wa kange kasera, kamaliza darasa la saba mwaka huu anasubiri majibu.

Baba yake ni bodaboda tu hana kipato kikubwa na hua anachelewa kurudi nyumbani, siku kama tano nyuma alirudi nyumbani usiku binti hayupo.

Alipomuuliza mkea anamjibu hajui, wakaanza kumtafuta mpaka leo hajapatika ila cha ajabu binti ana simu na hua anamtumia baba yake sms kuwa asisumbuke kumtafuta yupo sehemu salama Mkoa wa Mtwara.

Polisi kaenda anasema hajapewa ushirikiano wa kutosha, kesho nitakutana nae anipe picha ya binti na namba anazowasiliana nazo ili apate msada, kijana mwenzangu hana raha anateseka kwa kumuwaza nwanae hana uwezo ajui afanyaje.
 
Back
Top Bottom