Msaada:mtoto wa miaka 12 analazimishwa kuolewa.

vunjajungu

JF-Expert Member
Nov 25, 2011
576
240
Habari wanajamvi
poleni na majukumu ya kila siku,mwezi wa nne mm na mke wangu tulibahatika kupata mtoto.kutokana na wote kua na majukumu ya kazi tuliona ni vyema tutafute mdada wa kazi wa kutusaidia.
Tukawasiliana na jamaa yetu anaeishi dodoma atusaidie kwa hilo.akafanikiwa kumpata na kumsafirisha hadi tanga.
Alipofika tulishangaa kuona ni msichana mdogo sana lakini baadae tukakubaliana tukae nae huku tukimsomesha kwani alikua hajui kusoma wala kuandika.mshahara wote walikua wanachukua wazazi wa binti.sasa tokea mwezi huu wa nane uanze mama mtoto anasema anataka mwanae arudi sababu kuna mtu amelipa mahali hivyo anataka kumuoa.
binti hataki analia kila siku lakini mama yake anatishia kutushitaki kwa kumng'ang'ania mwanae!naombeni ushauri tufanye nn?
 
report kwa watu wanaoshughulika na haki za watoto pamoja na wamama ili kuhakikisha hicho kitu hakitokei tena mngewahi mweleze hyo situation ila msimrudishe kwa sasa hadi mhakikishe anausalama wakutosha huko mtapata ushauri wakitaalan zaidi
 
Habari wanajamvi
poleni na majukumu ya kila siku,mwezi wa nne mm na mke wangu tulibahatika kupata mtoto.kutokana na wote kua na majukumu ya kazi tuliona ni vyema tutafute mdada wa kazi wa kutusaidia.
Tukawasiliana na jamaa yetu anaeishi dodoma atusaidie kwa hilo.akafanikiwa kumpata na kumsafirisha hadi tanga.
Alipofika tulishangaa kuona ni msichana mdogo sana lakini baadae tukakubaliana tukae nae huku tukimsomesha kwani alikua hajui kusoma wala kuandika.mshahara wote walikua wanachukua wazazi wa binti.sasa tokea mwezi huu wa nane uanze mama mtoto anasema anataka mwanae arudi sababu kuna mtu amelipa mahali hivyo anataka kumuoa.
binti hataki analia kila siku lakini mama yake anatishia kutushitaki kwa kumng'ang'ania mwanae!naombeni ushauri tufanye nn?

Tamaa mbaya hiyo! huyo mama naye aliolewa akiwa na umri huo? ulimwengu unaelekea wapi jamani? Anyway nimekusifiu kwa jinsi ulivyofanya mpaka sasa unae huyo binti. sheria ya ndoa inasema binti ataolewa kuanzia umri wa miaka 15 mpaka 18 kwa ridhaa ya wazazi wake! miaka 12 kuolewa huo ni UBAKAJI na wote watakao husika hakika hawatakwepa panga la miaka (wazazi na mwoaji). ila ukienda polisi au haki za watoto ukasema huyo binti nio mfanya kazi wako wa ndani napo ni balaa linaweza kukutokea hapo, hiyo ni CHILD LABOUR!
 
km anataka kukushitaki mwambie kachelewa sana. kwa mujibu wa sheria ya ndoa,mtoto wa miaka 12 hawezi kuolewa,labda km angekuwa na miaka 15 ila na penyewe isingewezekana kwa kuwa bado anasoma.
 
Kaka katoto kadogo umekakandamizia child labour? Hebu jaribu kufuta hiyo kauli kuwa ni mfanyakazi wako wa ndani
 
Back
Top Bottom