Nina mashaka huyu mtoto si wangu, ushauri wako wa muhimu mwana MMU!

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Assalam mwana MMU, pole na majukumu ya kimaisha.

Niende moja kwa moja kwenye mada, mwaka 2015 baada ya kuhitimu elimu nilanza harakati zangu kitaa, nilitoka mkoa niliokulia na kuja kanda ya ziwa Mwanza.

Maisha ya kuwa mwenyewe, sijaoa, nikajikuta nakula kwa mama mmoja alikua na sehemu ya kuuzia chakula jirani na napoishi.

Miezi kadhaa baada ya kuzoeleka pale alikuja binti pale mfanyakazi, alikua mchangamfu sana, akawa ndie mtoa huduma kwetu.

Kitabia mimi si mtu wa kufahamiana na watu haraka sana, lakini kwa ule uchangamfu nikakuta nishazoeana nae. Hakuwa binti mkubwa sana kiumri, hata 20 kipindi hicho alikua hajafikisha bado.

Kuna kipindi nilianza kuwa nabanwa sana na majukumu, narudi nyumbani usiku sana, nikapunguza kwenda pale kula, siku moja nikakutana na yule mama, akanishauri kama nimebanana sana wale mabinti watakuwa wanakuletea chakula nyumbani, niliafikiana nae na chakula kikawa kweli kinaletwa nyumbani.

Tatizo lilianzia hapa, kwani mazoea ya yule binti yalizidi sana, japo nikiri sikuwahi kumtamkia swala lolote la kuwa mpenzi, kuna siku nilikua sijatoka nafanya usafi nyumbani, mida ya jioni, ghafla binti akaja na chakula, ilikua mapema sana, alivyofika utani ukaanza mambo mengi, nikajikuta tayari nimesex pasipo kupanga, na ukizingatia ni muda mrefu nimetoka nyumbani ilikua rahisi sana kushawishika (wanaume wanajua).

Wiki kadhaa kupita yule binti aliombwa na yule mama ahame aende kwa mwanae akamsaidie kazi za nyumbani, alivyofika kule akagundulika ni mjamzito!

Kasheshe ilianzia hapa, binti alikataa kata kata kusema, lakini nafsi ilinisuta, ikabidi nimwambie yule mama ukweli, nikamvuta pembeni, nikamweleza, "mama, inawezekana pengine huu ujauzito ni wa kwangu, maana nimewahi sex na huyu binti" mama aliniuliza sasa tunafanyaje? nikamwambia asiutoe nitaulea, kazi ikaanza!

Yule binti kumbe alikuwa mwanafunzi ametoroka kwao, na ameacha shule, kazi nyingine ikawa hapo! japo yule mama alisema tupambane tuu tuone itakapoishia, akampiga mikwara yule binti nae akae kimya asiseme kwa mtu!

Nikawa na hudumia, sasa mabadiliko ya ujauzito, binti akawa anafanya vituko, kuna siku halali nyumbani anasingizia alikua kwangu, kuna kipindi akapoteza vyombo vya watu masufuria makubwa aliyaacha nje usiku yakabebwa ikabidi nilipe, mambo yalienda mpka yule mama akatuchoka ikabidi anishauri nimrudishe kwao!

Basi nikaongea nae uzuri alikubali, nikampa fedha za kutosha nikamsindikiza akaondoka, alivyofika nyumbani tuu, akawa hapatikani tena hewani (anadai alipoteza simu).

Muda ulienda, nimefuatilia sana toka 2016 mpaka nikakata tamaa mwezi huu wa sita 2022 yule mama akanipigia usiku akaniambia yule binti amekuja yupo kitaa, nilijawa na shauku na furaha sana.

Nikamtafuta hatimae tukaonana, tulikaa sehemu, akanihadithia vingi, ikiwepo kupoteza simu, na jinsi alivyojifungua, akaenda Kenya akaolewa, huko akampata mtoto mwingine, wakaachana na huyo mume na sasa ndo amekuja huku Mwanza kunitafuta.

Nilimpa pole nyingi, na nikamuuliza anataka nini kutoka kwangu, akadai anataka TUISHI WOTE, nikamwambia sahivi nina mchumba, na nishamtambulisha nyumbani, nitafanyaje? akatulia, nikamwambia nimtafutie 3milion afungue biashara zake, lakini mtoto anipe akaanze shule.

Ah, nilivyomwambia swala la mtoto kunipa alibadilika, akasema haiwezekani, huyo mtoto ametoka nae mbali, hawezi kunipa alelewe na mama mwingine, kama ninamtaka mtoto tuishi wote yeye na wanae hao wawili sasa!

Muda ulienda nikamwambia aniletee mtoto nimwone kwanza, aligoma, nikamsisitiza sana, mwisho akakubali japo kishingo upande sana, nilianza kupata mashaka hapa!

Mtoto alivyoletwa doh, aisee hata kitu kimoja sijafanana nae, nilijitahid sana kujikaza, nisiulize, akawa kama ameshtuka hivi, akawa anaongea maneno mengi, mara mtoto wako huyu, mnafanana sana nywele sema nimemsuka hutaona, kidogo mwanao huyu ona alivyokuzoea haraka!

Akawa anamwambia mtoto mwite baba, mambo yalikua mengi, nikampiga mtoto picha tukaagana, nilipatwa na hofu sana, nikaona hapa naenda kupigwa, halafu kibaya dogo anafanana sana na kuna jamaa namfahamu!

Dogo hataki kuachiwa na mama yake, hata dakika moja!

Samahani sana kwa urefu wa story, lakini walau nimeamua kutoa matukio ya muhimu, ili niweze kupata ushauri mzuri, nifanyaje??

Natanguliza shukrani!
 
kasheshe ilianzia hapa, binti alikataa kata kata kusema, lakini nafsi ilinisuta, ikabidi nimwambie yule mama ukweli, nikamvuta pembeni, nikamweleza, "mama, inawezekana pengine huu ujauzito ni wa kwangu, maana nimewahi sex na huyu binti" mama aliniuliza sasa tunafanyaje? nikamwambia asiutoe nitaulea, kazi ikaanza!
Kasheshe uliianzisha mwenyewe kwa kufanyakosa la kiufundi hapo eti inawezekana"Hii mimba ni ya kwangu" Kusex na mwanamke hakukupi assurance ya kua baba wa mtoto hata kama ni mkeo. Ili mwanamke umpe mimba labda awe mjinga au aamue yeye nwenyewe ila huyo binti seeems alikua mjanja.

So wewe ulishoboka-ea ujauzito usiokuhusu kisa ulilala nae binti akaona atambae na biti ili siku zisonge, Pole kwa machungu na siku nyingine usirudie kosa hilo. Baba wa Mtoto anayemjua ni mama na sio wewe ujipe Authority ya kusema hii mimba yako Unless there's strong Controversy-ies
 
"kuna siku nilikua sijatoka nafanya usafi nyumbani, mida ya jioni, ghafla binti akaja na chakula, ilikua mapema sana, alivyofika utani ukaanza mambo mengi, nikajikuta tayari nimesex pasipo kupanga, na ukizingatia"............hivi ulipata degree ya fani gani? Loh wasomi wetu hovyoo sana
Kuna kudondoka, na elimu yangu haihusiani kabisa na madhaifu yangu!!
 
Kasheshe uliianzisha mwenyewe kwa kufanyakosa la kiufundi hapo eti inawezekana"Hii mimba ni ya kwangu" Kusex na mwanamke hakukupi assurance ya kua baba wa mtoto hata kama ni mkeo. Ili mwanamke umpe mimba labda awe mjinga au aamue yeye nwenyewe ila huyo binti seeems alikua mjanja.

So wewe ulishoboka-ea ujauzito usiokuhusu kisa ulilala nae binti akaona atambae na biti ili siku zisonge, Pole kwa machungu na siku nyingine usirudie kosa hilo. Baba wa Mtoto anayemjua ni mama na sio wewe ujipe Authority ya kusema hii mimba yako Unless there's strong Controversy-ies
Nakubali, nilikosea hapa!
 
"kuna siku nilikua sijatoka nafanya usafi nyumbani, mida ya jioni, ghafla binti akaja na chakula, ilikua mapema sana, alivyofika utani ukaanza mambo mengi, nikajikuta tayari nimesex pasipo kupanga, na ukizingatia"............hivi ulipata degree ya fani gani? Loh wasomi wetu hovyoo sana
Mbona unajikuta mkamilifu sana?? Sasa mambo ya degree yanahusiana nn na sex? Yaan unamaanisha wenye degree ndo hawana nyege au?? Kila mtu hua anakosea at some point hata awe na PhD
 
Pole sana.....nimependa umavyojibu comments na kukiri makosa yako.....inaonesha ukomavu wako....usimuoe huyo mwanamke ni mjanja mjanja.....endelea tu na mchumba wako......waka usije ukauza mechi akakupachikia mimba ingine......mtoto akupe umuanzishe shule hataki acha kaa mbali wala usitume hata mia.....kama ni wako atamleta tu
 
Shukran sana!
 
Back
Top Bottom