msaada '''mboga'' - kwa kiingereza

nadhani wazungu(waingereza) hawana concept ya kitoweo,iwe nyama,wali,mchicha vyote ni vyakula tu na vina majina yake, licha ya kuwa katika milo yao huwa kuna main dish na vikolombwezo vingine i.e main dish inaweza ikawa hata nyama na kikolombwezo ikawa salad, au main dish inaweza ikawa wali na vikolombwezo ikawa njegere na samaki!
 
bustani ya mboga: kwa kiingereza "vegetable garden"
kiasa cha mboga: 1.kiasi cha kuridhisha 2.kiasi kidogo cha kitu k.m chai
mboga za majani: kwa Kiingereza: "vegetables"
ni mboga: ni rahisi sana (mtaani)

Tafadhali -kwa nini kiasi kikubwa cha michango hapa ni mchanganyiko usiofaa wa Kiingereza na Kiswahili?
 
Endeleeni tu na harakati zenu za kutengeneza lugha mpya toka ubavuni mwa Kiswahili na Kiingereza....
Nilifika mlimani City nikamsikia sharo mmoja anaagiza Sprite, na maongezi yalikuwa hivi;

Mhudumu: Kaka nikuhudumie soda gani?
Sharo: Eeer..mimi..? Ok, Sipo-right (Sprite)
 
Muungwana! Samahani hujajieleza vya kutosha kukusaidia.Neno Mboga laweza kuwa na maana mbili katika kiswahili. Maana ya kwanza ni:matunda au majani ya mmea yatumikayo kama sehemu ya chakula kwa mfano bamia mchicha, ngogwe nyanya nk.Kwa Kiingereza hivi vyaitwa greens au vegetables.Hivi huandaliwa ili viliwe na chaklula kingine kama wali, ugali, viazi, ndizi nk.Ndo maana tunasema mboga ya ugali. Mchicha au ngogwe vikishaandaliwa tayari kuliwa na ugali kwa mfano bado ni mboga tu kwa kiswahili ila kwa kiingerezajina hubadilika.Mboga iliyopikwa kwa ajili ya ugali ikiwemo nyama au samaki inaitwa relish kwa kiingereza. Kwa hiyo muungwana ni hayo tu na bila shaka utakuwa umepata kitu hapo.
 
Sasa hapo SAUSE au SOUP au STEW iko wapi?
Nakubaliana na wanaosema kuwa HAKUNA NENO KAMILI hasa ukichukulia utamaduni wetu na wao.

Nilishaona mtu anakula ugali kwa kutumia tui la karanga na chumvi.

Ngoja tuwasubiri wataalamu wa Kiingereza watakuja na definition nzuri sana kwetu sote.

Nimeona "mboga" kwa maana ya kitoweo/kitoweleo, mchuzi imepewa jina la sauce, soup, stew

Iko na hii pia curry...chicken curry, fish curry..... Curry - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Mimi nina F ya kiingereza lakini nazani hakuna neno la mkato inategemea na mboga iko katika hali gani baadhi ya zinazotumika ni , broth, sauce, stew, curry, etc au kutaja mboga yenyewe direct kwa inavyoonekana mfano meat balls, smoked fish, roasted meat etc.
 
hapa kuna vitu tofauti:
sauce
soup
stew
mboga (kitoweo)
halafu, hivi maharage ni mboga? kuna mtu husema 'maharage ni mboga ya serikali'
 
Hakuna neno mboga km kitoweo in Eng.
Vegetables ni mbogamboga za majani.
Stew and soup ni supu ambazo kwa wenzetu hua ni nzito sio km sisi maji na nyama au kuku au samaki tu na mara nyingi hua served yenyewe tu bila ugali au mkate au wali.
Curry ni chuzi la kukaanga km yale ya kihindi yanotiwa na spices ambayo mara nyingi hua served na wali, ugali au mikate.
So neno mboga halina neno lake in English km ilivo kwa bungo na doriani
 
wadau, habari ya saa hizi, naomba msaada wa neno husika hapo juu kwa kiingereza

Humu ndani kuna vituko!!
Hiyo mkuu
Mboga kwa kiswahili safi ni hiyo wanaita Vegetable kwa kiingereza!! Mboga hii unayozungumzia wewe ni ile kwa kiswahili fasaha inaitwa Kitoweo, Nikosoe kama sijakupata.
soo Mboga ya kwanza = vegetable
Mboga ya pili yaani kitoweo = Side Dish.
these two goes under ile kitu tunaita Noun
utaweza kuipata Mboga pia katika slang za kiswahili kama Adjective, e.g. Mkuu huyu ni mboga (aka Boga) that mean he is weak or soft.
you these words if you need it as adjective!
I hope nimesaidia kidogo. Kumbuka tu misamiati yetu ya kiswahili mingi yake haipatikani katika lugha zingine kama vile maneno ya ukarimu. e.g " pole kwa kufiwa" kiingereza wanatumia "sorry" at the same time they use the same word when they mean samahani!!
sisi tuna 2 different one with each their meaning!
Merry New Year
 
Si kweli. Huwezi kwenda restaurant Magharibi ukakuta choice ya "steak and salad" peke yake! Nyama au mboga za majani always zinakuwa served na french fries, rice, pasta, mashed potatoes, au mkate, why?

Au ushamtembelea mzungu gani ukakuta wamepika li nyama peke yake wanalila na majani?

Concept ya "balanced diet" ambayo tunafundishwa na elimu za wazungu hao hao zinasema chakula shurti kiwe na hamirojo/wanga. Na wanga unaliwa na mboga. Kwa hiyo magharibi mboga ipo!
Nadhani hukunielewa mkuu.
Nimesema hii concept ya ugali/mboga (kitoeo au majani) sio ya ulaya zaidi.
Umesema balanced meal ni hamirojo/wanga... I am sorry, sijaelewa hichi kiswahili, naomba unifafanulie.
Ila ninacho jua kuhusu a balanced meal ni kwamba ukiwa na carbohydrates nyingi, lazima uwe na vegetables nyingi pia. Au ukiwa na proteins nyingi, uwe na vegetables nyingi. Na sio balanced kua na carbohydrates+proteins, bila vegetables.
Kwa hiyo mtu anaweza kabisa kuagiza a steak (proteins) and salad (vegetables), with nothing else, na bado ikawa ni sawa tu.
 
Watu mnabishana juu ya vyakula vya Ulaya wakati watu wenyewe mnashindia mrenda na mihogo.
 
Tunatofautaina sana 'concerpt' ya mlo na Uingereza (na nchi za magharibi)....
Kwetu 'main dish' mara nyingi huwa ni vyakula vya wanga (vyatokana na mchele, mahindi, viazi, ndizi n.k), ila kwa wenzetu mara nyingi 'main dish' inatokana vyakula vya asili ya nyama (ambavyo kwetu ndio mboga)...

Sasa kwa kua lugha haitengamani na tamaduni, hakuna tafsiri ya neno mboga katika lugha hizi (neno kwa neno).

 
... Umesema balanced meal ni hamirojo/wanga... I am sorry, sijaelewa hichi kiswahili, naomba unifafanulie.
Hujui Kiswahili cha hamirojo na wanga, kwani wewe hukwenda shule au umekulia shamba gani huko ambako hamuongei Kiswahili? Sasa sijui tutaendeleaje kujadili wakati mwenzangu lugha yangu huielewi.
 
Hujui Kiswahili cha hamirojo na wangu, kwani wewe hukwenda shule au umekulia shamba gani huko ambako hamuongei Kiswahili? Sasa sijui tutaendeleaje kujadili wakati mwenzangu lugha yangu huielewi.
Sorry. tulikua tunaongea kiswahili ila shule nilienda mimi hatukua tunapewa chakula. Kila mtu anatoka na mitewe nyumbani. kama sio mitewe ni rowe. Unajua mitewe na rowe? lol
 
Sorry. tulikua tunaongea kiswahili ila shule nilienda mimi hatukua tunapewa chakula. Kila mtu anatoka na mitewe nyumbani. kama sio mitewe ni rowe. Unajua mitewe na rowe? lol

Mkuu inaelekea ulikusudia kuandika "Mitebwe" badala ya "Mitewe."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom