msaada '''mboga'' - kwa kiingereza

Kwa kuwa mboga ni kitoweo kinachotokana na kitenzi "kutowea" au "kutoelea" katika maana ya kuchanganya ili kupata ulaini wa kuweza kutafuna ugali na kuumeza kirahisi, basi mimi ningesema kiingereza cha "mboga" ni "mixer". Kumbe unaweza kusema "ugali mixer", wali mixer, nk. ukimaanisha kile unachochanga na ugali au wali ili kuula kwa raha na kwa urahisi. Hivo, mixer yaweza kuwa mchuzi, nyama, dagaa, nk.
 
Ni stew

stew 1 |st(y)oō|noun1 a dish of meat and vegetables cooked slowly in liquid in a closed dish or pan : lamb stew | : add to casseroles, stews, and sauces.

katika michango yote ya members mbalimbali, i think this is the most correct answer.... Thanxx sana mkuu
 
Kwa kuwa mboga ni kitoweo kinachotokana na kitenzi "kutowea" au "kutoelea" katika maana ya kuchanganya ili kupata ulaini wa kuweza kutafuna ugali na kuumeza kirahisi, basi mimi ningesema kiingereza cha "mboga" ni "mixer". Kumbe unaweza kusema "ugali mixer", wali mixer, nk. ukimaanisha kile unachochanga na ugali au wali ili kuula kwa raha na kwa urahisi. Hivo, mixer yaweza kuwa mchuzi, nyama, dagaa, nk.

asante mkuu,,,
 
kitaalamu hasa ukiongelea mambo ya mavyakula, tofauti yetu ni kwenye tamaduni zetu. kama waliowahi kuelezea hapo juu. hakuna neno linalotosheleza kama mboga kwa kizungu, full stop!
wenzetu wana protein badala ya starch kwetu. sauce na sio souce ina maana ni ule mchuzi tu wa chochote kile iwe mboga (yaani vegetables) or any protein source.
kama kuna mwenye tatizo nitarejea kwa maelezo zaidi.
 
katika michango yote ya members mbalimbali, i think this is the most correct answer.... Thanxx sana mkuu

For the sake ya kubishana/ kuelimishana?
Nyama ya kuchoma ni mboga?

Pia kumbuka kun akiingereza cha wale wenyewe wandani, na kuna international English isiyo na mwenyewe, kiswahili nacho ni hivyo hivyo kinapopanuka kinawaacha wale wenyewe na kuwa lugha ya kimataifa, yani kinapita tamaduni tofauti, lazima kusiwe na 'muafaka' sometimes.
Kuna maneno mengi sana 'waingereza' wenyewe hawajui kama ni ya kiingereza, wala hayako kwenye maisha yao, japo utayakuta kwenye kamusi.
Kwa hio kusema kiswahili ni lugha dhaifu, si kweli hata kidogo, bali uelewa/ ufahamu wa mtu mara nyingi ndio unakuwa dhaifu.
wataalamu wa lugha, sio sisi wapitanjia wanakiona kiswahili ni kugha yenye uwezo mkubwa sana, na inauwezo wa kuvuka tamaduni na kutumika kokote, yani ina uwezo wa kukua, na kutosheleza kila inapotaka kutumika.
Tatizo kubwa ni sie KUAMUA kuienzi.
 
Neno stahiki ni "relish"
sio vegetable, maana unapokula wali-nyama, ile nyama ndio mboga yako na si vegetable
 
concept ya ugali/rice/chapati versus mboga (aina yoyote) is not an english concept. ... wanaweza kula steak na salad, vyote ni mboga.
Si kweli. Huwezi kwenda restaurant Magharibi ukakuta choice ya "steak and salad" peke yake! Nyama au mboga za majani always zinakuwa served na french fries, rice, pasta, mashed potatoes, au mkate, why?

Au ushamtembelea mzungu gani ukakuta wamepika li nyama peke yake wanalila na majani?

Concept ya "balanced diet" ambayo tunafundishwa na elimu za wazungu hao hao zinasema chakula shurti kiwe na hamirojo/wanga. Na wanga unaliwa na mboga. Kwa hiyo magharibi mboga ipo!
 
For the sake ya kubishana/ kuelimishana?
Nyama ya kuchoma ni mboga?

Pia kumbuka kun akiingereza cha wale wenyewe wandani, na kuna international English isiyo na mwenyewe, kiswahili nacho ni hivyo hivyo kinapopanuka kinawaacha wale wenyewe na kuwa lugha ya kimataifa, yani kinapita tamaduni tofauti, lazima kusiwe na 'muafaka' sometimes.
Kuna maneno mengi sana 'waingereza' wenyewe hawajui kama ni ya kiingereza, wala hayako kwenye maisha yao, japo utayakuta kwenye kamusi.
Kwa hio kusema kiswahili ni lugha dhaifu, si kweli hata kidogo, bali uelewa/ ufahamu wa mtu mara nyingi ndio unakuwa dhaifu.
wataalamu wa lugha, sio sisi wapitanjia wanakiona kiswahili ni kugha yenye uwezo mkubwa sana, na inauwezo wa kuvuka tamaduni na kutumika kokote, yani ina uwezo wa kukua, na kutosheleza kila inapotaka kutumika.
Tatizo kubwa ni sie KUAMUA kuienzi.

dah, unayoyaongea kweli yana ukweli sana,,, asante ndugu kwa kuendelea kutuelimisha
 
Hivi mie Ngosha nikachukua nyama ya kuchoma, maziwa ya mgando na ugali wangu, si nitasema nakula Ugali kwa Mboga?

Sasa hapo SAUSE au SOUP au STEW iko wapi? Nyama ya kuchoma na mtindi ni STEW?

Nakubaliana na wanaosema kuwa HAKUNA NENO KAMILI hasa ukichukulia utamaduni wetu na wao.

Nilishaona mtu anakula ugali kwa kutumia tui la karanga na chumvi.

Mpare hula ugali kwa SAMAKI ALIYECHORWA Ukutani kama mboga na wakati mwingine wanalowesha maji ya moto Perege ili apate tu radha ya samaki na hapo wanakuwa na SOUP na bado wanaita MBOGA (Jokes kwa shemeji zangu).

Ngoja tuwasubiri wataalamu wa Kiingereza watakuja na definition nzuri sana kwetu sote.
 
inategemea unazungumzia mboga gani. Kama samaki unasema fish mboggar, kama nyama unasema meat mboggar nk

wait a minute.... whaaaaaaaat.. eeeeer. mmmh.... "mboggar". zisi is veri veri interesting..... well i am official quit inglish stadis.. kama ni kuongeza "r" au "s" to kwenye kinglish... bac naenda kudai ada yangu hawawezi kunichakachua c wangesema tu we ongeza "r" katika kila neno...... nahamia kwenye kiarabu na wanakochora maua....... kutoka kushoto kwenda kulia.... au wachora vibox na vijumba vya msonge wachina na japanese
 
Hahahaa, hii imenikumbusha miaka ileeee.............

Mwalimu: Rais wa Kenya anaitwa?
Mtoto: Sijui.
Mwalimu: Anaitwa Kenyatta.
Mtoto: Ohhh, safi sana. Sasa nimeshaelewa, Wa Zambia anaitwa Zambiatta, Uganda anaitwa Ugandattta, Malitta, Senegalitta, Libyatta....

hahahahahahahaaahaha,,, mkuu umetishaa
 
[FONT=arial, helvetica, sans-serif]Nimejaribu kuangalia kwenye TUKI KAMUSI YA KISWAHILI-KIINGEREZA wao wametoa maana tatu ya neno mboga[/FONT]mboga[SUP]1[/SUP] nm mi-[i-/u-] pumkin plant,
mboga[SUP]2[/SUP] nm [i-/zi-] 1. vegetables. 2. relish, side dish.,
mboga[SUP]3[/SUP] kv 1. weak. 2. soft, cheap

Kulingana na swali la mleta hoja hiyo namba mbili inahusika. Sasa kupata uhalisia tuone hayo yaliyoandikwa kwenye namber mbili kwa kiingereza yanaleta maana ya mboga tuijuayo waswahili? Nimeangalia kwenye CAMBRIDGE ADVANCED LEARNER'S DICTIONARY nao wanasema hivi...

1.Vegetable (US INFORMAL veggie) a plant, root, seed, or pod that is used as food, particularly in savoury dishes:2.Relish(SAUCE) a type of sauce which is eaten with food to add flavour to it.

Hiyo ya tau side dish inajieleza yenyewe.Kwangu mimi naona ni sahihi kutumia neno SAUCE huku ukitaja ni sauce ya kitu gani yaani Chicken sauce,fish sauce..... etc
 
MBOGA = VEGITABLE (eg, Spinach<mchicha>, Kisambu cassave leaves>) ====> kiswahili hiki huongelewa visiwani.

MBOGA kama mchuzi = CURRY =====> kiswahili hiki huongelewa sana mainland,

what type of curry it depend on main contents or ingredient of that curry
eg, beef curry, fish curry vegetable curry, etc,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom