Msaada kwa waliochukua malipo ya NSSF hivi karibuni

unakuta wewe ni prof umeingia kazini na non prof.ila jamaa ambae ni non prof akawa analipwa mzigo mkubwa labda kazi yake ni fundi au operator anatumia nguvu nyingi ,at end anatoka na mzigo mkubwa NSSF tena yote .wewe na prof yako unapewa 33% kwa installment
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo

Naomba kuuliza, wiki iliyopita nilirudisha fomu yangu ya madai NSSF na baada ya kufanya uhakiki wao wakanambia kwamba siku flani niangalie kwenye akaunti yangu ya benki nitakuta hela imeingia.

Kwakua mpaka natoka pale na akili nayo ilikua imechoka kiasi kwamba nilisahau hata kuuliza kwamba hiyo hela wataniingiza yote kwa pamoja au ndo yale mambo ya kuingiziana kidogo kidogo ambapo huwezi hata kufanya chochote cha kimaendeleo.

Naomba kwa yoyote humu mwenye uzoefu au ambae amechukua pesa zake hivi karibuni anisadie kunielewesha juu ya hili swali langu.

Asanteni.
Nilirudisha fomu tarehe 28 April juzi 12 may wakaingiza pesa sawa na mshahara wa mwezi mmoja,nimeenda kuulizia Leo wananiambia kuna shida ya mtandao.Mpaka Sasa sijaelewa wamelipa kitu gani.
 
Usitegemee kupata hiyo pesa mwaka huu, nakuhakikishia hilo, usije ukaingia madeni kwakutegemea malipo ya Nssf utaonekana tapeli mtaani.

Nssf hawawezi kukuingizia pesa kwenye akaunti amini ninachokueleza, tarehe waliyokwambia nenda kadai check yako waambie utakwenda kuideposit mwenyewe bank, vna utapigwa kalenda wala check hautopata.

Kama watakuwa wamejirekebisha angalau baada ya miezi 6 ndio utapata hiyo ela, tafuta pesa ya kujikimu kwa sasa usiitegee kabisa hela ya hao mashetani wa Nssf utajuta.
Acha hearsay ,usidanganye watu.
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo

Naomba kuuliza, wiki iliyopita nilirudisha fomu yangu ya madai NSSF na baada ya kufanya uhakiki wao wakanambia kwamba siku flani niangalie kwenye akaunti yangu ya benki nitakuta hela imeingia.

Kwakua mpaka natoka pale na akili nayo ilikua imechoka kiasi kwamba nilisahau hata kuuliza kwamba hiyo hela wataniingiza yote kwa pamoja au ndo yale mambo ya kuingiziana kidogo kidogo ambapo huwezi hata kufanya chochote cha kimaendeleo.

Naomba kwa yoyote humu mwenye uzoefu au ambae amechukua pesa zake hivi karibuni anisadie kunielewesha juu ya hili swali langu.

Asanteni.
Toa pesa upate pesa
 
Ndugu pole huko NSSF kuna changamoto kubwa. Haya mashirika hayana ela ela zao zinaingizwa kwenye makusanyo ya TRA. Utasikia TRA wamekusanya kodi kumbe hakuna kitu kabisa. Huwezi kukusanya kodi kubwa Serikali inashindwa kuwalipa watu mafao yao kwa wakati.
NSSF ukienda kudai mafao kwa utaratibu wao kama una professional unalipwa 33% ya mashahara wako kwa miezi sita. Pesa nyingine iliyobakia utasubirie miezi 18 kama haujapata kazi ndipo utaenda kudai

Kama mashahara wako 500,000 kwa mwezi
33/100*500,000=. 165,000 *6 months = 990,000
Pesa utakayo pewa ya mafao yako ni 990,000

Pesa nyingine utaendelea kusubiria. Inauma kweli kukuta watu waliofanya hii sheria mishahara yao ni million 5, 8, 10
Uko sahihi kabisa....! Na pale sio kiwa ukishapeleka form zako tu basi unapewa next week pana madai mengi tu, watu wanaanza kuchukua pesa wale ww mwanzo kabisa then wanakuja wengine kutegemea na ulileta lini? Haiwezekani wewe wa mwezi wa 5 ukachukua wkt kuna mtu alileta mwezi wa 2.

Lingine kuna mlolongo mwingi sana mpaka uchukue mzigo,stages of verification za kutosha.

Hata ukiwa unprofessional usidhani utakuwa peke yako, sasa usiombe mwajiri wako awe hajapeleka mchango hata mwezi mmoja...basi ili hesabu ziende sawa lazima alete mshiko...sasa kampuni iwe ilishakufa utaomba pooo.

Tumtakie kila la kheri ila pesa ipo cha msingi kila baada ya week 2 tia team tia pressure.

Sent from my SM-J510FN using JamiiForums mobile app
 
Funguwa, Nssf ni mfuko wa private sector.

Ajira yako serikalini haina uhusiano na Nssf na hawana uwezo wa kujuwa hilo, chukuwa pesa yako hata kama itachelewa funguwa madai.
Ukishasema unafanya kazi serikalini au popote sahau kuhusu hayo mafao.
 
Back
Top Bottom