Msaada kwa waliochukua malipo ya NSSF hivi karibuni

Zero Competition

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
307
448
Habari zenu wakubwa kwa wadogo

Naomba kuuliza, wiki iliyopita nilirudisha fomu yangu ya madai NSSF na baada ya kufanya uhakiki wao wakanambia kwamba siku flani niangalie kwenye akaunti yangu ya benki nitakuta hela imeingia.

Kwakua mpaka natoka pale na akili nayo ilikua imechoka kiasi kwamba nilisahau hata kuuliza kwamba hiyo hela wataniingiza yote kwa pamoja au ndo yale mambo ya kuingiziana kidogo kidogo ambapo huwezi hata kufanya chochote cha kimaendeleo.

Naomba kwa yoyote humu mwenye uzoefu au ambae amechukua pesa zake hivi karibuni anisadie kunielewesha juu ya hili swali langu.

Asanteni.
 
Usitegemee kupata hiyo pesa mwaka huu, nakuhakikishia hilo, usije ukaingia madeni kwakutegemea malipo ya Nssf utaonekana tapeli mtaani.

Nssf hawawezi kukuingizia pesa kwenye akaunti amini ninachokueleza, tarehe waliyokwambia nenda kadai check yako waambie utakwenda kuideposit mwenyewe bank, vna utapigwa kalenda wala check hautopata.

Kama watakuwa wamejirekebisha angalau baada ya miezi 6 ndio utapata hiyo ela, tafuta pesa ya kujikimu kwa sasa usiitegee kabisa hela ya hao mashetani wa Nssf utajuta.
 
Shida ninayoiona mifuko yeti hii wanakuwa hawana cash. Fedha zetu wanaziingiza kwenye mizunguko ya Moshe zao...inakuwa kama UPATU vile wanakera sana kungekuwa Hanna sheria nchi hii hawa watu wangesimamiwa na sime milangoni mwao .
 
Usitegemee kupata hiyo pesa mwaka huu, nakuhakikishia hilo, usije ukaingia madeni kwakutegemea malipo ya Nssf utaonekana tapeli mtaani.

Nssf hawawezi kukuingizia pesa kwenye akaunti amini ninachokueleza, tarehe waliyokwambia nenda kadai check yako waambie utakwenda kuideposit mwenyewe bank, vna utapigwa kalenda wala check hautopata.

Kama watakuwa wamejirekebisha angalau baada ya miezi 6 ndio utapata hiyo ela, tafuta pesa ya kujikimu kwa sasa usiitegee kabisa hela ya hao mashetani wa Nssf utajuta.
Wanatoa acha kupotosha ingawa sio wote wanapewa kwa wakati ila unapata ela yako
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo

Naomba kuuliza, wiki iliyopita nilirudisha fomu yangu ya madai NSSF na baada ya kufanya uhakiki wao wakanambia kwamba siku flani niangalie kwenye akaunti yangu ya benki nitakuta hela imeingia.

Kwakua mpaka natoka pale na akili nayo ilikua imechoka kiasi kwamba nilisahau hata kuuliza kwamba hiyo hela wataniingiza yote kwa pamoja au ndo yale mambo ya kuingiziana kidogo kidogo ambapo huwezi hata kufanya chochote cha kimaendeleo.

Naomba kwa yoyote humu mwenye uzoefu au ambae amechukua pesa zake hivi karibuni anisadie kunielewesha juu ya hili swali langu.

Asanteni.
Ndugu pole huko NSSF kuna changamoto kubwa. Haya mashirika hayana ela ela zao zinaingizwa kwenye makusanyo ya TRA. Utasikia TRA wamekusanya kodi kumbe hakuna kitu kabisa. Huwezi kukusanya kodi kubwa Serikali inashindwa kuwalipa watu mafao yao kwa wakati.
NSSF ukienda kudai mafao kwa utaratibu wao kama una professional unalipwa 33% ya mashahara wako kwa miezi sita. Pesa nyingine iliyobakia utasubirie miezi 18 kama haujapata kazi ndipo utaenda kudai

Kama mashahara wako 500,000 kwa mwezi
33/100*500,000=. 165,000 *6 months = 990,000
Pesa utakayo pewa ya mafao yako ni 990,000

Pesa nyingine utaendelea kusubiria. Inauma kweli kukuta watu waliofanya hii sheria mishahara yao ni million 5, 8, 10
 
Ninachoweza kukuambia tu Ni kwamba jiandae kisaikolojia.
Watakua walimuambia urudi baada ya wiki sita. Utarudi utaambiwa wiki tatu, utarudi utaambiwa urudi baada ya wiki mbili. Utarudi utaambiwa anayeshughulikia Yuko likizo Dubai, utarudi baada ya mwezi utaambiwa Facebook ilizimwa siku uliyojaza fom. Utarudi utaambiwa lete picha uliyoleta huku smile. Ukileta picha utaambiwa muhuri hauonekani vizuri Rudi ofisini ukagonge muhuri vizuri utarudi utaambiwa Sasa fomu zako ziko vizuri zimekamilika. Type akaunti namba yako halafu tutakupigia simu.
Cha Msingi watakujaza gesi ili uwatukane.
Kama ulipeleka ubungo kwenye kile kidada sura mbaya na roho mbaya kisicho na utu shauri yako.
 
Ndugu pole huko NSSF kuna changamoto kubwa. Haya mashirika hayana ela ela zao zinaingizwa kwenye makusanyo ya TRA. Utasikia TRA wamekusanya kodi kumbe hakuna kitu kabisa. Huwezi kukusanya kodi kubwa Serikali inashindwa kuwalipa watu mafao yao kwa wakati.
NSSF ukienda kudai mafao kwa utaratibu wao kama una professional unalipwa 33% ya mashahara wako kwa miezi sita. Pesa nyingine iliyobakia utasubirie miezi 18 kama haujapata kazi ndipo utaenda kudai

Kama mashahara wako 500,000 kwa mwezi
33/100*500,000=. 165,000 *6 months = 990,000
Pesa utakayo pewa ya mafao yako ni 990,000

Pesa nyingine utaendelea kusubiria. Inauma kweli kukuta watu waliofanya hii sheria mishahara yao ni million 5, 8, 10
Asante sana kwa taarifa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom