DOKEZO Msaada: Taasisi ya WATED (Women Actions Towards Economic Development) yagoma kutulipa malipo yetu ya kazi ya makala tuliyofanya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Rouhy

New Member
Nov 10, 2022
3
0
Tulipewa kazi ya kufanya makala na Taasisi ya WATED, ambapo ilifanyika mkoani Tanga, na ilitakiwa tulipwe na taasisi ya WATED wakishalipwa na Shirika la OHCHR ( Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights) baada tu ya kukabidhi kazi, na kazi ilikabidhiwa ndani ya wiki moja tukionyeshwa kuwa makala imekubaliwa na OHCHR na malipo yetu yangefuata lakini yapata miezi saba tunazungushwa kulipwa malipo yetu. Tulitumiwa fomu ya malipo tukajaza kwa ahadi kwamba tungelipwa karibuni, lakini haikuwa hivyo.

Na leo 10/11/2022 Taasisi ya WATED wametujulisha kwa barua pepe kuwa shirika la OHCHR bajeti yao haija jumuisha malipo ya makala tuliyoiyandaa ambayo wanaitumia mpaka sasa kwenye kazi zao. Inasikitisha na kuuzunisha Taasisi inayo jifanya kuchochea harakati za wanawake kiuchumi kufanya dhulma kama hii.

Naimani kwa kufikisha hapa taarifa zitawafikia, naomba mtusaidie tupate haki wapenda haki wa jamii forums.

NB: Nimeambatanisha na uthibitisho wa madai haya.
View attachment 2412353View attachment 2412354View attachment 2412358
 
Sana tu! Wanakupa presha ukabidhi kazi kwa wakati lakini kwenye malipo wanakuwa slow, na wengine kama hivi wanakataa kulipa kwasababu zisizo na msingi.
 
Mkataba unasema malipo yafanyike siku tano baada ya kukabidhiwa kazi. Toka mwezi wa 3 tunazungushwa tu.
 
Back
Top Bottom