Msaada kuhusu mtoto kusumbua usiku kucha

Habari.

Nina mtoto wa miezi miwili. Kuna changamoto aliyonayo ya kutolala karibia usiku mzima yaani analala kimagepu huku akiwa hayuko comfortable.

Na akiwa macho hatulii na mama yake pia akimuweka kitandani hataki kukaa peke yake anaanza kulia. Akimpatia pia nyonyo muda mwingine anakataa muda mwingine ananyonya.

Hali hii inatokea pia na mchana.

Msaada kudhibiti hii hali kama umeshawahi kuipitia na mwanao.
Kabla ya kulala muogeshe maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na chumvi kiasi hilo tatizo litakwisha na hata mama yake pia anaweza kuogea
 
Mcheulishe kila akila anaponyonya

Akimaliza kuogeshwa mfanyie massage tumboni na mafuta ya nazi uliyopekecha mikono ili iwe ya moto then unamkanda kanda tumbo.

Mama yake asile vyakula vya gesi aongeze kula matango na matikiti , chakula anachokula mama ndo mtoto ananyonya kama kina acid nyingi mtoto anapata gasi

Mimi nilikuwa pia nikihisi gas nalamba magadi ya mawe kidogo gasi inaisha.
 
Gesi kuna wakati wamama huchoka sanaa aisee so unakuta anampa mtoto usiku nyonyo yeye analala mpaka mtoto ananyonya hewa tu.
1.nunua Grip water hii itamsaidia sana.
2.kama unahisi mambo ya uswahili usipewe dawa yoyote mkate tunywele kidogo kichwani mwake kisha hizo hizo nywele zake mfunge kichwani mwake.
3.Jitahidi kumbeba kwa kumweka begani kusaidia kutoa gesi.
 
Comment number 8 ofuate pia angalia inaweza kuwa joto pia linamsumbua kama ni dsm!!! Miezi ya mwanzo watoto husumbua ni kawaida lkn zaidi muone daktari wa watoto amcheck tumbo!!
 
Gesi inamsumbua
Hili ndiyo la kuzingatia.

Pia mtoto akimaliza kunyonya anatakiwa acheulishwe kwa sababu hawezi kucheuwa mwenyewe bila msaada wa mzazi,mleta mada mama yake aende naye kituo cha afya wamuelekeze namna ya kum-care mtoto ktk uchanga wake.
 
Ni gesi hiyo Mkuu hakuna tatizo lolote hapo na pia mtoto akizaliwa mpaka miezi sita usimpe kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama yake.. akinyonya mpumzishe kama dakika 5 hivi ili ukimuweka begani kumtoa gesi asicheue na maziwa aliyotoka kunyonya...unamuweka begani unatembea nae ndani au unakaa kwenye sofa ila uwe umenyooka mgongo na yeye asipinde akitoa gesi atalala au atataka kunyonya tena ndio maisha yake hayo usimpe kitu kingine zaidi ya maziwa ya Mama yake hata maji asipewe kila kitu kipo ndani ya maziwa ya Mama...
Unaweza kutumia Bonnisan dawa ya India hii akitumia inamsaidia kupata choo vizuri na kutoa gesi pia ingawaje kazi yako ya kumtoa gesi ipo pale pale...
Miezi mitatu ikipita hiyo kazi itakua imeisha pia...
 
Habari.

Nina mtoto wa miezi miwili. Kuna changamoto aliyonayo ya kutolala karibia usiku mzima yaani analala kimagepu huku akiwa hayuko comfortable.

Na akiwa macho hatulii na mama yake pia akimuweka kitandani hataki kukaa peke yake anaanza kulia. Akimpatia pia nyonyo muda mwingine anakataa muda mwingine ananyonya.

Hali hii inatokea pia na mchana.

Msaada kudhibiti hii hali kama umeshawahi kuipitia na mwanao.
Pole kwa shida anayopata mtoto.

Tatizo linalomkabili dogo ni gesi iliyozidi tumboni ambayo anaimeza wakati wa kunyonya maziwa, sababu kubwa inayosababisha mtoto ameze gesi nyingi wakati wa kunyonya ni poor positioning ya mtoto wakati wa kunyonya kiasi cha kusababisha gesi nyingi kuweza kupita mdomoni kwa mtoto na kumsababishia Hali hiyo uliyoelezea.

Cha kufanya
1.Achana na wazo la kumpa gripwater,au sijui maji ya uvuguvugu au chochote kile mbali na maziwa ya mama,kwani utazidisha tuu tatizo na sio nzuri kwa afya ya mtoto mchanga ambae anatakiwa apewe maziwa ya mama tuu kwa muda wa miezi sita ya kwanza ya maisha yake.

2. Hakikisha mama wa mtoto anam position vizuri mtoto wakati anamnyonyesha. Position ya mtoto ikiwa vibaya husababisha gesi kuingia mdomoni kwa mtoto wakati ananyonya na kumsababishia gesi. Angalia video ifuatayo ambayo inaonyesha jinsi ya kumshikilia mtoto vizuri wakati wa kunyonyesha.

View: https://www.youtube.com/watch?v=or4OnMxihUg

3.Kila baada ya mtoto kunyonya na kushiba,mama yake amcheulishe mtoto kwa kumbeba na kuegemeza tumbo la mtoto kwenye bega lake (mama), huku akimgusa mgongoni gently,fungua video ifuatayo kuona jinsi ya kumcheulisha mtoto baada ya kunyonya. Hii husaidia mtoto kutoa gesi ambayo inaweza kuwa iliingia wakati wa kunyonya.

View: https://www.youtube.com/watch?v=m50PTFmmlxw

4. Amfanyie mtoto massage inaitwa "I love you tummy massage" akiona mtoto analia na kujinyonga nyonga na hayuko comfortable. Cheki vide chini hapa kuona namna ya kufanya

View: https://www.youtube.com/watch?v=nUNzi9PYBwc


View: https://www.youtube.com/watch?v=xfGtACWT9ng

Ukifanya kwa usahihi massage hiyo, kama mtoto alikuwa na gesi tumboni,basi utaona anajamba na ataacha kujinyonga na atalala kwa amani kabisa.
Financial Analyst
 
1. Hakikisha ananyonya na kushiba.
2. Mtoe gesi kwa kumbeba begani au mlaze kwenye mapaja kifudifudi baada ya kunyonya
3. Kwa vile hujui ni kiwango gani cha maziwa ananyonya kwenye ziwa. Ni vizuri nyakati za usiku umkamulie maziwa na umfanyie bottle feeding ambapo umnyweshe kulingana na umri wake.

4. Usimvalishe nguo za mpira au za joto hasa msimu wa joto.
5. Asikae na mikojo au kinyesi au uchafu. Kila akikojoa mbadilishe. Ikiwezekana usimvalishe Pampas kama anashinda nyumbani.

6. Kila baada ya siku moja aoge.

7. Mnyooshe viungo.
8. Angalau kwa siku umtoe nje akapigwe na upepo. Akilia.

9. Kabla hajanyonya maziwa hakikisha mamaake ameosha ziwa na maji masafi na kulifuta.
 
Duh mnanikumbusha kuna dogo nae alikua analia hivyo hivyo sasa huyu hata kunyonya hataki (Mtoto wa baba mdogo),kulala halali ucku kucha,ila mchana anauchapa vzr sn,bibi yake alisema mbadilisheni jina tu. Tangu limetekelezwa hilo hajawaji leta shida tena not sure why and what happened to previous name.
 
Mwambie amfanyie tummy time
Anamweka kifuani pake alale hapo mpaka awe fofofo ndo amlaze kitandani
Kumbuka huyo kakaa tumboni miezi 9 na kule kuna joto tofauti na huku alipo sasa
So anapomueka kifuani anafeel safe then anatulia!
Ukitaka kujua kama ni gesi binya tumbo lake kama ni gumu sana mpe infacol kama si gumu usimpe dawa afanye tu hiyo tummy time utaona!
Nami ilimsaidia sana mwanangu now ana 10months
 
Back
Top Bottom