Wadau,
Nina demu mmoja ambae tunapendana sana kwakweli, na nlipanga awe aje my wife wangu hapo baadae. Demu huyu kwa sasa amesafiri hivyo nimebaki mpweke karibia mwezi mzima.
Sasa nikajikuta katika kutafuta mapozeo, nikanasa mahali ambapo kweli nafikiri itakua ngumu kujinasua. Yaani kwa kipindi kifupi tu hapa nliponaswa nishatambulishwa mpaka kwa wakwe zangu, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki.
Kwakua nimeacha u-playboy, najiona kama siwezi kua nao wote wawili, aliesafiri nampenda sana, but najihis usaliti kwake hivyo sistahili kua nae. Najua ataumia, but sina jinsi.
Sasa kumwambia tuachane ndo sijui pa kuanzia. Nafikiria nimtegeshee kosa ili akijichanganya tu nipate sababu but roho inanisuta. Wadau msaada plz