Heshima Mkuu,
kzba .
Pole kwa masaibu yaliyokupata na yanayoendelea kukupata. Nimeona nipitie japo nami nitoe ushauri wangu wa dhati kama mwanaJamii Forums. Nb; Ushauri pia ni sumu usipochanganya na akili yako.
Binti ka-discontinuity College, huwezi tumia busara kuwajuza wazazi lililotokea?. Ukisema umfungulie biashara lengo lako la kuwa un-stressed linaweza lisitimie, You know "Love is a serious mental disease-Plato". If yes, kaa naye chini na umuulize kipi bora.
Hata kwa kuwatumia wazee, watumishi wa Mungu, pande zote za wazazi na kadhalika hudhani kuwa inaweza kusaidia?. Usiseme haiwezekani kabla ya kujaribu, What to fear is a fear itself. Nendeni kwa wazazi na Muombe radhi. Mseme lengo lenu ni binti kurudi chuo na upo tayari kusaidiana nao kulipia gharama za kielimu. Nb; usinijibu, Je ikitokea akaja kugoma kuwa nami..
Kwenda kuueleza hili suala kwa wazazi ni kwa sababu zifuatazo; Wazazi watapiga moyo konde na watatoa nafasi ya pili kwa binti kurudi shule (Things which she's suppossed). Lengo la wazazi lilikuwa binti a-graduate na si vinginevyo. Pia itakujengea wewe uhakika wa kuja kuishi naye then so far kuwa baba bora wa baadaye, If God wishes. Si anakupenda?.
Pia Itawapa wazazi Imani ya kuzidi kuwa bega kwa bega pamoja nanyi japo kosa ni la kishenzi sana (kumradhi), kwani nani asiyekosea?.
Kama una Lengo (si ndoto) na binti, kama bado unapenda kwa dhati basi huu ndiyo wakati ambao unapaswa kuwa naye karibu kuliko siku zingine zilizopita. She's in problem, she need u'r caring, humanity, empathy etc etc.
Masuala ya u-chagga, biashara anaweza, Nani alikuambia biashara ina element na u-chagga?. Tufanye maarifa binti arudi chuo next year If possible. Akishaipata Elimu, urudi na kutuomba tukueleze kiasi cha fedha pamoja na aina ya biashara ya kumfungulia binti (Mkeo mtarajiwa).
Nb; Naomba usimwache binti. Muombeni Mungu na atafanya njia pasipo na njia.
I beg to submit.