Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

Msaada: Gharama za nyumba ya vyumba viwili

Mimi ni mzoefu ..jenga chumba kimoja na choo ..chumba matofali 700 choo matofali 100
 
Bila kuandamana nyumba yako hutaka uione...
 
Hela hiyo unajenga iwapo sehemu ulipo mchanga unapatikana kwa urahisi.
Kuna sehemu nyingine hapa Dar mchanga unaupata kwa sh. elfu 45 kwa gari ndogo.

Chukua mchanga piga tofali, mfuko mmoja wa cement tengeneza tofali 40. Fyatua tofali 800.

Mtafute fundi wa mtaani anachimba na kujenga kwa sh. Laki 2 au 3.
Madirisha nunua mbao na nondo tengeneza mwenyewe madirisha mawili.
Mlango tengeneza mwenyewe mmoja, nunua mbao na misumari tu.
Choo chimba shimo dogo kama futi 6, jengea kwa matofali machache na vipande. Utatumia hata miaka 5, kisha utakuja kujenga cha kudumu.

Kama mchanga ni shida kupatikana au bei ghali, basi nunua tofali jenga chumba kimoja hamia. Mambo ya plasta utapiga wakati umeshahamia.

Usikatishwe tamaa na maneno ya watu eti huwezi, au litakuwa banda! Kumbuka unaanza chumba kimoja kitaonekana kama kibandà lakini baadae utaongeza vyuma vingine taratibu kadiri unavyopata pesa hadi itakuwa nyumba nzuri tu ya kawaida.
Dar ugumu upo kwenye kupata eneo/kiwanja,
Usife moyo.
 
Ingekuewa kwa pesa hiyo unajenga nyumba na unahamia kila mtu angekuwa kwake.
Kumbuka kujenga shida ipo kwenye kupata eneo/kiwanja kwa hapa Dsm.
Huyu mleta mada ana kiwanja chake tayari.
Anaweza kuanza kwa kujenga chumba hata kimoja halafu anamalizia taratibu vyumba vingine hadi nyumba ikamilike.

Akifanikiwa hicho kimoja atakuwa ameokoa pesa ya kulipia pango, ambayo ataitumia kujenga chumba kingine mwaka unaofuata.
 
ahsante sana mkuu umenifafanulia vizur umenipa mwanga kumbe nikisema nitengeneze chumba kimoja kwa hela hii naweza weka had tyres
Hapo kwenye rangi,
Unamaanisha Chumba chenye Magurudumu?

Siku nyingine sema 'Tiles' mkuu.
 
Mln 2 vyumba viwili unajenga bila tatizo...akihitaji mchanganuo naweza kumpa..Narudia msimkatishe tamaa kwa maneno yenu.
Wala usiwe na hasira kwasbb hili ni jukwaa la great thinkers kwahiyo sitegemei km great thinker unilishe maneno matupu. Umeelewa ulichokiandika? Nafikiri hata ww ukisoma baadae utashangaa sana kwa ulichokiandika. Nilitegemea utanipinga kwa fact huku ukitoa mchanganuo wa A-Z kumbe maneno matupu. Nasubiria huo mchanganuo wako
 
ulizia kwanza mwenyewe maana humu kila mtu atatoa uzoefu wake.
ukubwa wa vyuma pia unachangia tofali ngapi.
choo vipi hujengi? hapo pia kuna gharama ya shimo.
mabati, pita uulizie mitaa ya tazara, huwa kuna mabati ya bei rahisi geji za ujanjaujanja.
mbao vipi au utatumia miti/mirunda ulaze bati.
misumari haihitajiki sana,
milango na madirisha vipi, au utatengeneza wa bati,
naona watu wanahamia kachumba kamoja na maisha yanaendelea. tafiti mwenyewe. no gain without pain.

ila ukianza tu kuchimba msingi utafanikiwa mkuu. anza mdogomdogo.
Kwa kifupi kabisa... milioni mbili hawezi kujenga vyumba viwili vikaisha...
 
ahsante sana mkuu umenifafanulia vizur umenipa mwanga kumbe nikisema nitengeneze chumba kimoja kwa hela hii naweza weka had tyres
Mkuu unajenga nyumba au gari? Matairi kwenye nyumba unataka uwe unaenda baa na nyumba yako?
 
Back
Top Bottom