unaweza japo litakuwa banda na sio nyumba ambayo inaweza kukusitiri unahitaji tofari zisizopungua 1200 vyatua mwenyewe kwa kila mfuko tofari 40 unaweza ukagushi mpaka 45 ila maji mengi baada ya kuzivyatua na pia unapojenga saruji iwe kali. mifuko 30 ya cement itahitajika amboyo ni sawa na 360,000/-
utahitaji lory tano za mchanga wastani wa lory moja 120,000/- sawa na 600,000/-
nondo mbili mm12 sina uhakika na bei lakini inaweza kuwa 40,000/-
saruji ya kujengea kila tofari 60 mfuko mmjoa mifuko 20 sawa na 240,000/-
malango weka wa bati kwa dharura na madilisha weka kwanza wa mbao rahisi kila dirisha 30,000 madilisha manne 120,000/-
kitu bati bwana! weka bati la mstaafu gaji 30 au 32 kama zipo kila bati ukizunguka vizuri linaweza kuwa 8000/- unahitaji baji kama 30 sawa 240,000/-
mbao tenga 200,000/-
inabaki laki mbili fundi zinamfaa kabisa mpaka kuezeka.
sasa mafundi karibuni kwa data sahihi ila kwa kifupi unaweza kukamilisha kwa zaidi ya asilimia 75.