Zinatosha sana. Zingatia tu design, isiwe ya kifahari. Simple house.
-Floor design iwe mraba (rectangle) ya 7m × 2.5m. Hii itakupa vyumba viwili vya ukubwa wa 3.3m × 2.5m. Chumba kimoja unaweza kukifanya sebule na kingine cha kulala.
- Ezeka kwa mtindo wa slope.
- Choo kiwe cha nje prefarably cha shimo, bafu na jiko pia la nje.
Nyumba hiyo itakugharimu:
Tofali 19×10 courses × sh 1000 = Sh 190,000/ (hii bila kutoa nafasi itakayoachwa na madirisha na milango.
Bati 9 za 3m × sh 15000 = Sh 135,000/
Mbao za 3 by 2 za kuezekea slope = 18m × 3000 = Sh 54,000/
Jumla kuu hadi hapo ni Sh 379,000/ ya vifaa vya ukuta na paa la bati.
Hivyo hela iliyobaki kutoka hiyo sh 2m itatosha sana kulipa fundi, ujenzi wa msingi, sakafu, madirisha, milango ya kawaida, wiring za umeme na kuweka ceiling bord, kupiga lipu, kupaka rangi na ujenzi wa bafu, choo na mahali pa kupikia chakula! Ukisimamia vizuri utashangaa unaweza baki na chenji ya laki 5.