mh we zunguka bar ya hapo nyuma uyolee machungu tu hiyo pakee yako mkuu.Habari zenu wakuu,,
kwenye shughuli zangu za hapa na pale nimepiga bingo nna milion mbili cash ndan nataka kuondokana na maisha ya kupanga nna kiwanja Goba-Mbezi je ntaweza kujenga vyumba viwil nikaamia kwa gharama ya mill2,,, msaada wenye uzoefu please
hii nyumba hata matombo ipo ila sielewi galama ya ujenzi wake.
Dar es Salaam sehemu gani? Osterbay au huko Uswazi anakopanga huyu jamaa vyumba vya nyuma? Status ya nyumba inategemea na mahali ulipo. Banda la kuku la London ni nzuri kuliko nyumba ya middle class ya mtu wa Dar es Salaam anayeishi Sinza kwa wajanja na inawezekana likawa zuri kuliko nyumba unayokaa. Watu wote hawako sawa ndugu yangu. Hiko unachokiita kibanda cha kuku kwa mwingine ni bonge la bangallow. Kuna maeneo DSM yanayozidiwa na ya Koromije.Hii labda koromije,,,,,darslamu hili ni Banda la kuku.Milioni mbili nilijenga Banda la kuku na bati nilichukua Tazara veterinary.
Ndiyo unaweza. Itakuwa ya tembe na umeme unaweka.Habari zenu wakuu,
Kwenye shughuli zangu za hapa na pale nimepiga bingo nna milion mbili cash ndani nataka kuondokana na maisha ya kupanga nna kiwanja Goba-Mbezi, je nitaweza kujenga vyumba viwili nikaamia kwa gharama ya milioni2.
Msaada wenye uzoefu please
Mkuu vipi hukugusia huduma ya choo, au atumie cha bei rahisi kwenye vichaka???unaweza japo litakuwa banda na sio nyumba ambayo inaweza kukusitiri unahitaji tofari zisizopungua 1200 vyatua mwenyewe kwa kila mfuko tofari 40 unaweza ukagushi mpaka 45 ila maji mengi baada ya kuzivyatua na pia unapojenga saruji iwe kali. mifuko 30 ya cement itahitajika amboyo ni sawa na 360,000/-
utahitaji lory tano za mchanga wastani wa lory moja 120,000/- sawa na 600,000/-
nondo mbili mm12 sina uhakika na bei lakini inaweza kuwa 40,000/-
saruji ya kujengea kila tofari 60 mfuko mmjoa mifuko 20 sawa na 240,000/-
malango weka wa bati kwa dharura na madilisha weka kwanza wa mbao rahisi kila dirisha 30,000 madilisha manne 120,000/-
kitu bati bwana! weka bati la mstaafu gaji 30 au 32 kama zipo kila bati ukizunguka vizuri linaweza kuwa 8000/- unahitaji baji kama 30 sawa 240,000/-
mbao tenga 200,000/-
inabaki laki mbili fundi zinamfaa kabisa mpaka kuezeka.
sasa mafundi karibuni kwa data sahihi ila kwa kifupi unaweza kukamilisha kwa zaidi ya asilimia 75.
Kama ni chumba na "subure" unaweza ila chumba na sebule sahaunataka nyumba ya kawaida tu chumba na subure kama iz tunazopanga mjin
Mln 2 vyumba viwili unajenga bila tatizo...akihitaji mchanganuo naweza kumpa..Narudia msimkatishe tamaa kwa maneno yenu.Kuna mambo mengine haitaji majibu mepesi km haya unayotoa. Hakuna mtu anayemkatisha tamaa bali ukweli ndiyo unaongelewa hapa. Km anataka kujenga nyumba yenye chumba na sebule km bafu na choo inawezekana kbsa tena na chenji inabaki ila km chumba na sebule ile nyumba anayoishi binadamu bado
Ushajiuliza maswali haya?
*Nyumba itachukua matofali mangapi?
*Cement mifuko mingapi?
*Maji
*Mchanga wa kujengea
*Hela ya kuwalipa mafundi day fundi kujenga mmoja ni 25,000-30,000, msaidizi ni 10,000-15000? Kwa mauzo tofauli mmoja ni 250-300
*Itachukua mabati mangapi?
*Hela ya kuchimbia msingi? Hii ni tofauti na ile ya mafundi wa kujenga tofali
*Kuweka vifusi ndani
*Bado plaster km atapiga (nayo inahela yake) hapa mafundi lazima uwalipe
*Mafundi wa kupiga bati nao wanahitaji hela
*kupiga floor chini
Swali
1. Hiyo 2M inatosha?
Km itatosha nakupa 2M tunaandikiana mkataba kbsa unajengee nyumba ya chumba na sebule mm nakuja kuhamia tu. Ukishindwa unabid unilipe milion 6 jumla milion 8 km usumbufu
Aisee...I luv JFlabda choo peke yake
hahahaAisee...I luv JF
Labda kweli ngoja nipige hesabu ya choo/bafu cha kawaida
Choo na tank 180,000
Sink na mguu wake 150,000
Taps 50,000
Shower kit 150,000
Tiles 120,000
Tiles ukutani 120,000
Hapo tayari kama 700,000
Bado matofali,cement,bati,mbao,kokoto
Ha ha ha hakama wewe ni fundi matofali ya udongo kuna maji karibu bati na mbao utatumia fito inawezekana